Sina ajira, naombeni mbinu ya kujenga "network" na watu wa makazini

Bundeskanzler

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
215
49
Kwa kudra za mwenyezi Mungu ninaamini ninyi wote ni wazima wa afya,

Jamani mwenzenu nipo Tabata Segerea kwa kaka yangu, kwa sasa nimeshindwa kila nikijaribu kujenga "network" ya jamaa na marafiki zangu wenye ajira niliokuwa nimesoma nao chuo ili itokee hata siku moja mtu aniambie "Ambakisye embu nipe CV yako niione" hakuna kitu,

ikitokea tumekutana facebook ama kwenye dalala ama njiani, tukipeana numbers za simu mawasiliano yanakuwa moto moto wiki moja tu baada ya hapo ukaribu unaanza kupungua, mpaka inafika wakati ninajiuliza sijui mimi nina gundu/nuski ama nini?
 
ungekuwa KE,kitaambo upo kwenye ajira,lkn kama ni ambakisye tena,endelea kupiga deki kwa kakayako...pole anyway!
 
Anza na classmates zako wote uliowahi soma nao. Ndugu zako, marafiki wa wazazi wako, majirani zako.
Nenda nyumba za ibada, jitolee. Ukikutana na watu wasalimie. Kama kuna fellowship we nenda tu, si sawa na kushinda kwenye TV nyumbani.
Peleka CV yako uombe kufanya internship kwenye taasisi mbalimbali. Anza huko wanapofanya kazi ndugu au marafiki zako.
Kama kuna seminar au workshop yeyote we nenda tu, utakutana na watu wapya. Jichanganye, elezea strength zako.
Uje kwenye social networks. Huko kwenye mitandao unaweka nini? Je watavutiwa wakisoma unachoweka? Kuna mijadala, huwa unajadili huko? Una account linkedin?
Invest in yourself, tafuta kitu unachoona kipo hot kwenye job market na wengine hawana. Jisomee kama part time tu. Kifanyie mazoezi hadi ukiweze. Jifunze lugha kwa ufasaha. Soma vitabu na majarida mbalimbali.
Pia usibweteke, kama unaona kuna sehemu unaweza kupata mtaji kidogo anza kuwekeza (if you love business). Au mshawishi ndugu yako afungue biashara na wewe umsimamie kwa uaminifu wa hali ya juu.
Usiwe unakaa nyumbani, kama unapenda mpira toka nje ya mitaa yenu. Nenda sehemu zilizochangamka angalia mpira huko. Utakutana na watu wa aina mbalimbali. Mtabadili mawasiliano, networking itaanzia hapo.
Usikate tamaa kwenye kuomba kazi, we omba tu hata kama unaona haikufai we omba tu. Anza hata kwa wahindi huku unajenga experience.
Usimsahau Mungu, kama wewe mkristu funga na kusali. Mungu hatakusahau.
 
Anza na classmates zako wote uliowahi soma nao.
Uje kwenye social networks.
Una account linkedin?
Huo ndio ushauri. Kwanna aanze na watu aliosoma nao, majirani ulioishi nao na pia watu anaokutana nao kwenye nyumba za ibada. Hapo utaanza kujuana na hao jamaa pamoja na rafiki zao.
 
Umesomea nini chuo?Muombe Mungu na tupia CV maofisi strategic alafu muombe Mungu,muujiza utafanyika tu
 
Back
Top Bottom