The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,071
Laiti mngejua hii kampuni ya Wind East Africa wamiliki ni akina nani....
Kwani huko wanakohamishiwa wanapelekwa juu ya nguzo za umeme? tena si kuhamishwa ni kusogezwa tu, kama vile inavyopitishwa barabara, watu huhamishwa kusogezwa na si kuhamishwa mji wala wilaya.
Naona hujui kuhamishwa wewe, haukuwepo wakati wa nyerere na vijiji vya ujamaa? basi hata hukuyasoma? kule ndyo kulikuwa kuhamishwa kwa nguvu, ukipenda usipende, unaweza kutolewa wilaya moja ukapelekwa nyingine bila kulipwa wala kujengewa mnatupwa maporini muanze wenyewe kila kitu. Tumetoka mbali kijana, hao wanaletewa neema wanalalamika, ama kweli. Hamsadifiki.
Hakuna ukiukwaji wa sheria hapo, hao watu wanahamisha na wanakuwa "compensated", wanahamishwa bila kulipwa?
Wacheni kulala katafuteni kazi kwenye hizo kampuni, zinalipa vizuri. Mnaletewa maendeleo mnalalamika, hata siwaelewi mu watu wa aina ipi? Sheria za Tanzania hazizuwii maendeleo, yanahamishwa makaburi kwa kufuatwa sheria itakuwa watu walio hai? wacheni chokochoko na ufataani.
Huyo anaeleta ufataani humu mbona hajasema kuhusu barabara ya Dodoma - Singida - Shinyanga na Singida - Dareda - Arusha, wamehamishwa watu wengi sana kupisha barabara mbona alikaa kimya?
Umeme wa upepo unahitaji utafiti wa kina wa kujuwa upepo unapopatikana kwa kasi fulani kwa mwaka mzima unapatikana wapi na hapo sehemu iliyochagiliwa ndio pameonekana panafaa zaidi, mnachotaka ni nini?
Ngojeni na hivi karibuni kuna kampuni zinakuja, moja ya dhahabu, nayo inahitaji eneo kubwa tu na moja ya uranium pale karibu na Manyoni, ndio mseme vizuri.
Waacheni wakishaweka mitambo nyie mpige kiberiti. Maguruneti matatu ti yanatosha kutuma ujumbe.
Msilalamike ... Hamtasikiwa. Take some action.
Kampuni iliyotajwa ni WIND EAST AFRICA, Bila kujali ni ya nani? Inaibua maswali mengi. MKuu wa Mkoa wa Singida analazimisha kuwa kampuni ina eneo, Mkurugenzi wa Manispaa husika ambapo hiyo kampuni inatajwa itawekeza anasema haina hata Eneo la Mita Moja. Kampuni hiyo imepewa msamaha wa kodi tangu 2008, ikapewa leseni ya kuwekeza iliyoandikwa majina ya vijiji viwili tu (Unyambwa na Kititimo), lakini wao wametoa ramani yenye vijiji sita, tofauti na vilivyotajwa katika leseni (Unyamikumbi A, Unyamikumbi B, Ughaugha A, Ughaugha B, Kisasida na Kisaki). Hapa kweli hatuoni Tatizo? Leseni Imeandikwa Dodoma, wewe unaleta ramani ya Morogoro, Leseni imeandikwa vijiji viwili, wewe unaleta sita taouti na vilivyotajwa katika leseni, WAKATI HAYO YOTE YANAFANYIKA wananchi wa eno husika hawajui. Wanaona Balozi wa Uingereza analetwa kuonyeshwa vijiji vyao, Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999, Inashauri wananchi wapewe fursa ya kushirikishwa ili ardhi itolewe kwa ajili ya maendeleo. Kumbukeni Kisa cha Wakaazi walioko katika maturubai Geita mjini waliotolewa nje ya nyumba zao na Serikali hii hii, Mwekezaji (Geita Gold Mines) akasambaza nyumba zao kwa Greda, hadi leo hawajui mbele wa nyumba. tunaoshabikia maendeleo yasiyofuata sheria tunaangamiza taifa kwa sababu ya Ulafi wa pesa. Madudu mengi yatajulikana tu.
avoid the ignorant." (Qur'an 7:199)Mkiletewa umeme shida msipoletewa umeme shida.
Kuhamishwa watu kwa ajili ya kuleta maendeleo ni kitu cha kawaida duniani. Unafikiri maendeleo yanakuja kwa kuota kama miti?
Wacheni kulala, amkeni. Mnaletewa umeme, mnaanza ooh Singiga imeuzwa, imeuzwa imepelekwa wapi? kuwa na fikra japo kidogo.