Simulizi: Mwanafunzi Mchawi (A Wizard Student)

Babu delegate power tu kwa wenye kuijua wakusaidie, hivi unatupa mshawasha alafu unakaa tena week ndo unaleta tena bhana..
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA

....DOREEN alikuwa bado hana hali nzuri kiafya, mwili wake ulikuwa hauna nguvu kabisa kwani ile adhabu aliyoipata usiku ilimwadhibu haswa. Alijikuta anamwogopa Nadia kupita kiasi, moyoni mwake alikiri kuwa kweli Nadia Joseph alikuwa Mchamungu kweli.

Wakati huo akiwa bado yupo kitandani akiugulia maumivu, Doreen alifikiria jinsi ya kuweza kupata titi la msichana mrembo ili akamilishe kazi yake aliyotumwa kuifanya. Siku zilikuwa zimeisha sana lakini alijipa moyo kuwa ameshamaliza kazi kwani kupata titi aliona kama kazi rahisi tu ingawa ilishaanza kupata vikwazo.

Doreen alishuka kitandani kwake. Akavua nguo zote kisha akasogelea begi lake na kuchukua shanga nyeusi akaivaa shingoni mwake.

Na kwakuwa alikuwa peke take chumbani mle Doreen alifanya mambo yake bila woga. Akachukua kichupa kimoja kidogo kwenye begi lake halafu akamimina kidogo unga unga uliokuwamo mle na kujipaka usoni kisha akapiga magoti chini na kuinamisha kichwa chake huku akitamka maneno Fulani.

Ghafla karatasi ambayo ilifanya mauaji ya walimu ofisini ikamjia mkononi make.Ikumbukwe kuwa karatasi ile ilichukuliwa na mwalimu Jason ambapo kulikuwa na maandishi yaliyomuonya kuwa asimpe mtu mwingine, hivyo Mwalimu Jason aliamua kukimbia nayo na alikuwa akikaa Nayo kwa siku zote zile.

Doreen alitabasamu baada ya kuitazama karatasi ile, akaishika vizuri kwa mikono miwili kisha akasema "NENDA KWA MWALIMU JASON! MWAMBIE ANILETEE TITI LA MSICHANA MREMBO! NAKUAMINI!" alisema Doreen kisha akaiachia karatasi ile, ikapaa hewani na ikapotea.

Doreen alifurahi sana akajua tayari amekwisha maliza kazi yake. Akiwa bado ameketi pale chini akiendelea na mambo yake mengine ghafla mlango wa bweni lake ukagongwa halafu akakumbuka kuwa hakuubana mlango ule vizuri kwa komeo Doreen alishtuka sana kwani alikuwa mtupu na alikuwa na maunga unga usoni. Akahisi fumanizi la uchawi tayari limemfikia.

********
Mansoor alikubali kumsaidia Dorice ili kumwokoa Eddy lakini bado moyo wake ulimuuma sana. Hakuwa radhi kumwacha binti yule kirahisi pasina kumuoa ilhali moyo wake ulizimia kwa mapenzi kwa mrembo yule. Mansoor alimpenda sana Dorice hivyo akajiona bwege sana kumwacha msichana yule aondoke kwenye himaya yao wakati moyo unamhitaji.

"Mwanamke anahitaji kubembelezwa! Nikimbembeleza sana anaweza kunikubali.... Yawezekana anamuogopa mama yangu kutokana na vitisho alivyompa... Mhh nitajaribu tena bahati yangu kwani moyo wangu hautakuwa na amani kabisa nikimuacha Dorice!" Aliwaza Mansoor akiwa ametulia peke yake kando ya Maua mazuri yanayotoa harufu ya kuvutia. Aliwaza sana juu ya kumpata Dorice lakini bado hakuona njia sahihi ambayo ingekubalika haraka zaidi ya kumshawishi tu huba na kumbembeleza kwa mahaba.

Akiwa katika wingu hilo zito la mawazo Mansoor alishtushwa na upepo mkali. Akajua moja kwa moja mama yake alikuwa njiani kwani upepo ule zilikuwa in hatua za Malkia. Punde si punde malkia akatia timu na kuketi kando ya Mansoor.

"Vipi mwanangu? Mbona unasononeka sana kiasi cha kuondoa amani ya moyo wangu?"
"Hakuna tatizo mama!" Alijibu Mansoor huku akijaribu kuachia tabasamu.
"Unanificha Mansoor.. Au yule binadamu asiyejaa hata kiganjani bado anakusumbua?"
"Hapana mama.. Hana tatizo lolote na anaonesha moyo wa kunipenda!" Ilibidi Mansoor amdanganye mama yake kwani alijua madhara ambayo angemfanyia Dorice kama angemweleza ukweli.
"Kweli?" Malkia alifurahi.
"Kweli mama yangu.. Malkia mtukufu..!" Alitabasamu Mansoor ingawa moyoni aliumia.
"Vizuri sana... Nadhani furaha yako itarejea sasa!"
"Ndio mama wala usiwe na wasiwasi!"
Malkia aliondoka zake akiwa ameghairi lengo lake la kumwangamiza Dorice. Kwani alipanga kuondosha uhai wake endapo angekataa kumpenda Mansoor.

Mansoor alimfuata Dorice kwenye chumba alichokuwa anaishi. Aliingia chumbani mle akiwa amemletea zawadi ya maua mazuri yanayonukia vizuri sana. Alipoingia tu, akasikia sauti ya kilio kutoka kwa Dorice. Mansoor akashtuka kidogo kisha akamsogelea taratibu Dorice.

"Unalia mini Dori?"
"Nataka nirudi nyumbani... Wazazi wangu watakuwa wananitafuta sana..!"
"Usilie Dorice...!"
"Siwezi kuzuia maumivu yangu juu ya wazazi wangu Mansoor... Pia namfikiria mpenzi wangu..!"
"Nyamaza Dorice.. Nitakusaidia kwa yote hayo... Hebu nitazame!" Mansoor alimkazia macho Dorice kisha akamkabidhi Maua aliyokuwa ameyashika.
"Yanini..?"
"Usijali.. We pokea tu.."
Dorice aliyapokea maua Yale huku akisitasita sana. Baada ya kuyapokea mansoor alitabasamu sana.
"Asante kwa kupokea zawadi yangu Dorice... Nakupenda sana!" Dorice hakujibu kitu zaidi ya kumshangaa Mansoor.
"Nataka nikusaidie... Upo tayari..?"
"Nipo tayari Mansoor tafadhali.."
"Sawa Dorice.. Kabla sijakusaidia nahitaji unisaidie kitu.."
"Kitu gani!?" Dorice alishtuka sana.
"Nataka uolewe na Mimi.. Tafadhali Dorice... Nitakusaidia kwa lolote utakalo ukikubali kuolewa na Mimi..!"
"Mansoor! Nilishakwambia nampenda Eddy..."

"Ukikubali kuolewa na Mimi nitakusaidia kumpata Huyo Eddy na nitakuruhusu uendelee Naye... Nakuomba Dorice! Ilidhishe nafsi yangu!" Alisema Mansoor huku akipiga magoti.

*******
Mwalimu Jason alikuwa akisumbuliwa sana na karatasi lile alilolichukua ofisini baada ya kifo cha Mwalimu Mbeshi. Halikutakiwa kuonekana na MTU yeyote wala kuguswa na maji.

Lilikuwa likimchanganya sana kichwa kwani kila siku lilikuwa likibadili ujumbe na kuandika masharti mapya.Siku hiyo asubuhi mwalimu Jason kutokana na kutokwenda kazini aliamka asubuhi na mapema ili afue nguo zake.

Alikusanya nguo chafu zote na kuziweka kwenye beseni la kufulia lenye maji na sabuni. Na alikuwa na uhakika kabisa kuwa karatasi halikuwa kwenye nguo zile. Akaanza kufua nguo zake kwa umakini ili azitakatishe ndipo alipogundua kuwa suruali yenye karatasi lile la maajabu ipo ndani ya beseni la maji.

Kengele ya hatari ikagonga kwa kasi moyoni mwake, akaipoa suruali ile huku mapigo yake ya moyo yakimpiga kwa kasi.

Akaanza kutafuta karatasi lile kwenye mifuko ya suruali ile. Hofu ikamzidia maradufu baada ya kutafuta kila mfuko na kulikosa karatasi lile.

Mwalimu Jason alichanganyikiwa sana, ikambidi aanze kupekua suruali zake zote na kutafuta vizuri karatasi lile alikuwa akiliita karatasi la kifo kwani kila mara lilikuwa likimuonya kuwa akikosea sharti basi lazima afe.

Mwalimu Jason alipekuwa kila suruali aliyokuwa ameiloweka kwenye maji lakini bado hakuona karatasi akazidi kuchanganyikiwa.

Alizitupa chini nguo zote kisha akaingia ndani na kuanza kupekua kwenye kila suruali lakini bado hakuona karatasi lile. Mwalimu Jason alipigwa na butwaa. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka kila kona ya mwili wake. Akajitupa kitandani na kuanza kulia kwa woga. Alijua tayari kifo kiko mbele yake si muda mrefu.

Ghafla simu yake ikaita na kwakuwa alikuwa kwenye kilio hakuweza kupokea simu. Akaicha tu bila hata kuingalia.

Lakini kwa bahati njema aliona karatasi ikiwa pembeni ya mto wake wa kulalalia. Mwalimu Jason alifurahi kisha akaichukua karatasi ile na kusoma ujumbe mpya ulioandikwa hivi "MSICHANA YEYOTE ATAKAYELALIA KITANDA HIKI.. UNATAKIWA UMKATE TITI LAKE LA KUSHOTO HARAKA IWEZEKANAVYO. LASIVYO UHAI WAKO UTAFIKIA KIKOMO!"

Mwalimu Jason akatumbua macho kwa mshangao. Akarudia kusoma ujumbe ule mara mbilimbili lakini hakuna kilichobadilika. Akahisi mwili wake unaishiwa nguvu kabisa kwani Siku ile alikuwa na miadi na mpenzi wake. Alijiuliza atafanya nini hakuwa na la kufanya.Simu take ikaita tena akaitazama ilikuwa ni namba ya mpenzi wake. Akapokea.

"Baby mbona hukupokea simu?"
"Ulipiga?" Jason alijifanya kama hajui lolote kama simu ilipigwa.
"Kwani hukuona? Ok.. Nipo njiani nakuja!"
"Eeeh!" Jason alishtuka sana.
"Vipi mbona unashtuka?"
"Ah..una.. Naomba usije home Leo.. Kama vipi tukutane Hotelini.."
"Hivi Jason una akili timamu wewe? Hapo kwako kuna nini? Au una MTU mwingine?"
"Sina MTU mwingine baby.. Ila.." Jason alitamani kujitetea ila hakuweza kufanya hivyo.
"Nitoke Dar kuja Iringa kwaajili yako halafu uniletee hizo habari zako.. Kwani tulikubaliana nini?" Msichana yule alimjia juu mwalimu Jason
"Usipaniki baby basi.. Hotelini ni kuzuri pia..!"
"Kama una michepuko yako basi tutajua..!"
Msichana yule akakata simu.

Mwalimu Jason alijiona ana mtihani mkubwa sana. Aliwaza na kuwazua lakini bado hakupata jibu. Majira ya SAA Kumi na nusu jioni mlango uligongwa. Mwalimu Jason alienda kufungua akakutana USO kwa uso na sura ya Judith ambaye ni mpenzi wake akiwa amenuna sana.

Mwalimu Jason hakuwa na la kufanya zaidi ya kumkaribisha Judith ndani.Waliposalimiana tu Judith akaingia chumbani kwa mwalimu Jason ili akaweke mizigo yake.Lakini kila alipomtazama Mwalimu Jason, hakuwa na furaha hata kidogo.

"Mbona hujanifurahia?"
Aliuliza Judith
"Nipo kawaida.. !" Alijibu mwalimu Jason.
"Ok basi ngoja nikapumzike kidogo maana nimechoka kweli..!" Alisema Judith huku akipiga hatua kuelekea kitandani........

ITAENDELEA....
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA

..... MANSOOR alimtazama Dorice kwa jicho la kiulizo lililomtaka azungumze chochote lakini Dorice hakusema neno zaidi ya kuangua kilio cha huzuni baada ya kukosa msaada kwa Mansoor. Dorice alilia sana kwani alijua kurudi tena duniani sasa ni ndoto.

"Mansoor naomba unisaidie!" Dorice alipiga magoti akamsihi Mansoor aweze kumsaidia ili arudi kwao pia amsaidie kumwokoa Eddy ili furaha ya penzi lake irudi.

"Dorice! Naweza kukusaidia kwa yote hayo... Ila inabidi ukubali kuolewa na Mimi maana bila hivyo mama yangu hatonielewa...!" Mansoor alisisitiza.
"Siwezi kuolewa na wewe..!"

"Kwanini? Au kwa vile Mimi sio binadamu mwenzio? Jua nakupenda na nitakuruhusu kuendelea na Eddy.. Nielewe Dorice!" Mansoor alizidi kumweka Dorice katika wakati mgumu sana. Kwani kiukweli Dorice aliuhitaji msaada wa Mansoor ila masharti yake yalikuwa kikwazo sana. Dorice alishindwa kung'amua juu ya mtihani ule mzito. Alijua fika wazazi wake wataumia sana endapo wakijua kuwa Hayupo duniani, aliyafikiria maumivu ambayo mama yake angeyapata kama yeye angepotelea kule kwenye ulimwengu wa majini.

