Sina raha

hivi huyo rafiki yako yeye hana mwanaume? tabu ni haya magonjwa tu yaliyoonea mdada. walie timing hao mpk uwabambe kisawa sawa.peleleza nyendo zao,mwizi lzm ashikwe na alichoiba. wote wawili ni shameless viumbe.na uwe unamtia wivu mume kwamba huyo hawara yake kapata buzi,wakati mwingine mwambie rafiki ana buzi lina ngoma ili atoke jasho. Pole dada.:

hahaha nimependa hio tactic.
 
are you trying to be a comedian or what?
unanivunja mbavu hapa...lol

Sasa Boss, nikimuacha nitaacha wangapi? Manake nikimuacha huyu niliyenaye nikienda kwa mwingine naye atakuwa hivyo hivyo tu. Sasa nitaacha wangapi? Nitavumilia tu ili mradi anafanyia hayo mambo yake mbali na mimi.
 
kuna uzi ulitoka hapa siku si nyingi jinsi mashost wa karibu wanavotoka na waume wa rafiki zao bila hata haya
:focus: pole sana dada ila muhimu umeujua ukweli na umejua mbaya wako nani...........cha muhimu ongea na huyo mwandani wako msikilize atakueleza nn ndio uamuzi utafanya mana hapa ni vigumu kukupa ushauri mana hujaongeana huyo mwandani wako pengine akawa na sababu za msingi za kufanya ivo......inawezekana ulikua unamnyima akatafuta alternative ama shost ulimsimulia sana juu yako na huyo mumeo sasa yy atakutumia udhaifu wako ww pale uliposhindwa kumtega mumeo na kumpata .............so kabla hujachukua action yoyote nakushauri ongea na mumeo kwanza uone tatizo lilikua wapi mpaka akachuku uamuzi huo ama ni uhuni tu anao damuni
 
siku aki ludi usiku mpemzingo achoke akilala fofofo chukua mche au mwiko kongota miguuni mwake mpaka kesho ashinde tembea aite watu ndo umwambie ule mwiko wa ndoa kavunja sasa niikuwa nauludisha na huyo shosty mwambie siku utapo muona lazimamjue babu wamezidi sana tetea ndoa mwaya utakaa kimya mpaka lini hasila inauwa lohoooo'
 
Mhh...Hii stori hii i doubt it najaribu ku-connects dots lakini haiji...anyways wakuu endeleeni kujadili..
 
Eti wanasemaga mwanaume hafumaniwi bali anakutwa... Afu mwanamke anafumaniwa.

Hiyo ni kama kuremba lugha tu lakini kufumaniwa kuko palepale!! Umenikumbusha kijijini kwa kina mama'angu, kuna mwanaume alifumaniwa anazini na mkaa mwana wake!! Skilizia stick zake aisee, alichunwa njiti za uchi asikwambie mtu, Sungusungu wanachapa hao heee!!!
 
Sasa Boss, nikimuacha nitaacha wangapi? Manake nikimuacha huyu niliyenaye nikienda kwa mwingine naye atakuwa hivyo hivyo tu. Sasa nitaacha wangapi? Nitavumilia tu ili mradi anafanyia hayo mambo yake mbali na mimi.
Hapa hata moyo wako unajua kuwa humaanishi ulichoandika na kama kupendwa ni kucomment hivi mie nakushauri bora usipendwe....

"Nyani Ngabu" jina kubwa jf we hujui tu! Usiniangushe bana manake najaribu kuvaa viatu vyako na naomba mungu visinipwae!
 
Hiyo ni kama kuremba lugha tu lakini kufumaniwa kuko palepale!! Umenikumbusha kijijini kwa kina mama'angu, kuna mwanaume alifumaniwa anazini na mkaa mwana wake!! Skilizia stick zake aisee, alichunwa njiti za uchi asikwambie mtu, Sungusungu wanachapa hao heee!!!
Lol Kipipi!!! Mka mwana???
 
Hapa hata moyo wako unajua kuwa humaanishi ulichoandika na kama kupendwa ni kucomment hivi mie nakushauri bora usipendwe....

"Nyani Ngabu" jina kubwa jf we hujui tu! Usiniangushe bana manake najaribu kuvaa viatu vyako na naomba mungu visinipwae!

Unasema kweli Sweetlady?

Basi hebu chukua hii dedication mahsusi kwako tu!

