Sinkala (JF Member) kuoa karibuni!

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Kwa wale mlio Dar na wale ambao mngependa kushirikiana na mwenzetu...

Kuna mwenzetu (Sinkala) anatarajia kufunga ndoa mwezi huu.

Kwa wale ambao wangependa kushirikiana katika kuiwakilisha JF ama kushirikiana na mwenzetu katika hali na mali tuwasiliane via PM ili niwape mwongozo wa huyu mwenzetu.

Aidha unaweza kuwasiliana na Maxence via +255713444649.

JF itatoa zawadi yake katika harusi hii. Ushirikiano wenu unakaribishwa sana.
 
Kila la kheri Sinkala, Mungu awatangulie katika maandalizi yenu ya ndoa takatifu.
Umefanya uamuzi wa maana wa kuoa.
Apataye mke, amepata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana.
 
Congrats Sinkala. Mods can we possibly get pics & vids of the occasion? Kama Mr. Sinkala will approve.
 
Hongera kijana Sinkala kwa kuuvua ukapera na kupata Jiko umetuonyesha njia na sisi tutakufuata punde. Kila la kheri mkuu.
 
Hongera sana Sinkala

Kila la kheri na Mungu awatangulie kwa kila mipango na maisha kwa ujumla
 
Hongera kijana Sinkala kwa kuuvua ukapera na kupata Jiko umetuonyesha njia na sisi tutakufuata punde. Kila la kheri mkuu.

yaani ya kwako hata kama nikiwa wapi kama ukihabarisha mapema muhimu nihudhurie...lol naisubiria kwa hamu!....kila la kheri Sinkala.
 
Hahaha Nyamayao subili utaarifiwa tu hapa hapa tena manaake itakuwa bab kubwa....nitafunika mbona.
 
Nasita kukupa hongera.....unatafuta kero kuowa mazee, uliza waliowa wakuambie ukweli....naona wengi tunasepa hicho kipengele....kwanini msiishi pamoja tu....na hata watoto mkazaa kuliko kujivalisha pingu?

Hongera basi kwa kuwa wengi wamekuambia ila I have warned you with your decision in the first place

Mas
 
Duh Mkuu Sinkala umekubali kuuza uhuru wako?
Ila hongera sana, is one step forward
 
Nasita kukupa hongera.....unatafuta kero kuowa mazee, uliza waliowa wakuambie ukweli....naona wengi tunasepa hicho kipengele....kwanini msiishi pamoja tu....na hata watoto mkazaa kuliko kujivalisha pingu?

Hongera basi kwa kuwa wengi wamekuambia ila I have warned you with your decision in the first place

Mas

Kubwa ni hii ya kuwahi kurudi home, umechelewa sana saa tatu
 
Haya luv bado nipo kwenye mchakato wa kumpata manaake kufunga PINGU za maisha si mchezo kuna milima na mabonde itabidi nivuke.

Project 2012 sio Fidel80

Kuoa nyie kazi wacha kabisa
 
Nasita kukupa hongera.....unatafuta kero kuowa mazee, uliza waliowa wakuambie ukweli....naona wengi tunasepa hicho kipengele....kwanini msiishi pamoja tu....na hata watoto mkazaa kuliko kujivalisha pingu?

Hongera basi kwa kuwa wengi wamekuambia ila I have warned you with your decision in the first place

Mas

Mkuu Mas. Heshima mbele.
Unaongea kwa uzoefu au hisia. Na kama kakwambia mtu umeuliza na wengine? Labda nikupe uzoeafu wangu. Kwa ufupi, "getting married is of the great decison I ever made in my life. I will never regret"!! Ila kila mtu analo lake ni si lazima aseme kama mimi!:rolleyes:
 
Kwa wale mlio Dar na wale ambao mngependa kushirikiana na mwenzetu...

Kuna mwenzetu (Sinkala) anatarajia kufunga ndoa mwezi huu.

Kwa wale ambao wangependa kushirikiana katika kuiwakilisha JF ama kushirikiana na mwenzetu katika hali na mali tuwasiliane via PM ili niwape mwongozo wa huyu mwenzetu.

Aidha unaweza kuwasiliana na Maxence via +255713444649.

JF itatoa zawadi yake katika harusi hii. Ushirikiano wenu unakaribishwa sana.

Mkuu nifikishie salamu zangu kwa kijana Sinkala zenye kumtakia kila la heri. Huu ni uamuzi unaofanywa na watu wachache kwa hiyo big up! Asimsikilize mtu, moyo wake tu. Sisi twaweza kumpa uzoefu tu lakini yeye asonge mbele. Kama ningeweza, basi siku hiyo ningekuwepo ili nimuume sikio na kumwambia kuwa saa yake ya ukombozi ni saa hiyo hiyo anapoachana na maisha ya kutanga tanga kama ndege. Mwambie apige kwata na kusonga mbele. Asimtishe mtu ila asiende kufanya majibio. Afanye kweli (huyo mdogo wangu) ili aingie kwenye orodha ya wanaume (na baba) wachache tuliobaki kwenye hii dunia ya vichaa wa utandawazi!!
 
Mmmmhhh!!! ambao hamjaoa mmetukanwa na Dark City kwenye hii post yake, isomeni kwa makini
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom