Simwelewi sheikh huyu!

Status
Not open for further replies.

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Ni shehe anayeendesha kipindi cha ARISALAH kwenye kituo cha Channel 10.

Jana nilibahatika kumsikiliza kwenye redio fulani ambapo pamoja na yeye alialikwa Askofu Gamanywa. Ndugu zetu hawa muhimu katika maswala ya kiimani pamoja na mambo mengi waliyoyajadili ni suala la viongozi wa dini kuingilia mambo ya kisiasa.

Shehe huyu mbali na kutotaja jina lakini alionekana wazi akimpiga vijembe Kakobe na kumlaumu kwa kitendo chake cha "kuwaelimisha waumini wake elimu ya URAIA" Lakini pia hakuacha kumwagia sifa kemekem mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa ni jasiri, anafuata utawala wa sheria, ametuongoza vizuri na wezi wote wa fedha za umma wamefikishwa mahakamani. Hakusita kuonyesha kukubali kwake uamuzi wa JK kuwasifia na kuwapigia debe hadharani wale wenye kesi mahakamani za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. Kwake yeye na alikuwa anataka kutulazimisha tuamini kuwa watu wale watakuwa na hatia pindi tu mahakama itakaposema watu wale ni wevi kweli. (hatujui ni baada ya miaka mingapi uamuzi utatolewa na watu wale wataendelea kula kuku tu)

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa:

1. Katika kipindi chake cha ARISALA aliwahi kusema Endapo CCM isingeleta mahakama ya Kadhi basi yeye angezunguka Tanzania nzima ikiwezekana kwa mguu kupiga mbiu ya wananchi kutoichagua CCM.
2. Aliwahi kusema kuwa si busara kumchagua Rais ambaye hana ndoa na kwamba akiapa atakuwa anaapa kwa kutumia kitabu gani cha dini maana biblia inakataa uzinzi na Rais huyo akichaguliwa akiwa hana ndoa tafsiri ni hiyo kuwa tutakuwa na rais mzinzi.
3. Kupitia Radio Kheri aliwahi kusikika kuwa waislam wasiwe na waswasi na CCM kwakuwa JK hakuhusika kuandaa ilani iliyowekwa ahadi ya mahakama ya Kadhia na aliyeweka ni BWM, Maleccella pamoja na Mangula so wakristo wanaunga mkono mahakama hiyo.

Wakati yeye ni kinara wa kumkoromea kakobe kuwa anachanganya dini na siasa yeye, pamoja na Magazeti yake ya ALHUDA pamoja na ANNUUR wanashabikia Udini kwa asilimia 100%.

Mfano, Alhuda ya Jana ilikuwa na habari ya kuwachonganisha waislamu wema na Dokta slaa. Kichwa Cha habari kilisema Mpangoi wa Dkt Slaa wakwama. Eti kwa research waliyofanya Alhuda, Wakatoliki wapo Milioni 8 ambao wote wangempigia kura Slaa. Kwakuwa hesabu za Slaa na Chama Chake ni kuwa Wapigakura ni milioni16 kabla tume "haijachomekea" wapigakura milioni3 maana yake Slaa alikuwa na uhakika na nusu ya kura za wapigakura wooote (uchochezi wa uongo). Eti tume imeharibu mkakati wa Slaa.

Wanajamvi, viongozi wa dini wa namna hii tuwafanyeje?
 
ni kiongozi wa kupuuzwa kamuulize aliposomea, zaidi ya kubwabwaja tu, kiongozi wa dini bila elimu ni upuuzi mtupu.
 
Naogopa ku-comment but hawa jamaa na magazeti yao hata siyaelewi
 
Ndugu yangu usipoteze muda wako kumsikiliza mtu mwenye upeo mdogo na fikra mgando!
 
:biggrin1:Mwaka wa uchaguzi kaaaaaaaaaaazi kweli kweli, taatibu jamani titaonana wabaya.
 
Hayana mwelekeo magazeti ya aina hii.Wanatenda ujinga huo kwa kujua kabisaaaaa.Sijui nini wanachofaidi,huku wakidai kumkomboa mwanadamu kumbe ni kumwangamiza kabisa kwa kutumia kigezo cha mnyazi mungu.
 