Last edited by a moderator:
kuna uzi ulitoka hapa siku si nyingi jinsi mashost wa karibu wanavotoka na waume wa rafiki zao bila hata haya
:focus: pole sana dada ila muhimu umeujua ukweli na umejua mbaya wako nani...........cha muhimu ongea na huyo mwandani wako msikilize atakueleza nn ndio uamuzi utafanya mana hapa ni vigumu kukupa ushauri mana hujaongeana huyo mwandani wako pengine akawa na sababu za msingi za kufanya ivo......inawezekana ulikua unamnyima akatafuta alternative ama shost ulimsimulia sana juu yako na huyo mumeo sasa yy atakutumia udhaifu wako ww pale uliposhindwa kumtega mumeo na kumpata .............so kabla hujachukua action yoyote nakushauri ongea na mumeo kwanza uone tatizo lilikua wapi mpaka akachuku uamuzi huo ama ni uhuni tu anao damuni
Kwa hiyo unataka kusema maybe hana kosa, kosa ni la mke wake? kaaz kweli kweli...
Kwa mtoa mada: fikiria sana, hakuna haraka wa kutoa maamuzi wakati una ushahidi wote.
Kwangu mimi huna haja ya kumuhoji maana umesha ona ukweli na chochote atakacho sema hakita kusaidia.
Kama unaweza hama kwa muda, fikiria sana maisha yako ya leo na ya baadae, kumbuka sababu na lengo zilizo kufanya kukubali kuolewa, na kama unaona sababu na lengo hizo hazija potea basi fikiria ni kipi wewe na mume wako mnaweza kufanya kuimarisha ndoa yenu. Ikiwa huoni sababu za kuendelea kua nae, au ukiona hamuwezi kufikia lengo mlizo panga sababu ya hali ilio tokea basi achana nae.
Hakikisha huchukui uamuzi wowote ukiwa na udhuni au hasira. deal na hasira yako kwanza (hata kama itachukua wiki kadhaa, hakuna haraka)
 
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29.Nimeolewa na nina mtoto mmoja. Juzi nimegundua kwamba mume wangu anatembea na mmoja wa marafiki zangu. Nilimsindikiza rafiki yangu kumuona shangazi yake mgonjwa,tukiwa pale nikataka kumkumbusha mume wangu kununua baadhi ya vitu ambavyo tulikua tunahitaji nyumbani. Nikaazima simu ya rafiki yangu kwakua yangu ilikua imeisha chaji,akanipa. Nikadial namba za mume wangu bila wasiswasi,baada ya kuandika zote nikaona kwenye screen imeandikwa mpenzi. Nikajua labda nimekosea maana nilikua natoa namba kichwani kwahiyo nikadial upya,matokeo yale yale.Nikaona nipige,ikapokelewa "mambo darling" sauti ya mume wangu bila ubishi. Kigugumizi nilichopata sikuweza kutoa neno zima.Akaishia kusema "mpenzi unakatakata ngoja ntakupigia" simu ikakata. Nilichofanya nilifuta namba nilizodial alafu nikadial simu ya dada wa kazi.

Kuchungulia msg box naona zinazotoka na kwenda kwa mpenzi zimesheni. Nikamrudishia na pale pale nikaaga.Sijamuuliza yeyote kati yao wala sijaongea na rafiki yangu since.Nafikiria nini cha kufanya.Naombeni ushauri.

ama kweli huna raha.....pole sana dada ila kukaa kimya hapana. Mueleze mumeo kuwa umegundua ana mahusiano na shoga yako. Halafu huyo shoga,ushoga na ufe.
 
Lol Kipipi!!! Mka mwana???

Ndio.......watu hawana adabu eti!! Tena nami nilipita maeneo hayo nikawaona, sikujali coz mi sio mwenyeji na nilikuwa siwafahamu vizuri!! Kumbe raia wamewalia mingo tu alafu wakawapulizia kipenga!!!
 
Kama usipomwambia ulichogundua utakuwa unajiumiza tu. Bora ukae naye uliongelee jambo hilo kwa utulivu na uwazi, yaani bila sauti yenye hasira ili naye asiwe aggressive na defensive. Umjulishe ulichoona kwenye simu ya rafiki yako, umwombe awe mkweli kwako, akuambie kama ana uhusiano wa kimapenzi na rafiki yako. Haitakuwa rahisi lakini ndicho unachopaswa kufanya ukitaka kuondoa wasiwasi ulio nao. Ndoa yenye furaha na kudumu haiwezekani kama mke na mume hawawasiliani.
 
Kuongea ni muhimu ila asiongei nae kwa lengo la kutafuta ukweli maana amesha ujua. Amwambie tu kua amesha jua kinacho endelea, na achukue muda wa kufikiria upya hiyo ndoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom