Sina mkia na sijazaliwa nao

bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,206
2,899
Nimesikia na nimeona kupitia TV alichokisema mwenyekiti mpya wa ccm kuhusu wanaorudi ccm toka upinzani. Hoja ya mkia nilivyoielewa ni kwamba ukiwa ccm una mkia na ukienda upinzani lazima ukatwe mkia.

Upinzani hakuna wanyama kwa maana wanyama wana mikia na unyama tumeuona,tunauona na tutauona.

Mimi sina mkia na nitaishi kwa kutokuwa na mkia na nitaishi kisiasa na wasio na mikia, na in any case akitokea mwenye mkia lazima tuukate ili asiendane na sisi.

Sasa kwa vile nimezaliwa bila mkia nitawezaje kwenda kuishi na wenye mikia? Ila wenye mikia ni rahisi kuishi na sisi kwa sababu mkia utakatwa hata kwa operesheni ya ganzi.

Nawasilisha, ni rahisi kukatwa mkia kuliko kuungaunga ili uwe na mkia
 
Maana ya msemo huo kwa maoni yangu ni kwamba uongozi wa juu unaweza kumsamehe anayerudi tena CCM lakini siku zote huyo atakayesamehewa ni lazima uwepo wake kwa mara nyingine baada ya kurudi utaambatana na kunyooshewa vidole siku zote.

Kukatika mkia ambako mwenye zizi anaweza kuona sio tatizo ni ule msamaha wa uongozi wa juu lakini ng'ombe wengine wataiona tofauti ya mwenzao, maana yake wanachama miongoni mwao ni lazima watakuwa wanamsimanga mwenzao.

Mwanachama wa aina hiyo hawezi kuukwepa unyonge pamoja na kejeli zisizokwisha. Masimango yatakuwa sehemu ya maisha ya mwanachama wa aina hiyo.
 
Uko sahihi 100% na ndo ukweli wenyewe. Ninachomaanisha Mimi ndo nilichokimaanisha
 
Msemo wa Mheshimiwa ulikuwa na mantiki moja tu nayo ni anaerudi toka upinzani hafanani nasi so tukae nae makini!
 
Msemo wa Mheshimiwa ulikuwa na mantiki moja tu nayo ni anaerudi toka upinzani hafanani basi so tukae nae makini!

Hao waliorudi wameingia choo cha kike hata kama wameomba msamaha na kurudi bado dhambi ya usaliti watabaki nayo mbele ya wanachama wa ccm, na wasitegemee kuaminiwa tena humo au kupewa nafasi kama waliyokuwa nayo kabla ya kuhama, sasa kama walirudi wapewe madaraka wategemee, wajiandae kustaahafu kwa masimango
 
Nimesikia na nimeona kupitia TV alichokisema mwenyekiti mpya wa ccm kuhusu wanaorudi ccm toka upinzani. Hoja ya mkia nilivyoielewa ni kwamba ukiwa ccm una mkia na ukienda upinzani lazima ukatwe mkia.

Upinzani hakuna wanyama kwa maana wanyama wana mikia na unyama tumeuona,tunauona na tutauona.

Mimi sina mkia na nitaishi kwa kutokuwa na mkia na nitaishi kisiasa na wasio na mikia, na in any case akitokea mwenye mkia lazima tuukate ili asiendane na sisi.

Sasa kwa vile nimezaliwa bila mkia nitawezaje kwenda kuishi na wenye mikia? Ila wenye mikia ni rahisi kuishi na sisi kwa sababu mkia utakatwa hata kwa operesheni ya ganzi.

Nawasilisha, ni rahisi kukatwa mkia kuliko kuungaunga ili uwe na mkia
Mikia saccos. Hahahaaa
 
Nilivyoelewa mimi ni kuwa wote wanaorudi ccm toka upinzani ni watu wasiotimilika. Yaani thamani yao haiwezi fanana na wale ambao wamekomaa na ccm mwanzo mwisho. Tegemeeni kubaguliwa nyie mliosaliti upinzani na kurudi ccm.
 
Wewe mtoto! Umelitoa wapi hilo neno? Mkia ni takoo la mwanamke, lile lililobinuka.
Kama kuna mwanasiasa amelimiss use, hana maadili na inabidi aitwe kwenye kamati ya maadili...
 
Maana ya msemo huo kwa maoni yangu ni kwamba uongozi wa juu unaweza kumsamehe anayerudi tena CCM lakini siku zote huyo atakayesamehewa ni lazima uwepo wake kwa mara nyingine baada ya kurudi utaambatana na kunyooshewa vidole siku zote.

Kukatika mkia ambako mwenye zizi anaweza kuona sio tatizo ni ule msamaha wa uongozi wa juu lakini ng'ombe wengine wataiona tofauti ya mwenzao, maana yake wanachama miongoni mwao ni lazima watakuwa wanamsimanga mwenzao.

Mwanachama wa aina hiyo hawezi kuukwepa unyonge pamoja na kejeli zisizokwisha. Masimango yatakuwa sehemu ya maisha ya mwanachama wa aina hiyo.
Kama makapi yakipeperushwa yanaweza kurudi na kuwa mchele basi tuendelee kuamini miujiza ipo.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom