Sina mapenzi naye tena, ushauri wenu tafadhali

yewomi

Member
Jul 20, 2012
78
27
Mimi ni binti nina mpenzi wangu ambaye tuna muda mrefu kwenye uhusiano wetu.

Tatizo ni kwamba wakati nampenda alinifanyia visa vingi sana aliniumiza mpaka nikaona dunia chungu ila sikuwa na uwezo wa kumuacha kutokana na jinsi nlivyompenda.

Sasa yale maumivu ya vitu alivyokua ananifanyia sasa hivi ndo yamekua makali kiasi kwamba hata ule upendo umepungua na yeye ndo kama amezidisha mapenzi na amenitambulisha kwa wazazi.

Ushaur wenu nifanyeje ili ule upendo urud mana nkikumbuka vile visa sitamani hata kumuona.

Ushauri tafadhali
 
Hutamani hata kumuona. Sasa hapo kuna ushauri tena kama siyo porojo tu.
 
....mwambie kuwa huna hisia zake tena....

then sepa...

muache atafute mwingine wa kumfanyia visa na kumpenda
 
Mfungukie tu kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha ili atafute utaratibu mwingine mapema kuliko kuendelea kumpa matumaini mpaka anakutambulisha kwao. Fanya maamuzi sasa kuzidi kuchelewa utakujamuumiza zaidi mwenzio
 
ushauri gani unataka mdogo wangu? tukuunge mkono umuache tukwambie umsamehe au tukwambie uolewe naye au usiolewe naye?
 
wivu umezidi upendo/ni uvivu zaidi ya vitendo/
kila siku lawama na kunizushia skendo /
kama hunitaki ni vema uniweke wazi /
nijue nitambue kwani mademu wapo shazi/

naimba tu/
 
Jibu unalo ila unataka tukujibie ili maamuz utakayofanya usingizie ulipata idea huku.....noo hilo jibu ulilonalo moyoni mwako ndo fata hilo
 
mimi naona kama hujielewi,ulitaka kupendwa kakupenda.......baada ya kupendwa unapunguza upendo basi seems not yo type
 
ushaur wenu nifanyeje ili ule upendo urud mana nkikumbuka vile visa sitaman hata kumuona,.ushauri tafadhal
Kuolewa na hayo maumivu ni vitu viwili tofauti.

Unaumia kwa alivyokufanyia na keshajirudi huwezi kumsamehe. Hiyo haijengi wala kubomoa ubora wa huyo mumeo mtarajiwa. Thats on you. Wewe ndiye mwenye tatizo la kutosamehe na kusahau.

Unatakiwa ukubali akuoe kama unadhani ana quality nzuri za kuwa mumeo na mtajenga familia bora. Uwezo wako wa kusamehe ndio guarantee kuwa utakuwa mwanandoa bora. Kwa sababu ndoa ni kukosa na kusameheana. And trust me, kwenye ndoa kuna issues hayo maumivu unayosema ni piece of cake my dear!

The fact that you came here to ask for advice tells me you still love him. Its just that you can't forgive and thats on you
 
jamani umesema alikuwa anakufanyia lkn bdo uliendelea kuwa naye nasasa anaonyesha mapenzi ya kweli ww upendo umepungua ni bora uwe muazi kwake mapema kuliko kuja kumtesa baadaye
 
Kuolewa na hayo maumivu ni vitu viwili tofauti.

Unaumia kwa alivyokufanyia na keshajirudi huwezi kumsamehe. Hiyo haijengi wala kubomoa ubora wa huyo mumeo mtarajiwa. Thats on you. Wewe ndiye mwenye tatizo la kutosamehe na kusahau.

Unatakiwa ukubali akuoe kama unadhani ana quality nzuri za kuwa mumeo na mtajenga familia bora. Uwezo wako wa kusamehe ndio guarantee kuwa utakuwa mwanandoa bora. Kwa sababu ndoa ni kukosa na kusameheana. And trust me, kwenye ndoa kuna issues hayo maumivu unayosema ni piece of cake my dear!

The fact that you came here to ask for advice tells me you still love him. Its just that you can't forgive and thats on you

Asante kwa ushaur mzuri
 
mambo kote ni magum tu na wenzio nao wanavumilia tu,ukimwacha utakutana na mwingnine nae atakutesa ka huyo huyo
 
Back
Top Bottom