Simuelewi

Maega

Senior Member
Jul 10, 2010
156
30
From the bottom of my heart kuna mdada mmoja nimempenda na tangu tumekuwa marafiki (wa kawaida tu) zaidi ya mwaka sasa nimeona ana sifa za kuwa wife wangu na tumekuwa tunawasiliana vizuri kama marafiki wenye mwelekeo wa watu wanaoelekea kuwa wapenzi na yeye anafahamu wazi kuwa I am interested to her japo sijamtamkia tu . Sasa hivi karibuni kama wiki 2 zimepita (nakumbuka mara ya mwisho kuwasiliana nae yeye ndio alnipigia simu tukaongea vizuri tu na hakuna shida yoyote katika urafiki wetu huo) najaribu kuwasiliana nae bila mafanikio kwani nikipiga simu hapokei wala sms hajibu na hata nikikutana nae akiniona tu ananipishia mbali sasa nimeleweje ndo ananijaribu, niji-conside unsucessfull au nimpotezee tu? though nampenda
 
ww umeenda kwa watu ukakalia kupiga stori, mwenzio kaingia kaomba jamvi kapewa! sasa ww bado unawaza jinsi ya kuomba jamvi ambalo halipo tayari. ww ndo hueleweki!
 
Inabidi umtamkie kuwa unampenda iliasionekama unamwekea kwa uzibe kwa wengine ambao wanamtokea na wana nia kama yako ya kutaka kumwoa!
 
Inabidi umtamkie kuwa unampenda iliasionekama unamwekea kwa uzibe kwa wengine ambao wanamtokea na wana nia kama yako ya kutaka kumwoa!

Chris unalolizungumza ni kweli kabisa, ila tatizo ndo hataki kuwasiliana na mm
 
Kuna uwezekano kuna mwenzio kaja na tembocard mastercard full mistari,sasa we kila siku unaongelea habari za gadafi tu mkiwa naye unategemea nini?
 
Kaka unaambiwa strike the hammer while IRON is hot! ilishawahi nitokea mie nikiwa form 2 baba, demu alinipenda mwenyewe akanitangaza mwenyewe kwamba mie ndo mshika dau pale, mzee nikariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiinga, haaaaaaaaa si dereva teksi akafanya mambo, tena akampa na mimba na mtoto mpaka leo yupo nadhani form 4 sasa, ila demu alijiharibia akaacha shule sasa hivi anauza ki stationary maana dereva tax aliingia mitini. kwa kweli akili ziliponijia nikaenda kuomba mchezo kumbe tayari demu ana ujauzito akawa anacheka tuu! Mkuu usifanye tena kosa kama hilo! hapo ujue demu anakudharau sana kishapata jamaa linamdungua kibandidu, pindua pindua, wewe eti a good boy uikuwa unasubiria kengele ilie hahahaaahaaaha
 
Ndo uelewe sasa! We utakaaje na mtoto siku zote hizo alafu ushindwe kumwaga vyombo!! Siku nyingine ukiwa na njaa usivunge!!
 
Mueleze ukweli kama alikua anakupenda atarudi kwako na nyie wanaume wengine hasa mnanishangaza,mwanamke anawataka mnajitia uzuri mnjipandisha bei msokua nayo sasa nyie mkiringa sie tufanyeje?
 
Pole mkuu, kuwa ktk mahusiano ya normal friendship hakumfanyi mtu asiwe katika mahusiano ya kimapenzi na mwingine, I think its already too late kwako. Nahisi mwenzio sasa hivi anaweza akawa anakuchukulia kama kaka yake koz kwa namna mmoja au nyingine atakuwa na shemeji yako.
 
alisha kusoma janja yako.wewe unachoma kwingine ukienda kwake anaambulia story tu.mwenzangu ulizidi..mwaka mzima unang'ang'a macho!.ulimgeuza dada yako au?kweli penye miti hamna wajenzi.ningekuwa mimi duh!,yaani siku tatu tu kwisha habari yake.mia
 
Aise,watch out! huyo mpotezee mbali,atakuwa kishapata smbody else. Mwaka wote huo ulikuwa unasubiri nini? Ulitakiwa walau ujenge mazingira fulani ili naye ajue kuwa kuna future btn you 2!
 
From the bottom of my heart kuna mdada mmoja nimempenda na tangu tumekuwa marafiki (wa kawaida tu) zaidi ya mwaka sasa nimeona ana sifa za kuwa wife wangu na tumekuwa tunawasiliana vizuri kama marafiki wenye mwelekeo wa watu wanaoelekea kuwa wapenzi na yeye anafahamu wazi kuwa I am interested to her japo sijamtamkia tu . Sasa hivi karibuni kama wiki 2 zimepita (nakumbuka mara ya mwisho kuwasiliana nae yeye ndio alnipigia simu tukaongea vizuri tu na hakuna shida yoyote katika urafiki wetu huo) najaribu kuwasiliana nae bila mafanikio kwani nikipiga simu hapokei wala sms hajibu na hata nikikutana nae akiniona tu ananipishia mbali sasa nimeleweje ndo ananijaribu, niji-conside unsucessfull au nimpotezee tu? though nampenda
unasubiri nini hapo? ingekuwa ndo unaanza kumzoea/kumtongoza, ningekushauri uendelee, lakini kwa situation yako dawa ni kusepa tu, kashakuchoka huyo
 
Hebu tulia kwanza na ufanye uchunguzi wako taratibu aidha uongee naye au kupitia kwa watu wake karibu ujue sababu ni nini,wanafiki hawachelewi kufikisha fitina kuhusu wewe thats why anakupotezea!!
 
Back
Top Bottom