Singita Grumeti Reserves named as one of the World's Top Hotels

Huyu jamaa ni mtoto wa mmoja wa waanzilishi wa Dow Jones Indexes. Hii kitu ilianzihswa kama sikosei na Babu yake aitwaye Edward Jones pamoja na jamaa wengine wawili, Charles Dow na Charles Bergstresser.

Kwa hiyo, duniani, jina JONES ni kubwa sana kwenye ulimwengu wa wauzaji na wanunuaji kwenye minada.

Watu huwa wanasifu ile hotel ya Dubai kuwa ni aghali ila ukweli hizi hoteli (Apartments) za jamaa zinaweza kufika hadi $12,000 kwa siku moja. Ila ukifika hapo, basi kila mtu ana mhudumu wake. Hata kama una kitoto, kitoto kinakuwa na mhudumu wake. Sijui kwa chakula pakoje ila ninavyofahamu, Burj Al Arab ukiacha bei, wana sifa moja kubwa sana, pale utapata chakula chochote unachotaka kama umefikia sehemu ya bei mbaya.
Hii ina maana kuwa, ukifika pale uagize ugali kwa Bamia, basi watatuma wanunuzi wakanunue bamia sehemu ya karibu na kuzituma kwa ndege na unga wa mahindi. Ugali utaletewa na bamia zako. Hii ina maana kwa vyakula vya kawaida hata kama ukitaka Mtori, pia wanaweza kukutengenezea. Sijui kama kisusio wataweza :)

Mkuu Mr Rocky

Nakubaliana na hoja yako kwamba Singita inaweza kuwa ya South Afrika na ni waendeshaji tu wa hizo Lodge.

Bwana Paul Jones ni mtu wa 336 kwa utajiri duniani anamiliki pia kampuni ya Tudor Investment ya huko USA,Bwana Paul Jones anakisiwa ana utajiri wa 3.3 bilion U$.
 
Mkuu Nyandaigobeko nakubaliana na tafsiri yako
Ila ukija kwenye Kanuni zinazotambua maeneo hayo zinataja wazi wazi kuwa ni hifadhi ya wanyamapori
Yaani kanuni za Hifadhi ya Wanyamapori (Maeneo ya Hifadhi za Wanyamapori) za mwaka 2005 japo kuna Kanuni mpya za mwaka 2009 ambazo bado hazijaanza kutumika.
Japo kanuni zinasema ni hifadhi ya wanyamapori ila zinasema wazi kuwa ndani ya maeneo hayo unaweza kufanyika utalii wa matumizi na usio wa matumizi yaani consumptive and non consumptive wildlife utiilization

GR kwa upande wao wanaendesha utalii wa matumizi kw akiwango kidogo sana maana lengo la PTJ ni kuona idadi ya viumbepori inaongezeka katika eneo hilo na kwa hilo wamefanikiwa sana
 
Asante sana kwa sahihisho Mkuu.

Mkuu. Asante kwa habari hii.

Lakini nikusahihishe, kurya sio kabila ambalo linapatikana sana karibu na maeneo ya Grumeti Game Reserve na Ikona WMA. Waikoma na wasenye ndio wanapatikana sana; tena waikoma wakiwa ndio wengi. Haya makabila ndio yana ugomvi sana TANAPA (kwa upande wa SENAPA eneo hilo; na hiyo kampuni ya bwana Paul Jones.
 
Hapo ndipo penye shida, kama kanuni zinakua zinakanganya mambo hivyo, ndio maana WMAs (hususani Ikona, Enduimet na ipo pale Tarangire (jina limenitoka, lakini lina asili ya kimaasi) zinakua zina migogoro isiyoisha. Pamoja na mapungufu mengi ya kanuni za WMA; hilo la kusema WMA ni sawa na hifadhi ya wanyamapori ni grave mistake katika suala zima la uendeshaji na usimamizi wa WMA.
 
Daaah ni kweli mtupu...mimi nilipata bahati ya kufika grumet kikazi...daah wale jamaa wako juu kinoma, kwanza ndege ya kutoka arusha mpk grumet ni usd400. Pia misosi yao ni noma wanapika fresh na wafanyakazi wao(wabongo) wanalipwa hela nzuri na wanalishwa vizuri sna...nilipewa ride ya siku mbili bure pamoja na kulala rum ya usd500 per night. Ni wakarimu sna...mmlliki wake ambae ni best ake g.bush huja mara moja kwa mwaka kufanya uwindaji akiwa na rafiki zake...akija vijana wote huwa na furaha ya hatari huwaletea zawadi mbalimbali na sherehe nyingi tu. Pia ndio mbuga ambayo wanyama ni rafiki wa binadam....yani unadrive kumfwata simba wala hakimbii na wala hakutishi they are human friends hicho nacho kinaipandisha hadhi ile mbuga na vyote vilivyomo humu.
 
