Sina upendo kabisa kwa mama yangu mzazi

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
WanaJF wenzangu natumai hamjambo kabisa.Ni story ndefu sana ila nitajitahidi kuifupisha. Ni mkasa (ugomvi) ulioikumba familia yetu kuanzia mwaka 2000 kati ya mama yangu na baba yangu. Kwa asilimia mia moja ugomvi huo ulisababishwa na mama nasema hivyo kwa sababu vituko alivyoanza kumfanyia baba tulikuwa tunaviona ilipelekea aliwahi kutoka nyumbani na kwenda kuishi Mwanza pasipo baba kujua alipeleleza hadi hapo alipogundua kuwa yuko mwanza ndipo alipochukua jukumu la kumfuata alimsihi sana arudi nyumbani aje kuwalea wadogo zangu akakubali kumbe ilikuwa danganya toto aliporudi hakukaa zaidi ya miezi sita akaondoka tena ila kwa kipindi hiki sasa baba aliamua kutomfuata tena akasema kwa kuwa sii mtoto mdogo siwezi kumlazimisha.

Katika ugomvi huo sikuwahi siku hata moja kumuona baba ameinua mkono wake kumpiga mama yangu.Yote hayo yalisababishwa na mama kuwa na hawara mimi na dada yangu ninayemfuata kwa mara ya pili tulikuwa tunachukizwa sana na vitendo vile ambavyo mama alikuwa anamfanyia baba na hiyo ilisababisha mama kunichukia mimi na dada yangu akidai sisi ndio tunampatia baba taarifa ya yale anayoyafanya.Ninachomshukuru sana baba yangu alitumia sana busara kukabiliana na hali ile kwa sababu ilifikia wakati baba aliingiwa na mawazo ya kutaka kuua kutokana na dharau zile alizokuwa anafanyiwa.

Ilipofika mwaka 2004 mama aliondoka moja kwa moja akimwacha mdogo wetu wa mwisho akiwa darasa la kwanza.Kitendo hicho kilimuumiza baba na hata sisi,pia upande wa kielimu ilituatiri sana kwa kipindi hicho nilikuwa kidato cha tatu. Ilikuwa tukitoka shule ndio tunajiandalia chakula au wadogo zangu waliokuwa wanasoma shule ya msingi tulikuwa tunakuta wamepika halafu wametubakizia chakula wao wamerudi shuleni.Mwaka 2005 Nilihitimu kidato cha nne ila kwa bahati mbaya sikuweza kuchaguliwa kuendelea na masomo sikukata tamaa niliamua kuingia mtaani kujifunza mambo ya ufundi wa umeme na masuala ya IT ambayo kwa kiasi ninayamudu pia mimi ni installer wa hizi dishi za satellite za tv.

Nikiwa na ndoto mbili 1.kuwa na uelewa mkubwa zaidi juu ya masuala ya IT au 2.Kuwa oparetor wa ile mitambo ya kulima barabara.Mwaka 2008 niliamua kuoa nimejaliwa kupata mtoto mmoja.Mwaka 2009 mdogo wangu anayenifuata kwa mara ya pili alihitimu kidato cha nne alikuwa na uwezo mzuri sana shuleni alipatwa na ugonjwa tulimpeleka hospitali tulimuuguza kwa kipindi hicho chote tukiwa na baba ila kabla matokeo hayajatoka ambapo hapo baadae matokeo yalitoka akawa amefaulu kuendelea na kidato cha tano ila kwa mapenzi yake mola alimchukua mdogo wangu alinifia tukiwa naye wodi nakumbuka aliniambia KAKA YANGU SIJUI KAMA NITARUDI NYUMBANI NAOMBA UWASALIMIE WADOGO ZANGU NA MAMA KAMA ATAKUJA KWENYE MAZISHI YANGU kauli hiyo huwa inaniumiza sana kila ninapoikumbuka.

Ilipofika saa kumi jioni mdogo wangu alifariki.Tulishughulikia taratibu za mazishi tulimzika mdogo wetu bila ya mama kuhudhuria mazishi ya mwanae.Baada ya miezi miwili sijui ni nani alimpa taarifa ndio akaja kuliona kaburi la mdogo wetu.Na juzi amekuja amefikia kwangu yaani nampa heshima tu ya mama ila kiukweli simpendi kabisa.
 
Pole sana hivi vitu huwa vinathiri sana maisha ya watoto huenda ungeweza hata kufaulu mitihani yako vizuri kama sio huo ugomvi,muombe Mungu akupe roho ya msamaha kwani hicho kinyongo kinakuathiri zaidi wewe kulioko Mama yako
 
Duh,pole sana kwa Masahibu yaliyokupata.Ushauri wangu ni kwamba,ufahamu kuwa Huyo bado ni mama yako au kwa lugha nyungine mzazi wako, hivyo endelea kumpa heshima ile unayotakiwa kumpa.Hayo yaliyotokea ni baina ya wazazi wenu hiyvo wao wanaweza kuyatatua ama vinginevyo Mola ndiye muamuzi.
lakini pia si vibaya ukimueleza namna mlivyoathirika kwa yale aliyowatendea ili aweze kutambua makosa yake na kujirudi kwa muumba,maana maamuzi mengine huwa tunayafanya kwa tamaa na makosa ya kibinadamu.

Ki ufupi haya mambo huwa ni magumu sana.ila sikushauri umchukie, kwani nyuma ya pazia kuna mengi pia unakuwa umejifunza kutokana na magumu yaliyo wapata.nakushauri uwe mvumilivu na mstahimilivu, na usijeshangaa pia familia yenu ikaungana kama hapo awali, na kuanza maisha mapya.Dunia ina mapito yake.
 
dah poleni sana......dunia in amitihani mingi sana......kwanza hongera kwa kujitambua na kufanya icho ulichoweza kukifanya ..wapo watu na elimu zao za chuo kikuu lakini hawajaweza kusimama....naamini unanielewa.........kuhusu suala la mama na baba..kweli mama alifany amakosa hasa kuwachanganya watoto na ugomv wao........ila kuhusu kutengana kwao hapo hauwezi kuingilia...kaa nae mwambie taratibu jinsi alivyoinyima familia haki yake..amewafanya mmeathirika kisaikolojia kw akukosa upendo wake.....mwambie si kwamba hata unahitaji arudi nyumbani hapana but awape ule upendo aliowapokonya..awaponye majeraha.........najua mlivyoumia hasa ukizingatia ni watoto wa kiume.....watoto wa kiume wanawapenda sanamama zao......ila pia Muombe Mungu.
 
Duh! what a sad story...
Mkuu pole sana na maswahiba na mitihani ya dunia hii ya leo...
Kilichokupata naamini kimeugusa moyo wako na kimeuumiza na sasa moyo unaugua maana hakuna hata chembe ya uungwana ambayo ilioneshwa na mama yako...
Pamoja na hayo, nafasi yako kama mtoto hupaswi kuwa na kinyongo na mama yako, jinsi utakavyokuwa ukimtendea wema kama ana akili nzuri, moyo wa kujuta na kutubu utamrudia na atang'amua ya kwamba alivyokuwa akifanya havikuwa sahihi hata kama walipishana kimawazo na mumewe...

"Dunia tambara bovu"​
 
Stahamili umsamehe umwachie Mungu hukumu ... na uondoe chuki moyoni mwako kwani haitokusaidia zaidi ya kukuumiza tu kwani huna nafasi ya kumkabili na yote aliyoyafanya na hataweza kukupa sababu kwani si nafasi yako kujua yote hayo wala huwezi mlazimisha.

So, nakushauri ujitahidi tu kumsamehe kama baba yako aliweza kukaa kando na kukubali matokeo nawe fanya hivyo hivyo.
 
