Sinema ya Rostam, Kikwete na CCM

Lyehagi

Member
Dec 10, 2010
19
13
Gamba limetoka ingawa kwa shinikizo ndani ya Watanzania na mchezo ya siasa za makida makida za ndani ya ccm. Yasadikika sasa mh. Rz yupo Uswisi anapumzika baada ya siasa za mchosho. Je, nikweli kutoka kwa Rostam ni Gamba kuvuka au kujaza visasi? ua Je kutoka kwake ni mafanikio ya slogan na Nape anayeisimamia? Au ndo mwanzo wa mauzo ya siasa za kebehi, kejeli na makundi ndani ya CCM?

Sijapata uhakika kama kuna mafanikio make kilichopo sasa ni mkanganyiko wa mawazo juu ya jambo hili, Sitta anajaribu kuonesha kukerwa kwake na watu hawa lakinitofauti na kundi lake wapo watu wanajaribu kuuhadaa umma kuwa hayo si ukweli bali asemacho yeye ndo ukweli. Je, hizi si mbio za Uraisi tu zinazotutesa?

Pande ingine ni juu ya umeme na madini ambapo sasa hawa kinajairo wameonekana wao ni wabovu wakati barua yake inadhihirisha kuwa ni mchezo wa kila siku kwani amesema "...kama ilivyokawaida wakati wa bajeti..." hili ni jambo la kawaida kwa wizara zote na ndo wafanyavyo, sasa kapatikana na Rais analijua sana jambo hili si geni kwake.

Swali la msingi, Je zile fedha za sherehe baada ya bajeti kupita hutoka fungu gani? je si zile za walipa kodi? au katika bajeti fedha ya sherehe hizi hutengwa mapema? Serikali ya ccm sasa inatakiwa ijipange, ikubali kuwa imedhulumu vya kutosha watanzania na isafishe bakuli zake zote si mmoja tu na bado sijashawishika kuwa Sitta, Mwakyembe, na wenzake ni watetezi wa wananchi. Ni wanafiki tu.
 
Back
Top Bottom