Mkuu historia ya hapa ni kubwa sana na kwa kweli ukienda kwa mfano maeneo ya robanda kile kijiji kimezungukwa na maeneo ya hifadhi katika pande zote
Kuna Ikorongo Game Reserves, Serengeti National Park na Ikona WMA
Kwa hiyo kijiji kiko ndani ya maeneo ya hifadhi
Historia ya hapa mkuu ni ngumu sana na ni kubwa sana na ndo maana kuna chuki za chini chini baina ya GR na SNP na wakazi wa hapa haswa masuala ya mipaka na maeneo ya wafugaji
 
Mkuu nafikiri maana nzima ilikuwa ni hifadhi kwa maana kuwa uwe ni ule utalii usio wa matumizi
Ila walipoingiza kipengele cha utalii wa matumizi wanaharibu maana nzima ya hifadhi ya viumbepori
Inakuwa sasa ni kuwa maeneo hayo pia yanaweza kuwa kitalu na WMA husika ikawa na mgao wake kutoka Idara ya Wanyamapori kwa ajili ya uwindaji wa kitalii na ule usio wa kitalii (residence hunting)
 
Mkuu ni normal behaviour kwa wanyamapori ambao wanakua treated friendly. Lakini kama wanyamapori wanakua treated aggressively (kupitia uwindaji husio na mipaka, mitego, milio ya risasi n.k.), nao wanakua aggressive; kwani ubadili tabia kutokana na mazingira wanayoishi.
Ila kama kuna uwindaji maeneo hayo, halafu simba wanakua wapole hivyo, basi nafikiri hii ni interesting case, ambayo it could make a good research hypothesis! (labda kama wawindaji wanawinda maeneo ambayo simba hayupo, nikimaanisha maeneo ya malisho ya simba).
 
Daaah ni kweli mtupu...mimi nilipata bahati ya kufika grumet kikazi...daah wale jamaa wako juu kinoma, kwanza ndege ya kutoka arusha mpk grumet ni usd400. Pia misosi yao ni noma wanapika fresh na wafanyakazi wao(wabongo) wanalipwa hela nzuri na wanalishwa vizuri sna...nilipewa ride ya siku mbili bure pamoja na kulala rum ya usd500 per night. Ni wakarimu sna...mmlliki wake ambae ni best ake g.bush huja mara moja kwa mwaka kufanya uwindaji akiwa na rafiki zake...akija vijana wote huwa na furaha ya hatari huwaletea zawadi mbalimbali na sherehe nyingi tu. Pia ndio mbuga ambayo wanyama ni rafiki wa binadam....yani unadrive kumfwata simba wala hakimbii na wala hakutishi they are human friends hicho nacho kinaipandisha hadhi ile mbuga na vyote vilivyomo humu.

Safi sana kama ulipata huduma nzuri na za kuridhisha
na mengi uliyoyaona ni real na ni eneo ambalo kweli unaweza kwenda kupumzika ukiwa na ukwasi wa kutosha maana huwezi kwenda na pesa kidogo na ukategemea kwenda kupumzika maeneo kama Sasakwa
 
Mkuu historia ya hapa ni kubwa sana na kwa kweli ukienda kwa mfano maeneo ya robanda kile kijiji kimezungukwa na maeneo ya hifadhi katika pande zote
Kuna Ikorongo Game Reserves, Serengeti National Park na Ikona WMA
Kwa hiyo kijiji kiko ndani ya maeneo ya hifadhi
Historia ya hapa mkuu ni ngumu sana na ni kubwa sana na ndo maana kuna chuki za chini chini baina ya GR na SNP na wakazi wa hapa haswa masuala ya mipaka na maeneo ya wafugaji

Inasemekana kuna imani pia za kimungu hapo ambazo jamaa (haswa waikoma) waliona uhifadhi unaingilia imani yao. Wana mungu wao mmoja hivi (jina limenitoka), lakini hii nayo ni moja ya sababu ya mfarakano huo.
 
Mkuu hii sijawahi sana kukaa na Waikoma nikaiuliza
Ila ugomvi mkubwa ni mipaka maana mwaka juzi ilibidi Idara ya wanyamapori ije iweke mipaka upya ya Ikorongo Game Reserves maana ilichukua maeneo ya kijiji cha park Nyigoti
 
Mkuu nafikiri maana nzima ilikuwa ni hifadhi kwa maana kuwa uwe ni ule utalii usio wa matumizi
Ila walipoingiza kipengele cha utalii wa matumizi wanaharibu maana nzima ya hifadhi ya viumbepori
Inakuwa sasa ni kuwa maeneo hayo pia yanaweza kuwa kitalu na WMA husika ikawa na mgao wake kutoka Idara ya Wanyamapori kwa ajili ya uwindaji wa kitalii na ule usio wa kitalii (residence hunting)

Mkuu uhifadhi bila significant and direct benefits kwa adjacent communities unakua na maana gani?!?
Hawakukosea mkuu. Kwani waliona kwa kuongeza kipengele cha matumizi, watazivutia adjacent communities katika ushiriki wao wa kuhifadhi hao viumbe. Kwani bila kuwashirikisha mkuu, ndio mambo ya poaching and the like yanaongezeka sana.
Kwa hapo Ikona WMA na Grumeti GR aisee kuna mambo mengi sana ambayo bado hayajajulikana. Ingawa kama nilivyosema awali, kanuni za WMA bado zina mapungufu mengi sana, na hayo ndio yanapelekea mifarakano kwenye WMAs hisiishe.

Mfano suala la mgawanyo wa mapato wa asilimia 25 kwenda kwa hiyo respective WMA, bado una shida, kwani mapato hayo uwa yanaisha kuliwa na AA (Authorised Association) kupitia ile uitwa "elite capture". Kwa hiyo unakuta wanakijiji wa kawaida hawaoni faida; hapo ndipo upeleka hasira zao kwa viumbepori na kuleta mifarakano na TANAPA na wadau wengine (kwa case hii Grumeti GR na Singita). Kuna study moja inafanyika sasa "protected area and poverty reduction" na Ikona ni moja ya study site; natumaini inaweza kuja na majibu mengi.

Lakini kwa ujumla mkuu, uhifadhi bila ya adjacent communities kupata na kuona faida za uhifadhi ni vigumu sana kufanikiwa. Ndio maana katika mbuga za taifa; kuna kitu inaitwa CCS (Community Conservation Services), hii ni katika kuhakikisha adjacent communities zinaona na kupata faida za uhifadhi. Sasa katika kuhakikisha faida zaidi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo, ndio suala la WMA likaanzishwa.

Mkuu huwezi amini wamaasai waliokua wakipinga sana suala la WMA (wakiamini wao hawahitaji kufundishwa namna ya kuishi na viumbepori, kwani wameishi navyo enzi na enzi), lakini kutokana na kero za uhifadhi kuzidi na maeneo zaidi kutengwa kama ushorobo "wildlife corridors" (naongelea Loliondo GCA, vijiji vya Ololosokwani, Soitsambu, Losoito Maaloni na Oloirien Magaiduru), wamaasai sasa wanalilia WMA.
 
Mkuu. Asante kwa habari hii.

Lakini nikusahihishe, kurya sio kabila ambalo linapatikana sana karibu na maeneo ya Grumeti Game Reserve na Ikona WMA. Waikoma na wasenye ndio wanapatikana sana; tena waikoma wakiwa ndio wengi. Haya makabila ndio yana ugomvi sana TANAPA (kwa upande wa SENAPA eneo hilo; na hiyo kampuni ya bwana Paul Jones.

Mkuu maelezo yako yako sahihi.

Ningetaka kuweka rekodi vizuri kidogo. Maana hapa nina maslahi, ndipo nyumbani kwangu-kama ni mwenyeji nyumbani kwangu ni Kibeyo.

Kwanza marekebisho madogo, ni Ikoma , sio Ikona, Ikoma ikiwakilisha eneo la nyumbani kwa waikoma!!

Hizi hoteli na lodges zimepakana na wakurya kwa upande mmoja na waikoma/wanata/waisenye kwa upande mwingine.

Kama utakuwa na kumbukumbu ya wananchi wa kijiji cha nyamuma kuchomewa nyumba zao na serikali chini ya usimamizi wa mkuu wa wilaya enzi hizo bw. Thomas Sabaya na OCD Lyimo, sababu pekee ilikuwa ni kupisha uwekezaji huu wa Grumeti Reserves Ltd.

Kuna vijiji kama Nyamuma, Bonchugu,Kebosongo, Rwamchanga, Miseke, Tabora B, Guruneti, Bisarara, Nyambuli na Mbalibali vyote hivi viko katika eneo la Grumet Game Reserve. Vijiji vya Ikoma Robanda, Bwitengi, Natabigo, Nyakitono, Nyichoka, Fort Ikoma, Isenye na kuendelea kuelekea vijiji vya wilaya ya bunda vipo kwenye eneo la Ikoma WMA, na hivi vyote ni waathirika wa huu uwekezaji.

Hivi vijiji vyote vilivyoko katika Ikoma WMA, Grumet Game reserve na Ikorongo game reserve(mara nyingi game reserve za Ikorongo na Grumet huunganishwa pamoja kiutendaji-na hivyo kujumuisha vijiji vingi zaidi) vimepakana na Serengeti national park. Na kwa asili na tabia ya wanyama aina ya nyumbu(wilderbeest) ambao huhama hama kutoka serengeti national park kwenda maasai mara kenya na kisha kurudi, hulazimika kupita katika makazi ya watu. Na kwa asili wakurya, waikoma, wanata na waisenye ni wawindaji pamoja na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji. Chakula chao kikuu ni ugali nyama na maziwa, na hapa nyama pori nayo huliwa sana.

Hawa wawekezaji walivyoingia, wakajitengenezea jeshi lao kwa kuajiri vijana na kuwapa mafunzo ya kijeshi. Kazi yao ya kwanza na ya umuhimu wa kipekee ilikuwa kudhibiti ndugu zangu wasile nyama pori. Vijana walikuwa wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba kukamata nyama pori, na kikubwa zaidi walikuwa wanwadhalilisha sana wananchi, kwa kupewa support na uongozi wa wilaya na jeshi la polisi. Kitu kingine ambacho kilianzisha ugomvi na bado upo kati ya hawa wawekezaji na SENAPA kwa upande mmoja dhidi ya wakurya(kwakuwa ndio wafugaji-wenye mifugo wengi kuliko waikoma na waisenye) kwa upande wa pili ni suala la kukamatwa, kufilisiwa kwa mifugo ama kufungwa jela kwa wananchi inapotokea mifugo yao imeingia ndani ya eneo la WMAs na GRs.

Na kitu kingine ambacho ni common kwa maeneo yote ya uwekezaji nchini Tanzania ni suala la ajira, ni wazawa wachache sana waliobahatika kupata ajira katika uwekezaji huu. Walio na nafasi nzuri za maslahi ni wageni, has toka nchi jirani. Hata ukorokoroni ambao vijana wetu wa kikurya wanaweza kuufanya kwa umahiri sana nao wanapewa "wakuja". Sasa wakiingia mugumu hawa watu mwisho wa mwezi wanasumbua sana, "dada zetu" hawalali majumbani kwao!!
 
Mkuu hii sijawahi sana kukaa na Waikoma nikaiuliza
Ila ugomvi mkubwa ni mipaka maana mwaka juzi ilibidi Idara ya wanyamapori ije iweke mipaka upya ya Ikorongo Game Reserves maana ilichukua maeneo ya kijiji cha park Nyigoti

Hiyo ni kweli kabisa. Suala la mipaka ni moja ya vyanzo vya mifarakano katika maeneo ya uhifadhi (iwe wa viumbepori na hata misitu). Tatizo hapa pia linaenda kwenye mamlaka kuignore mipaka ya wananchi. Hifadhi zote hapa nchini (ukitoa za visiwani, ambazo mimi naziona ni kama sanctuaries tu) zimeanzishwa mahala ambapo wananchi walikua wakiishi. Hivyo kwenye suala la mipaka, interests za wananchi zingepaswa ziwe priority ya kwanza. Tatizo hapa linakuja, kwa mamlaka hizo kuamua kinyume na hapo (hivi kuna haja gani ya kuwa na walinzi wenye silaha za kivita; kama mamlaka zingekaa chini na kusikiliza na kutekeleza matakwa ya wananchi?!?)