Waislamu msikubali kutumiwa na watu ili kuwabeba kisiasa. Hawa mashehe ubwabwa, na magazeti uchwara yanajifanya yanatoa maoni ya waislamu, kumbe wanatoa maoni ya watu wenye nia zao za kisiasa...
 
Tetete,inabdi nitabasamu kdgo wana Jf, uyu shehe kzidi sana nanajua kwnini anasema hyo,lkn navyo dhni anaupeo mdogo,kwani uo uzinzi anautafsiri kwa imani gni? Hlo ndyo swali la kuhuriza,kwa wakrist mtu mwenye mke zaidi ya mmoja yeye anakuamzizi?sasa ukianza kuhukumu kwatfsiri za imani bsi ata JK nayeye ni mzizi au babu Ally Assahn mwinyi ni mzizi....huyu shehe ni mnafiki sanaa,anahukumu wengne yeye anajiona safi..2mpuhuze 2
 
kuna Radio Imanai ya Morogoro, Gazeti la AlNoor, Habari nyingi wanazozitoa zinaelemea kuwapigia debe Viongozi wa KiIslam Dr. Jakaya na Prof.Lipumba na kumdhofisha Dr. slaa
 
Achana naye! Hawa ndo wanaofanya nchi yetu ionekane ina udini. Wanasema tz hakuna udini, ila upande wa wenzetu
:dance:
 
Poor thinking capacity

Nani kamwambia kuwa kuwa mkristo ndo inakupa maono ya kujua uzuri wa chama cha chadema na viongozi wake. Wangapi ni wakristo wazuri lakini wako na ccm damdam na wala hawajui na wanadanganyana ndani ya CCM?

Watu kama hawa sijui wanatokea wapi jamani! Sasa eti huyu naye ni kiongozi wa group fulani katika society yetu, hao anaowaongoza si watakuwa zero kabisa jamani.

Hawa ndio type ya watu wanaokitetea chama cha mapinduzi na hizo ndo defending point zao za kwanini unatakiwa kumchagua kikwete

Hamna kitu, zero kabisa.

Chagua chadema, vote for Dr slaa
 
JF kiboko!Kipindi Kakobe anampigia dede slaa alisifiwa huyo!Shehe akipmponda slaa hana elimu!!!duuh!!!
 
Nilimsikia jana. Pia alikiri kuwa hata shehe Yahaya anaingilia siasa lakini akasema hawezi kumsemea. Wakati huo huo akawa anabeza usemi uliosemwa na Methodius Kilaini (PHD)kuwa JK ni chaguo la Mungu akilalama kuwa na yeye Kilaini aliingilia siasa kinyume cha taratibu. Ila wao wakiingilia siasa hakuna neno.
 
Aliwahi kusema kuwa si busara kumchagua Rais ambaye hana ndoa na kwamba akiapa atakuwa anaapa kwa kutumia kitabu gani cha dini maana biblia inakataa uzinzi na Rais huyo akichaguliwa akiwa hana ndoa tafsiri ni hiyo kuwa tutakuwa na rais mzinzi- POINT!!!!
 
Ukiuliza slaa amelifanyia nini taifa hili hupati jibu, ukiuliza kwanini unampigia kura slaa utaambiwa anaongea sana mpaka povu linamtoka! siasa za bongo bwana yaani wewe ujue kuongea sanaaaaa ndio utafagiliwa kama hujui kuongea basi wewe hufai kuongoza hawajui kama uongozi sio kuongea sana ni vitendo.

Watanzania ni watu wa ajabu sana likifanywa jambo na upande wao hata kama ni baya wanalishabikia. Kakobe alipompa tano Slaa watu walifurahia ila Kilaini akisema JK chaguo la Mungu anasakamwa mbaya zaidi sheikh akijitokea akisema JK anampa tano ataambiwa hana elimu kazi yake kuzaliana!

Wajameni hebu fikirieni nje JF I mean out of the box
 
Nina amini leo naweza kuwa cuf kesho nccra na mwakani chadema lakini daima nitakuwa muislam tukana chama changu usitukane dini yangu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom