utantambua
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,367
- 321
Waungwana,
Mtaniwia radhi. Hivi kweli kama sisi ni watu makini, kwa nini tunajisumbua kulalamika kuhusu kushindwa kwa TANESCO kumaliza tatizo la mgao wa umeme? Kwani nani alisema kwamba TANESCO peke yao ndio wenye dhamana ya kuzalisha umeme? Kwani nani amekuzuia wewe kuweka mtambo wa wind power, au solar power, nyumbani kwako, ukaachana na huo mgao?
Jamani, kama sisi ni watu makini, tutajua kwamba ni kazi bure kuilalamikia Serikali na TANESCO. Dawa ni (1) funga mtambo wako mwenyewe wa umeme nyumbani, kama ni wind, solar, bioga, etc., kisha (2) ng'oa kabisa service line ya TANESCO, ili uachane na dhana kwamna TANESCO ni kampuni ya kuzalisha na kusambaza umeme, kwani hilo si kweli.
Hata kufikiria mambo madogo kama haya, tunaiachia Serikali? Ujinga huu!
Samahani kwa kuwaambia ukweli lakini TANESCO SIO SOLUTION ya kumaliza mgao wa umeme, na hata Serikali pia, haina nia hiyo.
Umemaliza?