Pia kuna suala la wanakijiji kutoka kwenye vijiji vya jirani kuajiriwa kwenye SENAPA na Grumeti GR. Jamaa wanasema hawapewi sana nafasi za ajira huko. Pia suala la faini kwa mifugo inapokutwa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kuchunga; faini ni kama kukomoana. Faini ya ths. 5,000 hadi 10,000 kwa mfugo mmoja kwa mwanakijiji kweli mkuu ni haki hiyo!? Haya yote yanachangia sana mifarakano kama hiyo kuendelea.

Hapa mkuu, tatizo ni hao wanyama kupewa priority kubwa kuliko adjacent communities. Na hii imekua hivyo toka enzi za ukoloni. Too bad kwamba hizi the so called people centred approach to natural resources management bado zina elements za fences and fines approach. Na hii ndio imepelekea kwa kiwango kikubwa sana mifarakano kuendelea mpaka leo.
 
sasa huu utalii wa ndani tunaoamasishwa tulale kwenye magari? embu naomba nitajieni hotel za bei rahisi huko mbugani ambazo wakina sisi tunaweza kulala?
 
Mkuu MM.

Maneno mazito sana nimesoma mara mbili mbili nikajikuta najichukia mwenyewe kwakuwa mTanzania.

Mkuu nakushukuru sana kwa maelezo murua kabisa.

Serikali kushindwa kuheshimu mahitaji ya wanadamu na kuweka mbele maslahi ya wanyamapori limekuwa ni tatizo kubwa sana.

Suala la mipaka nalo ni big issue, kuna watu wamehamishwa toka maeneo yao ya asili, kwa nguvu na kwa kunyanyaswa, kijiji cha nyamuma ni kesi ya hivi karibuni. Lakini haya maeneo ya WMAs na GRs ni maeneo ambayo mababu zetu wameishi miaka na miaka. Mimi binafsi niliwahi kuishi Kijiji cha nyamuma nikifanya shughuli za kilimo, niliposikia kijiji hicho kimechomwa moto na serikali na jamaa zangu niliokua nao nikasoma nao wakafukuzwa na kuambiwa sio watanzania nilisikitika sana. Hata shule zilizokuwa zimejengwa maeneo hayo nguvu zote na rasilimali walizojitolea wananchi zikawa zimeteketa siku moja tu.

Sidhani kama kuna sababu yoyote ya kuwa na hizi WMAs na GRs ambazo hazishirikishi kikamilifu wananchi, ama wananchi hawaoni matunda yake, ama maeneo yao ya kufanyia shughuli zao za kimila kuvamiwa, kuharibiwa, kuzuiliwa kuingia ama kuhamishwa. Kwa mfano ndugu zangu waikoma wana eneo lao maarufu sana la kufanyia mitambiko yao(ni haki yao maana ndio imani yao) wanapokwenda kukutana na mungu wao Machaba. Sasa inapotokea serikali inamkabidhi mwekezaji eneo muhimu sana kwa shughuli za hawa wananchi inasikitisha sana, na kwa hali kama hiyo huwezi kutarajia wananchi hao watoe ushirikiano wa kutosha kwa mwekezaji ama serikali kwa maana ya serengeti national park.
 
Asante kwa nyongeza mkuu.

Kwanza nami nikurekebishe. Ingawa wewe ni mwenyeji wa huko, hiyo WMA ya hapo inaitwa IKONA WMA na siyo IKOMA WMA. Hilo ndio jina linalojulikana kiserikali na kiutawala. Sijakataa, pengine nyie huko mnaliita IKOMA WMA.

Hilo ndilo moja ya matatizo niliyokua nikimwambia Mr. Rocky; serikali badala ya kusikiliza na kutekeleza matakwa ya adjacent communities, yenyewe inasikiliza na kutekeleza matakwa ya wageni wenye interest ya kuona viumbepori vinalindwa kwa any means ili kuattract wageni kwenye investments zao!! Na hiyo imekua hivyo toka enzi za mkoloni; no wonder sasa inasemwa tuna wakoloni weusi!!

Kwani mbona hao waikoma, wasenye na wakurya wameishi na huyo viumbepori enzi na enzi?! What's the fuss sasa baada ya mzungu kutaka masilahi yake yapewe kipaumbele?!? Huo utaratibu walioutumia na wanaendelea kuutumia hautakaa kamwe kuna na manufaa kwa pande zote. Kwani vijana wa kiikoma, kisenye na kikurya nao watataka kurevenge; na mbaya zaidi wanarevenge kwa viumbepori ambavyo wanafahamu fika kwamba hao wazungu ndio wamevitolea macho. Kwa hiyo hapo inakua jino kwa jino!!
 
Mkuu MM.

Maneno mazito sana nimesoma mara mbili mbili nikajikuta najichukia mwenyewe kwakuwa mTanzania.

Ngongo,

Mkuu hii nchi ni yetu lakini tumeshaporwa na wachache miongoni mwetu.

Huwa nashindwa kuelewa hawa viongozi wetu wanapokuwa wanaingia mikataba mbalimbali kama hii ya uwekezaji ndani ya serengeti national park huwa wanawaza nini juu ya wananchi.

Katika hali kama hii migogoro baina ya wawekezaji, serikali na wananchi haitaweza kwisha, itabaki kuwa sehemu ya maisha.

Fikiria kuna mgao wa 25% ambazo zinatakiwa ziende kwenye halmashauri husika kwa ajili ya kuchangia shughuli za maendeleo lakini hazionekani matunda yake kwa wananchi. Bila shaka hapa kuna kamchezo kati ya wawekezaji na uongozi wa halmashauri.

Pia kuna majukumu ya hawa wawekezaji kwa jamii na vijiji vinavyowazunguka lakini hawatekelezi hiyo corporate social responsibility. Utashangaa hoteli zinaingiza fedha nyingi lakini vijiji jirani viko katika hali mbaya katika huduma ya afya, elimu, maji na miundombinu.
 
Mkuu nakushukuru sana kwa maelezo murua kabisa.

Serikali kushindwa kuheshimu mahitaji ya wanadamu na kuweka mbele maslahi ya wanyamapori limekuwa ni tatizo kubwa sana.

Suala la mipaka nalo ni big issue, kuna watu wamehamishwa toka maeneo yao ya asili, kwa nguvu na kwa kunyanyaswa, kijiji cha nyamuma ni kesi ya hivi karibuni. Lakini haya maeneo ya WMAs na GRs ni maeneo ambayo mababu zetu wameishi miaka na miaka. Mimi binafsi niliwahi kuishi Kijiji cha nyamuma nikifanya shughuli za kilimo, niliposikia kijiji hicho kimechomwa moto na serikali na jamaa zangu niliokua nao nikasoma nao wakafukuzwa na kuambiwa sio watanzania nilisikitika sana. Hata shule zilizokuwa zimejengwa maeneo hayo nguvu zote na rasilimali walizojitolea wananchi zikawa zimeteketa siku moja tu.

Sidhani kama kuna sababu yoyote ya kuwa na hizi WMAs na GRs ambazo hazishirikishi kikamilifu wananchi, ama wananchi hawaoni matunda yake, ama maeneo yao ya kufanyia shughuli zao za kimila kuvamiwa, kuharibiwa, kuzuiliwa kuingia ama kuhamishwa. Kwa mfano ndugu zangu waikoma wana eneo lao maarufu sana la kufanyia mitambiko yao(ni haki yao maana ndio imani yao) wanapokwenda kukutana na mungu wao Machaba. Sasa inapotokea serikali inamkabidhi mwekezaji eneo muhimu sana kwa shughuli za hawa wananchi inasikitisha sana, na kwa hali kama hiyo huwezi kutarajia wananchi hao watoe ushirikiano wa kutosha kwa mwekezaji ama serikali kwa maana ya serengeti national park.

Kweli kabisa mkuu.

Ndio nilikua namwambia ndugu yangu Mr. Rocky juu ya hili. Hilo suala ni sababu kubwa sana ya mafarakano kati ya hao waikoma, Grumeti GR na uhifadhi kiujumla.
Naamini unakumbuka saga ya OBC na uchomaji wa mali za wananchi kule Loliondo GCA.

Mamlaka na hao wazungu wanaamini kwa kufanya hivyo wanawatisha hao wananchi; kumbe ndio wanajenga uadui mkubwa sana. Jambo baya ni kwamba, kutokana na hao wazungu na waarabu kuwa wamejidhatiti kiulinzi, wananchi wanashindwa kufanya revenge kwao na mali zao; bali wananchi wanageukia viumbepori kumalizia hasira zao. Sasa hapo sijui nani anakua anafaidikia, kama sio wote kupata hasara!!
 
Back
Top Bottom