Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,744
hapo kwenye RED tunajiaminisha sana hivyo na ni vizuri tu kuamini hivyo.Pole sana ndugu KIBURUDISHO kwa yaliyowakuta,
Sie tulifundishwa kutoingilia ugomvi wa wazazi....kwa sababu wanayogombania chumbani kwao kamwe huwezi kuyajua!
Kwa sasa umekuwa mkubwa, nakushauri usijitafutie laana ya mama...Kwa hiyo, unatakiwa kumsamehe ili upate nafasi adhimu ya kujua walau mambo kidogo yaliyomfanya akakengeuka kiasi hicho...Naamini unaweza kujikuta mdomo wazi akiamua kukusimulia ugomvi wao na baba yako in her own perspective!!
Mama ni mama na hakuna mwingine.....Uwe mwangalifu sana!
Babu DC!!
kuna siku rafiki yangu mmoja aliniambia aliwahi kumwuliza mama yake kama kweli yeye ni mtoto wake, serious.
kuna rafiki yangu mwingine ana mpango wa kusitisha kumtembelea mama yake sababu hajawahi kwenda kwa mama yake wakakaa na kuongea na kucheka kama akiwa na wengine. ananisimulia kuwa yeye ndo mtu pekee katika familia ambaye anampa kila kitu mama yake (wenzake wote hawana maisha mazuri sana, kwa hiyo aliwaambia maswala yote ya wazazi yeye ndo atahusika, wenzake wajishughulishe na familia zao tu, ingawa hawakatazwi kama wanaamua kupeleka chochote kwa wazazi wao). lakini hasa mama mtu haridhiki kabisa na kila mtoto wake anachofanya. kila akienda kutembea ni malalamiko mwanzo-mwisho; na ni malalamiko ambayo hayana msingi. sasa anawaza kuna faida gani ya mimi kwenda kumtembelea mama wakati kila nikienda narudi depressed?