Simulizi ya kutisha kortini jinsi albino alivyochinjwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
headline_bullet.jpg
Yaelezwa muuaji alikunywa damu




[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi wa pili katika kesi mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino), ameieleza Makahama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza kuwa alimuona mshtakiwa wa kwanza, Kazimili Mashauri, akimchinja mdogo wake, Mariam Emmanuel (5) na kwamba aliwaambia wakipiga kelele na wao watauawa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sehemu ya mahojiano baina ya shahidi huyo, Nhindi Emmanuel, anayesoma darasa la tano na Wakili wa Serikali, Ayub Mwenda, mbele ya Jaji Projest Rugazia anayesikiliza kesi hiyo, yalikuwa kama ifuatavyo:[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Usiku mkiwa mmelala kilitokea nini?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Walituamsha watu watatu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Waliwaambia nini?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Lala ukipiga kelele na wewe tutakuua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Walishika nini?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Mmoja panga, wa pili kisu na sufuria na wa tatu tochi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Baada ya kuwaambia lala walianza kufanya nini?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Walianza kumchinja mdogo wetu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Nani alikuwa anamchinja?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Kazimili.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Wawili walikuwa wanafanya nini?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Mmoja alikuwa anakinga damu kwa kutumia sufuria.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Mwingine?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Anamulika tochi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Baada ya kumchinja nini kilifanyika?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Kazimili alikunywa damu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Nini kilifuata baada ya kumchinja?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Walimkata miguu marehemu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Ulimtambuajie Kazimili?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Alimulika tochi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Kazimili alikuwa anaishi wapi?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Palepale kijijini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili: Baada ya kuondoka ulifanya nini?[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi: Nilienda chumbani kwa babu kumwambia, nilimwita babu, babu, lakini hakuamka. Baadaye akaja mjomba naye aliendelea kumuita, baadaye ndio akaamka.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi huyo aliiambia mahakama kuwa alimueleza babu yake kuwa Mariam amechinjwa na Kazimili na ndipo babu yake aliwasha taa na kwenda kuangalia.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akihojiwa na wakili anayemtetea mshtakiwa wa kwanza, Willbard Butambala, kama wauaji hao walimpiga, shahidi alimweleza Jaji Rugazia kuwa Kazimili alimpiga kwa panga mgongoni[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika tukio lingine, Jaji Rugazia aliamua kutumia hekima zake baada ya shahidi wa tatu katika kesi hiyo, Jesca Emmanuel au Ndashaba kutoelewa maana ya kiapo na madhara ya kusema uongo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Shahidi huyo ambaye alishindwa kutaja umri wake, alimweleza Jaji kuwa anasoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Ukiriguru wilayani Misungwi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Huku akiongozwa na mkalimani, Jackson Tinapo, aliyetafsiri maswali kwa lugha ya Kisukuma, mtoto huyo alisema hajui alianza lini shule, masomo anayosoma na kwamba mtihani walifanya mwezi wa pili.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kutokana na hali hiyo, Jaji Rugazia alisema shahidi huyo haonekani kuelewa na sio vizuri kumfundisha maana ya kiapo, hivyo kumruhusu kutoa ushahidi wake bila kuapa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kesi hiyo namba 42 ya mwaka 2009 inawakabili washtakiwa wawili, Kazimili Mashauri (48) na Mathias Italanga (60) maarufu kama Mahona.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mauaji ya Mariam yalitokea Januari 21, mwaka 2008, saa 10 alfajiri katika kijiji cha Nyangh’olongo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Jumanne ambapo mama wa marehemu, Flora Mabula, alitoa ushahidi kabla Jaji Rugazia kuiahirisha hadi jana. Kesi hiyo itaendelea leo.[/FONT]




CHANZO: NIPASHE

Hawa Wanaouwa Maalbino ningeomba Serikali iwachukulie hatuwa kali sana
 
Wauwaji nao wauawe kama walivyoua, hao wanaotetea haki za wauwaji wakiuliwa watoto wao wa kuwazaa wenyewe wataendelea kuwatetea?
 
Hakuna haki inayoitwa ya binadamu kwa mwuaji. Kama hakuona maana ya binadamu wengine kuishi, hakuna haja ya kumwona mtu wa aina hiyo kama binadamu. So hayuko kwenda kundi linaloguswa na kanuni za haki za binadamu kwa sababu tayari yeye si binadamu
 
Back
Top Bottom