Sina cha kuongeza zaidi ya kukupa pole sana; siwezi sema naelewa unachofeel coz sina experience ya hivyo hata 1/8 yake. Una haki ya kumchukia, so unachofeel ni kitu cha kawaida; na ninakushukuru pamoja na yote bado umempokea kwako, l hope kifo cha mdogo wako kitamtesa na kumpa adhabu inayomstahili na huko alipo anaweza asipafurahie na mwisho wa siku aje awaangukie kwa kuwaomba msamaha!

Pole tena!
 
.. yaani nampa heshima tu ya mama ila kiukweli simpendi kabisa.
Kwa kuzingatia yaliyotokea, hiyo ni favour kubwa tu kwake. Vipi anaonesha kujutia/kutatizwa na aina ya maisha aliyoamua kuishi? Zaidi, nakupa pole sana.
 
Kiburudisho,

Kusamehe kunahitaji muda.
Na kusamehe kunatofautiana kati ya mtu na mtu, kuna watu mnaweza fanyiwa kitu kile kile na mtu yule yule, lakini mmoja akasemehe haraka kabla ya mwingine. Hii husababishwa na mambo mengi.

Inavyoonekana wewe bado kidonda hakijapona, ndio maana bado jambo hili linakutesa.
Je unadhani alolowatendea ni kubwa sana?????? Unadhani halisameheki????
Unaamini mama yako ana-control your destiny???
Je unaamini kusamsamehe mtu ni hadi akuombe msamaha???
Je, unaamini katika 'unspoken forgiveness/apology'??

Baada ya kujijibu maswali hayo hapo juu utajua ufanye nini ili uweze kumsamehe mama yako, kama unaweza samehe bila hata kuongea naye kama unaamini kwenye unspoken forgiveness/apology au ni hadi uongee naye utoe duku duku lako.

Sijui imani yako lakini, naweza elezea hili kwa mtazamo huu.

Binadamu tunazaliwa for a specific role, je roles ya mama yako katika jamii inayomziunguka ni ipi? Labda role yake ilikuwa ni wengine wajifunze kutoka kwake.

Kwa nini wewe kiburudisho? Kwa nini wewe upewe huyo mama asiyejali? Sijui, labda wewe kiburudisho na familia yenu ndio mmeweza kuyabeba mapungufu ya mama yenu bila kutetereka. Sometimes mambo haya yanaenda kwa watu wanaoweza survive, kwa hiyo usidhani ulionewa kuwa na mama wa aina hiyo.
Labda wengine wakisema hapa waliyonayo unaweza ona mama wenu ni malaika.

The way forward:
Inaonekana kumchukia mama yako inakusumbua 'kind of a personal conflict'
Kama umeshaona hivyo, kwa nini usifanyie kazi kutoa huo msamaha??

Hapa unaweza chukulia kwa mtizamo huu, je maasi/maovu ya mwingine uyaruhusu yakufanye uwe na chuki?? Je ina thamani hiyo?? Mwisho wa siku, wewe umeshaweza kujitegemea na unemdelea na maisha yako kama kawaida. Hii ichukulie kama 'sunk cost', lakini imekufanya labda kuwa mvumilivu zaidi na strong zaidi. Labda uvumilivu huu utakuja kukusaidia baadae katika maisha yako.

Najua ina changamoto sana kusamehe mtu wa karibu aliyekusaliti, lakini ni nzuri pia
Inakupa amani wewe mwenyewe na unaweza jikuta mnajaribu rudisha mahusiano yaliyokuwa yamepotea.

Ubaya au sijui uzuri, mzazi hata afanye maasi kiasi gani. huwezi kumdelete permanently sababu uhusiano huu huwa haufi na wala huwezi badili mzazi.

Bora kutambua njia za kufanya ili uweze samehe.

Wish you luck katika kutoa msamaha huo.

