Singida: Hakuna tofauti ya jambazi na polisi

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Tarehe 2/12/2011 Polisi Mkoani Singida walituhumiwa kumteka mfanyabiashara wa Kuku, kumpeleka eneo la Kindai, kutaka kumlawiti, kumtishia bunduku, na kumwingizia mtutu sehemu ya haja kubwa. Ikumbukwe kuwa Mtuhumiwa Ayubu Jafari alikamatwa na polisi akiwa mahakamani alipokwenda kumwekea dhamana ndugu yake kwa tuhuma za kumshambulia Askari. Hata hivyo ndugu huyo alionekana hana hatia. Jeshi la polisi limetoa taarifa kwa vyombo vya habari muda mrefu baadaye huku maelezo yote yakiwa ya kitoto kabisa. Kwanza kijana waliyemkamata mahakamani wanasema alikuwa mmojawapo ya watu waliokuwepo wakati askari anashambuliwa. Askari hawaelezi ni kwanini hakukamatwa siku ya tukio pale ambapo Askari walikamata watuhumiwa wengine 10 ambao 9 walionekana hawana hatia. Askari waliomkamata mtuhumiwa mahakamani wakiwa wanaeleza kuwa wanampeleka kituo cha polisi, eti alishuka kwenye gari (sio kwamba aliruka) wanasema alishuka akapanda bodaboda (pikipiki) wakaanza kumfukuza hadi Kindai ndipo walipomkamata. Ijulikane kuwa kutoka Singida hadi Kindai ni Kilometa 5. Je ni kweli Land Cruiser ya Polisi yaweza kufukuzana na bodaboda iliyopakia wakashindwa kuikamata? Polisi wanatembea na filimbi mbona hawakupiga kama kweli mtuhumiwa alikimbia? Kama alikimbia na Pikipiki ya ndugu yake mbona huyo hajakamatwa na kufunguliwa shitaka la kutorosha mtuhumiwa? Mbona Namba ya Pikipiki iliyofanya kosa haipo? Polisi kwa namna nyingine mmekiri kuwa mtuhumiwa mlimchukua, na mlikuwa naye eneo la kindai, nje kidogo ya Manispaa. Tuambieni huko kuna kituo cha polisi? Mlienda kumfanyia nini kijana wa watu? Kama kweli aliwatoroka kwa pikipiki itajeni pikipiki namba, na kwanini hakumkamata mwenye pikipiki. Polisi mnatoa maelezo kama walevi vile.,…… mnafanya kazi kisiasa. Huyo dereva wa polisi anayeendesha Land cruiser aliyeshindwa kukamata boda boda bora aache kazi maana hawezi. TUNAENDELEA KUJIFUNZA KUWA JESHI LA POLISI NI LA KIJAMBAZI, LA KISIASA, NA HALIFAI KWA MWENENDO HUU KATIKA JAMII.
 
Si ndo huyu ambaye walimwagia maji halafu wakamwambia wakifika kituon aseme amekatiwa mtoni akiwa anawakimbia polis? Teh teh teh, miaka 50 ya uhuru hiyo baba!
 
mkuu,hii taarifa unaitoa kama vile kila mtu anaij
ua,ungeanza kuelezea tukio kwa mpangilio ili watu wakuelewe vema
 
Back
Top Bottom