"Sijui nimkubali halafu akinirudisha duniani nimkatae?" Dorice Alizidi kuwa na utitiri wa mawazo kichwani mwake. Ghafla akashtushwa na sauti nzuri ya mahaba ya Mansoor akizidi kumshawishi kuwa amkubalie ili aweze kumsaidia kutatua matatizo yake.

"Dorice! Nifanye nifurahi tafadhali.. Nilipendwa na wengi ambao si chaguo langu.. Nasikitika chaguo langu linakuwa mwiba moyoni mwangu! Kwanini lakini?"

Dorice alivuta pumzi ndefu na kuishusha taratibu, huku akiwa ameinamisha kichwa chake. Taratibu akanyanyua kichwa chake na kumtazama Mansoor. Macho yake yalistaajabu uzuri wa asili aliokuwa nao kijana yule. Hata kama majini ni wazuri lakini Mansoor alizidi kipimo, kuanzia macho yake, pua yake na midomo mizuri ya kupendeza sana.

"Nimekubali Mansoor! Ila kabla ya yote naomba uniahidi kama utanisaidia!" Alisema Dorice kwa sauti iliyotulia sana. Maneno hayo yalifungua ukurasa mpya moyoni kwa Mansoor, alifurahi kupita kiasi akamkumbatia kwa nguvu Dorice.

"Nakuahidi kukusaidia Dorice!" Alisema Mansoor akiwa amemkumbatia Dorice.
Walikumbatiana kwa muda kisha wakaachiana. Mansoor akamtazama Dorice huku akitabasamu.
"Nataka uvae vizuri nikupeleke kwa mama yangu muda huu!"
"Nitavaa nini? Sina nguo!"

Alisema Dorice kwa woga huku moyo wake ukimsuta kwa kumsaliti Eddy kwani alikwisha muahidi kuwa hatokuwa na mwanaume mwingine yeyote zaidi yake."lakini ni kwa sababu yake..!" Alijipa Jibu Dorice.

"Unapenda nguo gani?" Aliuliza Mansoor.
"Nguo yoyote itakayonifaa!" Alijibu Dorice.
Mansoor alinyoosha mkono juu ghafla ukatokea mfuko mmoja wenye ukubwa kiasi kisha akamkabidhi Dorice. Dorice aliogopa sana, akasita kupokea.

"Usiogope.. Chukua!"Dorice akapokea mfuko ule japo kwa woga kisha akaufungua ili atazame kilichomo. Akapigwa na bumbuwazi.
*****
Eddy aliwaacha wazazi wake barabarani pale wakiwa hawaelewi la kufanya. Walibaki wanatazamana kwa muda wa dakika tano nzima bila kusema neno lolote. Kila mmoja alionekana kutoelewa kilichotokea.

"Mr. Alloyce.. Tutakuwa wazembe tena wajinga... Mtoto ameondoka tumesimama tu kama milingoti hapa!" Alisema mama Eddy.

"Tufanyeje mke wangu?"
"Tumfuate!"
"Tutamfuata wapi sasa?"
"Kokote, kwani we hujaona alikokimbilia?"
"Dah! Tuna mtihani mzito!"

Ilibidi waingie msituni na kuanza kumsaka Eddy. Walimtafuta kila kichaka lakini hawakuona hata dalili za uwepo wa kijana wao. Jua liliwawakia huku wakizidi kumtafuta Eddy lakini bado hawakuona hata dalili za kumpata.

"Hili tatizo la kimwendokasi dah!" Alisema baba Eddy.
"Inabidi tulitatue kimwendokasi!"alijibu mama Eddy akiwa ameshika mkono kiunoni. Anahema kupita kiasi kutokana na uchovu aliokuwa nao.
"Mke wangu!"
"Abee.."
"Mimi naona turudi tu nyumbani hapa tutafanya kazi bure!" Alishauri Mr.Alloyce
"Nilishasema wewe humpendi mwanangu.. Turudi nyumbani halafu?"

Mama Eddy alimjia juu mumewe, akaona kama hana mapenzi wala uchungu kwa mwanae lakini baba Eddy alikuwa sahihi kabisa kwani mpaka pale walipofikia wasingeweza kumpata Eddy. Walikuwa wamechoka sana, pia wasingeweza kusonga mbele zaidi kutokana na ukubwa wa msitu waliokuwamo.

"Sikiliza mke wangu.. Nataka turudi tutafute njia sahihi ya kumtafuta mtoto hapa tunazidi kupoteza muda!" Kwa shingo upande mama Eddy aliamua kusikiliza ushauri wa mumewe. Wakatembea umbali mrefu sana mpaka walipolifikia gari lao.
Walipofika kwenye ile gari, kengele ya hatari iligonga mioyoni mwao wakatazamana kwa mshangao lakini hawakuwa na la kufanya kwani gari yao ilikuwa ikiteketea kwa moto mkali utadhani imemwagiwa petroli.