Pia jaribu ku-connect na Mungu wako inakufanya ujione hata wewe hauko that perfect kwa hiyo waweza toa msamaha.
 
mkuu pole sana kwanza kwa kufiwa na mdogo wako kipenzi pili kwa kukosa upendo wa mama.

ngoja nikwambie maisha yako hivi hutupitisha kwenye vitu ama tunavyovitaka ama tusivyovitaka lakin all in all lazima tuvipokee tu hatuna ujanja.

najua wengi tu waathirika wa maisha ya ubinafsi wa wazazi ngawa wengi wetu wa kiume. lakin wazazi wa kike wengi huwa ni wastahimilivu huwa wanawabeba watoto wao. so usijutie kwa kilichotokea kwan ni namna tu ya maisha. Tatizo kubwa hapa ni kwamba wewe umetumka kama ubao wa kutufunza wengine so nakupa pole sana kwa hilo. na kwakua umekuwa ubao basi ngoja tujifunze hivi.

kwanza kabisa unatakiwa usamehe na uachilie ili uwe na amani, pia mwmbie mkeo asimsemeshe chochote kile mama yako no matter mama atamwammbia kitu kimkere namna gani. kwanini natoa angalaizo hili ni kwamba waweza kukuta roho ya mafarakano bado iko ndani yake hivyo uwe makin sana tena mwombe mungu akupe macho ya rohoni sana mkuu.

yawezekana pia baba yako akakasirika sana kwa uajio wa ama yako hapo nyumban kwako na hili likazua mtafaruku kaati yenu wote please mueleweshe baba juu ya hili ili akuelewe kaka usihamaki hii likitokea. uwepo wake hapo kwako jitahd sana usiwe wa muda mrefu na ikiwezekana ongea nae nafsi iumie aamue kurud nyumban.

nafikir hapa umenielewa ngoja nile kisha nitarudi kumalizia ushauri wangu.
 
haya nilirudi nyuma kusoma na posts za wengine, kimsingi maswali alaoakuauliza Kongosho ni sawa na niliyoyawaza mimi.

unachotakiwa kufanya sasa hivi uangalie kwanza kabisa amani yako po wapi? ukishajua basi fikiri waweza kuipatia wapi? ukishajua chukua hatua. samehe na achilia kabisa kisha hakikisha mama hakai hapo kwako muda mrefu hadi wakaanza ugomvi na mka mwana wake hili nalitoa kama angalizo kwani najua wanawake na roho zetu zilivyo. please nielewe kwa hilo.
 
Last edited by a moderator:
So sad. Nam-admire babako kwa namna alivyoweza kulihendo hili jambo. Maana mie kusoma tu stori yako, nimeona hata pumzi zinaniishia, yaani nimeshikwa na mihasira mpaka nasweat. Kama atawaomba msamaha, msameheni-ingawaje kusamehe si kusahau. Hiyo ndiyo sura halisi ya dunia lakini-dunia si njema sana!
 
Pole sana mkuu, mengi mazuri yamesemwa... sina cha kuongeza zaidi jitahidi kumsamehe ili watoto wako wasije wakaona chukiyako kwa mama yako.. ilkitokea hivyo kunapicha mbaya itajijenga na kuwaathiri wajukuu pia... Muombe sana Mungu
 
Mwachie Mungu Yote, Na Umwombe Mungu akupe neema yake uweze kusamehe na kusahau yote maana hutapata mamamwingine zaidi ya huyoPole sana kwa kubeba mzigo mzito ktk maisha yakoMUNGU TU ANAWEZA KUKUPA FARAJA YA KWELI
 
So sad. Nam-admire babako kwa namna alivyoweza kulihendo hili jambo. Maana mie kusoma tu stori yako, nimeona hata pumzi zinaniishia, yaani nimeshikwa na mihasira mpaka nasweat. Kama atawaomba msamaha, msameheni-ingawaje kusamehe si kusahau. Hiyo ndiyo sura halisi ya dunia lakini-dunia si njema sana!
na hivi ulivyo hovyohovyo huyo mama mbona saa hizi lingebaki jina tu (kidding)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom