DC Yamungu: Simwogopi Rais, acheni uoga!

Hii aina ya viongozi/wanasiasa askari hawajui hata ukomo wa madaraka/majukumu yao. Wana copy na ku paste principles za jeshini uraiani. Hii ni hatari .. Hana nidhamu na inaonekana hata aliyemteua kama vile anamuogopa
 
Jeshini mbona kuna nidhamu ya hali ya juu kabisa!. Na hiyo ndio siri ya ushindi katika ops zake.
 
Yamungu amekosa nidhamu...PERIOD.....na mtu ambaye amekosa nidhamu kuna taratibu zake.........

ameikosaje hiyo nidhamu,kwa kusema ukweli au?
nyie ndiyo wale wa nidhamu ya woga.ukiwa kwenye keyboard mafisadi mafisadi,ukikutana nao uso kwa uso hehe hehe muheshimiwa,tehe tehe tehe!!
 
Hii aina ya viongozi/wanasiasa askari hawajui hata ukomo wa madaraka/majukumu yao. Wana copy na ku paste principles za jeshini uraiani. Hii ni hatari .. Hana nidhamu na inaonekana hata aliyemteua kama vile anamuogopa

Sasa kama aliyemteua anamuogopa kwa nini wananchi anowatawala wasimkatae?
 
Jamani tusilete uchonganishi usiokuwa na msingi, yamungu anahaki ya kutoa maoni yake! Ila tunapata picha kuwa wananchi wameshachoka, serikali isipolifanyia kazi watakuja chomwa moto siku moja. bukoba wamechapwa, singida walichomwa visu.

Walimu wanahitaji sasa "performance contract", kila mwisho wa mwaka wafanyiwe evaluation wanao underperform wakatafute kazi zingine. Anaeona mazingira ya kazi magumu akafundishe kwa giriki FEZA. Kule wanapewa chai na mkate asubuhi.

Eddy ni kweli Yamungu katoa maoni yake na wala hiyo haimaanishi kwamba maoni yake ni sahihi that why we are questioning his ideas. Na sisi tu haki ya kuyasemea maoni yake na kuya clash taking in mind kwamba huyu ni mtu mkubwa kisiasa na maoni yake yanaweza kuonekana kwamba ni sera ya nchi na watu wataamka asubuhi wakianzia kwako kukupiga viboko mbele za wanao. Huu ni uhuni. Tutaukataa na hapa hakuna uchonganishi.
Na ni lazima ujue kuwa performance contract si kwa ajili ya walimu pekee bali ni kwa ajili ya watumishi wote wa umma na wakulima pia wafanyabiashara ambao wengi ni wakwepa kodi ya nchi.
Kila mtanzania leo ili tuiweke nchi kwenye hali nzuri lazima awe na contract ya perfomance kila mwaka.
Kwa mfano mkulima asipotekeleza majukumu yake vizuri unajua consquence zake kiuchumi?
wacha kuleta shida ya watanzania kwa walimu peke yao! maana hata walimu wakifanya vizuri kiasi gani, na nyie mnashadadia kupigwa wao viboko msitimize ya kwenu, hali itaendelea kuwa ngumu tu.
Hali mbaya katika nchi yetu haijaletwa na walimu, au madaktari, bali wana siasa. Hata perfomance mbaya ya walimu chanzo ni wanasiasa hawa hawa wakina Yamungu na Mnali type.
 
ameikosaje hiyo nidhamu,kwa kusema ukweli au?
nyie ndiyo wale wa nidhamu ya woga.ukiwa kwenye keyboard mafisadi mafisadi,ukikutana nao uso kwa uso hehe hehe muheshimiwa,tehe tehe tehe!!

Umeshapata ile kazi ya usalama wa viongozi na chama cha SISI M? Bwahahahaha
 
Afu mnataka rais awe effective wakati uzembe huko kwenye DNA ya watanzania.

Ha ha ha ha, eti uzembe uko kwenye DNA ya Watanzania!!! ama kweli baadhi ya Watanzania ndivyo walivyo!!! When you have nothing important to say it is better to keep QUIET.
 
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, James Yamungu amejitokeza hadharani na kukanusha habari zilizoandikwa juzi na baadhi ya magazeti kuwa hakuunga mkono kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali.

Yamungu aliyasema hayo jana jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya habari zilizoandikwa na magazeti hayo matatu ya kila siku, huku akisisitiza kuwa yeye binafsi na familia yake walizipokea taarifa hizo kwa mshtuko na masikitiko makubwa na amepanga kuyashtaki magazeti hayo Baraza la Habari.

"Ndugu zangu nimekuiteni hapa kuwaeleza habari zile kwenye magazeti yote matatu, zimeniletea usumbufu mkubwa, nimeona walivyoamua kunidhalilisha na kunitenganisha na familia yangu na uongozi wa serikali na kwa Rais wangu, walivyoamua kunichonganisha na walimu na walivyoamua kulifanya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kuonekana dhalili, watu wasiofaa katika jamii," alisema Yamungu.

Yamungu alisema kimsingi anaamini kuwa habari hizo kwenye magazeti yote matatu, ambapo ziliandikwa kwa nyakati tofauti zilikuwa ni za uchonganishi na zililenga kumchonganisha yeye na serikali na kwamba habari zote zilizoandikwa zilikuwa ni za lengo binafsi zaidi.

Alisema kuwa hata hivyo mwandishi aliyeandika habari katika gazeti mojawapo lililotolewa Februari 27 hawakuwasiliana naye ama ana kwa ana hata kwa simu na alikuja kushtukiwa akipigiwa na ndugu na watu wakimweleza juu ya habari hiyo ya mwanzo iliyochapishwa na gazeti hilo ikimkariri yeye kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na aliyekuwa DC wa Bukoba ya kuwachapa walimu viboko.

"Ukienda kwenye magazeti yote, utaona muundo wa uandishi wa stori (habari) ni ule ule, na utaona ni mwandishi yule yule mmoja, na kutokana na strori ya tarehe 28 Februari, Mhariri aliamua kuniandikia tahariri juu ya habari hiyo iliyoandikwa juu yangu, ya kuwa nimeonyesha utovu wa nidhamu kwa Rais kwa kuunga mkono kauli ya DC huyo aliyefukuzwa kazi, kwa nini chombo hiki cha habari hakikutafuta walau nafasi ya kuzungumza na mimi, huyu mhariri nguvu hii ya kunihukumu mimi bila ya kunipa haki yangu ya natural justice (nafasi ya kujieleza) kaitoa wapi?," alihoji Yamungu.

DC huyo amesema kuwa siku zote katika utendaji wake wa kazi amekuwa akitii miiko ya kazi ya ukuu wa wilaya kama alivyoapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yamungu alisema baada ya kutafakari yote hayo ameamua kuchukua hatua aliyoiita ya awali kufikisha shauri lake kwenye Baraza la Habari la Tanzania (MCT), kwa madai kuwa ndicho chombo kilichopo kwa mujibu wa taratibu kinachoshughulika na mambo mbalimbali ya vyombo vya habari.

"Suala hili ni zito na ninachokusudia kufanya ni kutafuta haki kwenye vyombo vinavyotoa haki, nimeamua shauri hili nilifikishe kwenye Baraza la Habari kwa hatua zaidi na niweze kutendewa haki juu ya suala hili, maana ninaamini kuwa ndicho chombo cha awali cha kushughulikia masuala kama haya ya kwangu kwa vyombo vya habari, na kesho (leo) ninatarajia kwenda kwa Mwanasheria wa Serikali Kanda ya Tabora kwa ushauri zaidi wa kisheria," aliongeza.

"Mwandishi aliandika sicho, wakati nilipokuwa nikizungumza na wanachama wa Saccos kule wilayani kwangu, tafsiri aliyoitoa juu ya DC Mnali sivyo nilivyoizungumza yeye aliipotosha na kwa sababu tulikuwa tumetofautiana, aliona hiyo ndiyo nafasi ya kuandika kile alichokiona kwa mtizamo wake," alisema Yamungu.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, James Yamungu amejitokeza hadharani na kukanusha habari zilizoandikwa juzi na baadhi ya magazeti kuwa hakuunga mkono kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali.

Yamungu aliyasema hayo jana jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya habari zilizoandikwa na magazeti hayo matatu ya kila siku, huku akisisitiza kuwa yeye binafsi na familia yake walizipokea taarifa hizo kwa mshtuko na masikitiko makubwa na amepanga kuyashtaki magazeti hayo Baraza la Habari.

“Ndugu zangu nimekuiteni hapa kuwaeleza habari zile kwenye magazeti yote matatu, zimeniletea usumbufu mkubwa, nimeona walivyoamua kunidhalilisha na kunitenganisha na familia yangu na uongozi wa serikali na kwa Rais wangu, walivyoamua kunichonganisha na walimu na walivyoamua kulifanya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kuonekana dhalili, watu wasiofaa katika jamii,” alisema Yamungu.

Yamungu alisema kimsingi anaamini kuwa habari hizo kwenye magazeti yote matatu, ambapo ziliandikwa kwa nyakati tofauti zilikuwa ni za uchonganishi na zililenga kumchonganisha yeye na serikali na kwamba habari zote zilizoandikwa zilikuwa ni za lengo binafsi zaidi.

Alisema kuwa hata hivyo mwandishi aliyeandika habari katika gazeti mojawapo lililotolewa Februari 27 hawakuwasiliana naye ama ana kwa ana hata kwa simu na alikuja kushtukiwa akipigiwa na ndugu na watu wakimweleza juu ya habari hiyo ya mwanzo iliyochapishwa na gazeti hilo ikimkariri yeye kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na aliyekuwa DC wa Bukoba ya kuwachapa walimu viboko.

“Ukienda kwenye magazeti yote, utaona muundo wa uandishi wa stori (habari) ni ule ule, na utaona ni mwandishi yule yule mmoja, na kutokana na strori ya tarehe 28 Februari, Mhariri aliamua kuniandikia tahariri juu ya habari hiyo iliyoandikwa juu yangu, ya kuwa nimeonyesha utovu wa nidhamu kwa Rais kwa kuunga mkono kauli ya DC huyo aliyefukuzwa kazi, kwa nini chombo hiki cha habari hakikutafuta walau nafasi ya kuzungumza na mimi, huyu mhariri nguvu hii ya kunihukumu mimi bila ya kunipa haki yangu ya natural justice (nafasi ya kujieleza) kaitoa wapi?,” alihoji Yamungu.

DC huyo amesema kuwa siku zote katika utendaji wake wa kazi amekuwa akitii miiko ya kazi ya ukuu wa wilaya kama alivyoapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yamungu alisema baada ya kutafakari yote hayo ameamua kuchukua hatua aliyoiita ya awali kufikisha shauri lake kwenye Baraza la Habari la Tanzania (MCT), kwa madai kuwa ndicho chombo kilichopo kwa mujibu wa taratibu kinachoshughulika na mambo mbalimbali ya vyombo vya habari.

“Suala hili ni zito na ninachokusudia kufanya ni kutafuta haki kwenye vyombo vinavyotoa haki, nimeamua shauri hili nilifikishe kwenye Baraza la Habari kwa hatua zaidi na niweze kutendewa haki juu ya suala hili, maana ninaamini kuwa ndicho chombo cha awali cha kushughulikia masuala kama haya ya kwangu kwa vyombo vya habari, na kesho (leo) ninatarajia kwenda kwa Mwanasheria wa Serikali Kanda ya Tabora kwa ushauri zaidi wa kisheria,” aliongeza.

“Mwandishi aliandika sicho, wakati nilipokuwa nikizungumza na wanachama wa Saccos kule wilayani kwangu, tafsiri aliyoitoa juu ya DC Mnali sivyo nilivyoizungumza yeye aliipotosha na kwa sababu tulikuwa tumetofautiana, aliona hiyo ndiyo nafasi ya kuandika kile alichokiona kwa mtizamo wake,” alisema Yamungu.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
Mkuu Balantanda salam,
Kukosekana kwa matamshi "SIMWOGOPI RAISI WACHENI UOGA" katika original post yanayodaiwa kuwa DC Yamungu aliyatoa,inaonyesha kwa asilimia kubwa kuwa hayo ni VICHOCHEZI vilivyopandikizwa na mwandishi wa habari husika. ni vema Yamungu achukue hatua alizokusudia.
 
Haya kumekucha! jamaa kaona mambo yamekuwa magumu...
 
Back
Top Bottom