"Nini hiki?" Walijiuliza kwa pamoja bila kupata jibu la haraka. Ilibidi wasogee kwa ukaribu ili wahakikishe wakionacho. Ni kweli gari yao ilikuwa ikiwaka moto, na alikuwa hatua za mwisho kiasi kwamba hata wangezima moto ule bado gari yao isingesalimika.

"Haya maajabu!"
"Tena maajabu haswaaa ya ulimwengu..!"
Wakiwa bado wanaendelea kushangaa ajali ile ya moto kwenye gari ile, ghafla moto ukazima kama vile umezimwa kwa maji halafu gari ikatoweka machoni mwao.
Waliogopa kupita kiasi wakajikuta wanatimua mbio bila kutazamana.

Walikimbia sana wakiifuata barabara, kwa bahati mbaya mama Eddy alijikwaa na kuanguka chini kama gunia. Damu nyingi zikaanza kumtoka mguuni. Akapiga kelele Kali za maumivu, zilizokatisha mbio za Mr.Alloyce. akageuka nyuma na kumwona mkewe akivuja damu nyingi sana. Akarudi haraka.

"Vipi mke wangu?"
"Nime..nimeumia Mme..wangu..!" Mama Eddy aliongea kwa shida sana kwani alipata maumivu makali sana.
Walikuwa hawana hata mia mbovu mifukoni mwao kwani pesa zote waliziacha kwenye gari ambalo limepotea kimaajabu.
"Mke wangu" aliita baba Eddy baada ya kuona mkewe anakoroma isivyokawaida.
"Mama Eddy..!!!!!!"
*****
Mwalimu John alikuwa bado anatokwa na funza mguuni, alitaka kuieleza familia take juu ya kile kilichompata lakini pindi alipotaka kuiambia familia yake juu ya mkasa ule mzito ghafla akapigwa Kofi zito lililomrusha kama shoti ya umeme kutoka juu ya kiti mpaka chini. Alipiga yowe Kali lililowashangaza watu wote sebuleni pale. Waliogopa sana.

Leyla mke wa Mwalimu John alimsogelea mumewe na kumwangalia kama yupo salama ghafla akapigwa na mshangao ulioambatana na furaha kwani miguu ya mwalimu John ilirudi katika hali ya kawaida na haikuwa na funza tena.
"Mume wangu!" Aliita Leyla kwa Furaha, lakini John aliendelea kulalamika pale chini kwani Kofi alilopigwa lilikuwa zito kuzidi uzito wa mwili wake lakini hakujua limetoka wapi.

"Jamani.. Njoo muone maajabu..!"
Alisema Leyla akiwaambia ndugu wengine wa mumewe.Wote walimsogelea na kushangaa kilichotokea, wakakiri kwamba kweli dunia ina maajabu tena yanayotisha na kuogopesha.

Mwalimu John aligalagala pale chini kwa muda wa kama robo saa kisha taratibu akainuka. Alipotazama miguu yake aliifurahia sana kwani ilikuwa imerudi kwenye hali yake ya kawaida. Akainuka pale chini na kumkumbatia kwa furaha. Lakini cha ajabu kila alipotaka kuzungumza chochote..

*****
Doreen alibaki ametulia kimya pindi mlango unagongwa. Aliona anachofanya ni ujinga ni heri ainuke avae nguo kabla hajafumwa. Alipoinuka tu mlango ulifunguliwa. Doreen alishtuka sana kwani alikuwa yupo uchi wa mnyama na alikuwa amevaa shanga huku usoni amejipaka maungaunga na kumfanya awe na mwonekano wa kutisha.

Madamu Amina akiwa ameambatana na nesi wa shule walishtuka sana kukmkuta Doreen akiwa vile. Walitazamana kwa mshangao kisha wakamtazama Doreen kwa hofu.

"Doreen unafanya nini?" Aliuliza Madam Amina kwa woga ingawa alikikaza tu. Doreen alibaki kimya tu bila kujibu chochote. Macho ya Madam Amina yalitua moja kwa moja kwenye kile kichupa cha dawa kilichokuwa pale chini tena kilikuwa kimefungwa kijitambaa kidogo cha kaniki kwa juu. Kiliwatisha sana.

"Doreen! Unafanya nini? Mbona hujibu?" Alisema nesi kwani walikuwa wamefikishiwa taarifa kuwa Doreen ni mgonjwa ndio maana amebaki bwenini.
Itaendelea.....
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom