Simu za Blackberry kuboresha Maisha ya Watanzania!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Kama kuna ujinga uliokubuhu na kupata PHD, ni kutoka kwa Serikali yetu na Wanasiasa wetu.

Ni vipi leo tudai Blackberry simu yenye uwezo wa kupata mtandao wa intaneti ndio iwe kichocheo cha kuboresha maisha ya Mtanzania?

Nilifikiri Elimu, Afya, Chakula, Ajira, Bei nzuri za Mazao,Maji, Umeme Kilimo bora, Uvuvi na Ufugaji wa kisasa ndio vyanzo vya kuboresha maisha.

Zaidi ongezea Siasa Safi na Uongozi katika vitu muhimu kuongeza ubora wa Maisha na kuleta maendeleo katika Taifa.

Sasa kule kijijini Simu ya intaneti itamsaidia nini mwanancho ambaye hana umeme wa kuchaji hiyo simu na ni lazima atembee maili 3 kwenda kwenye umeme wa kuaminika?

Je hizo gharama za mawasiliano tunazolalamika kila siku za kutaka miundombinu ya mawasiliano ibadilishwe, itasaidia vipi ufanisi na kuboresha maisha ikiwa bado tunatumia mitambo na utandawazi wa zama za kale?

Kinachosikitisha ni hili tamko lenye mamlakakuwa kijisimu cha Blackberry kitaboresha maisha ya Mtanzania!

Ama kweli Mtanzania unaendelea kudanganywa na Serikali yako na kufanywa mjinga kila siku!

Maisha Bora kwa kila Mtanzania kupitia Blackberry!

Serikali yaipongeza Vodacom kuzindua Blackberry

na Amana Nyembo

SERIKALI imeipongeza Vodacom Tanzania kwa kuzindua simu za kisasa za Blackberry kwani zitaboresha maisha ya Watanzania.

Akizindua simu hizo mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki, alisema simu hizo zenye kasi kubwa ya intaneti zitasaidia kuboresha maisha ya Watanzania.

Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na mtandao wa Vodafone imezindua simu mpya na ya kisasa ya Blackberry nchini yenye mvuto wa aina yake na uwezo mkubwa wa kuzuru internet pamoja na huduma ya kutuma na kupokea barua pepe popote nchini.

Awali, Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephahim Mafuru alisema simu kwa kuanzia na Vodacom kupitia mtandao wa Vodafone wamezindua simu za Blackberry za aina mbili ambazo ni Curve 8310 na Pearl 8110 mahsusi kwa wateja wa malipo kabla na baada.

Alisema lengo la kuzindua huduma za simu hiyo ni kuboresha mawasiliano na maisha ya Watanzania, kwani mawasiliano ya uhakika ni jambo muhimu la maendeleo.

Baadhi ya faida ya simu hiyo ni kuwa wateja binafsi na wafanyabiashara wenye anuani za mitandao, wanaweza kupata huduma za mitandao kama vile ya Yahoo, Hotmail, Gmail na mingineyo bila wasiwasi wowote na kwa muda wote.

"Kutokana na ubora wa huduma ya simu hiyo Watanzania kwa mara nyingine wanapata bidhaa bora kutoka Vodacom ambayo itawasaidia kuboresha maisha yao," alisema. Kwa wateja wa malipo kabla, wanaweza kujiunga na huduma za Blackberry kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi yenye alama sahihi kwenda namba 123 na kuunganishwa na huduma ya kuzuru ya internet pamoja na huduma ya kutuma na kupokea barua pepe kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kujiunga tena.

Mteja anaweza kuandika Blackberry1 kama anataka kutumia huduma ya internet kwa siku 30 kwa sh 36,000 au Blackberry3 kama anataka kutumia huduma ya internet kwa siku 90 kwa sh 99,000 na Blackberry6 kama anataka kutumia huduma hiyo kwa siku 180 kwa sh 180,000 na kisha kutuma namba 123.
 
Inakasirisha kweli... ulimbukeni to the core. Rev. Kishoka, siwezi hata kuandika mengi kuhusiana na hili... i'll curse!!
 
Inakasirisha kweli... ulimbukeni to the core. Rev. Kishoka, siwezi hata kuandika mengi kuhusiana na hili... i'll curse!!

Heheheheheheeeee.....I want to say something but I'm not gonna...heheheheheheeee
 
Heheheheheheeeee.....I want to say something but I'm not gonna...heheheheheheeee
:) :D...... wewe sema tu bana, usijiminye minye tu bure usijevimba mashavu kama hizo nanihii zinazobembea na kushangaza watoto.....kama kuchapia ni jambo la kawaida, kama ni hoja tutaijadili, au vipi?!... lol
 
Mbona wakuwa kaa una jazba yakhe....? Forgot to take that stuff or what?
 
Mbona wakuwa kaa una jazba yakhe....? Forgot to take that stuff or what?
... naah, am of good spirits dude, worry not. lest mess up otherwise good thread dawg. ila ungenistua ulichotaka sema ingekuwa fresh zaidi au vipi, anyway poa tu, baadae
 
Nimeona keywords mbili hapo: VODACOM + Serikali

CCM ni Adui wa Maendeleo ya Tanzania na Watanzania

.
 
Watanzania huwa hawakosi kudanganywa hata kwa vitu vya kijinga kama hivyo na wengi uingia mkenge.
Kama ni internet mbona wameanzisha huduma nyingi za jinsi hiyo?
Kuna internet ya kwenye simu ya kiganjani na wana ile wanaita 3G na sasa wanaongeza wizi mwingine zaidi?
Zile zingine zime prove failure nini?
Utakuta mtu ananunua lisimu la 1 millioni ili aonekane kwa watu kwamba wamo. Lakini mwenye simu ya 40 elfu mbona baye mawasiliano ni yale yale?
Sana sana ni kujiweka kwenye risk ya vibaka kukukata mkono.
 
Ngoja nilale kwanza ntakuja kesho....na mtizamo...ila Kishoka u have a point here.
 
Rev,

Mtanzania anayeongelewa hapo ni Mbenzi, mwenye nyumba kedekede kama John McCain kutokana na ufisadi. Mtanzania ambaye ana purchasing power kutokana na ma foreign bank accounts yaliyo na hela nje kama Chenge, amabaye ana uwezo wa ku bill simu hizi ofisini bila ya kutiliwa mizengwe wala kuulizwa uzalishaji unawezake kuruhusu manunuzi ya huduma hizi.

Mtanzania wa kijijini ambaye umeme hana hata hiyo simu ya kawaida haipati, na akiipata haitamsaidia maana ataichaji vipi?

Inabidi tujenge kutoka chini kwenda juu, siyo kutoka juu kwenda chini.

Na wanaposema "Blackbery kuboresha maisha ya Mtanzania" inabidi wai qualify hiyo sentensi kwa kuielezea zaidi kwamba mtanzania huyu ni yule anayeweza kwenda kwenye mikutano au matanuzi Sea Cliff Hotel, Kempinski au hiyo Sheratoni inayobadilika jina kila wiki mpaka sijui inaitwaje sasa hivi (Movenpick is it?)

Watu wa Sinza kwa Remmy tu hapo -hujafika hata Mbagala Rangi Tatu, Mkuranga au Kisarawe - hawana running water wanaishia kununua maji ya mapipa. Wenye umeme hawawezi hata kupikia katika majiko ya umeme kwa kuhofia Luku na lockdown yake kama ya Soweto enzi ya mkaburu, leo unasema maisha yataboreka kutokana na Blackberry?

Yataboreka kwa hao ma fat cat executives wa kampuni za simu wanaochaji exorbitant fees ambazo hazipo sehemu yoyote ile duniani.
 
.... hapana, sasa hivi inaitwa Waitara Lodge baada ya kubadilishwa kutoka Tanzania Tax Exemption Inn!!! :) :D
 
Huy anachekecha kweli badala ya kuongelea report ya watu wa Tanzania Bureau of Statistics na jinsi gani ataimprove hizo failure walizoonyesha yeye anaongelea matumizi ambayo kwa mtanzania wa kawaida na walio wengi hawawezi kufanya.
Waandishi muulizeni kwanini watu wanatumia kuni zaidi kupikia kuliko umeme? kwanini watu hawaendi hospitali wakiumwa wanabaki kununua dawa wenyewe na kunywa?
Jamani tusaidieni maana nyie ndio mko karibu na hawa watu, waulizeni mpaka wakimbie kukutana na nyinyi, mtu akiwa na kitu kisicho cha msingi kwa mtanzania kama hicho aogope kuwaita.
 
vodacom ni jumuiya ya ccm kama ilivyo uvccm, uwt nk, iko katika propaganda kama akina hiza tambwe nk, ilishaandikkwa sana hapa kuhusu uhusiano wa mafisadi na vodacom, lts move another stage
 
Nashauri huyo waziri akapimwe akili kwanza. By the way huenda hata hajui bkackberry ni kifaa cha aina gani. Bei ya mitandao ya internet ikwa njia ya simu iko juu sana Tanzania. Huku niliko natumia 3G internet na nalipa $30 tu kwa 3GB. Vodacom wanatoza shs 200 kwa 1MB ina maana kwa 3GB unatakiwa kulipa 1024 X 3 X 200 = 614, 400 Tsh. Jamani duu hayo maisha bora yako wapi?

Kama kweli serikali ina nia ya kuboresha maisha ya watanzania kwa njia ya internet kwanza inabidi kuboresha miundo mbinu ili kufanya gharama za internet kuwa affordable.
 
Black Berry....iko na future kibao ambayo hata huyo waziri hawezi kuzitumia...achilia mbali mtanzania wa kawaida ambaya anapanda dala dala yenye watu zaidi ya ishirini ukukasimama..

Blackberry haimsadii mtu kama haujui internet,GPS etc wala hana email...hiii iko kwa watu walioko kwenye kiwango cha mapata ambayo kwanza ni prepaid...na wanalipiwa na company....
Mlala hio kuwa nayo ni kujitakia kukabwa na vibaka na ikipotee na mawazo tuu....hii hesabu juu ambayo mpiganajinambamoja kasema...ni kwa watu wa tabaka la juu watanzania wangi hawawezi hata ku afford dola moja ya kuweka kwenye simu...thanks hakuna kuweka pesa ya kupokelea...MTN na mobitel zamani...ulikuwa huwezi pokea kama hujaweza pesa ya kupokela.

So hii haiji kuboresha maisha zaidi ya kuwaboresha walio wachache waweze kua access accounts zao uko ng'ambo...
 
Mkuu Rev, nilipooanza kusoma habari yako nilikuwa natafuta secondary source ya nani aliyesema utumbo huo. Hii ndio Tanzania, viongozi wenye akili sawa na wagonjwa wa mtindio wa ubongo.

What are correlations between blackberry and reduction of povetry? Mimi bado nazilaumu media kwa kuacha kufocus kwenye remarks za kishenzi kama hizi. What a mess.
 
Nakumbuka makala za Bw. Samson Mwigamba katika gazeti la Tanzania daima zilizokuwa na heading "Je Kuna Tanzania mbili?" Katika makala hizo nilitambua kuwa kuna Tanzania mbili:

a) 20% ya waTz wenye maisha bora, wenye nafasi za kutawala, wenye nafasi za biashara nzuri nk. Hawa ndo wanaofaidi kodi na michango ya waliosalia kwa kupata huduma bora za afya, elimu, nishati, miundombinu nk. Kundi hili haliwajui wenye shida. Linamiliki 80% of total wealth ya Tanzania.

b) 80% ya Wtz, hawa ni walalahoi, walipakodi, wavuja jasho, wasioona matokeo ya kodi wanazolipa, wanamiliki only 20% of total wealth. Hivi karibuni wameanza kuamka usingizini baada ya kushtuliwa na visa vya rushwa kubwa kubwa. Mwanzo walidhani maisha wanayoishi ni mapenzi ya Mungu, lakini sasa fikra zinabadilika kwa kasi sana. Kwa kusaidiwa na baadhi ya waaminifu waliopo kwenye kundi la kwanza, wanaelekea kushinda kama Wazimbabwe.

Fikra hii ya Tanzania mbili ni ya hatari sana, kwasababu inaligawa taifa katika makundi. lakini ndo ukweli uliopo therefore inabidi kuusema ili upate dawa. Nilimshukuru sana Bw. Mwigamba kwa makala hizo.

Sasa huyu Waziri ndo anatia mihuri ya mgawanyiko huu, anaposema Watanzania anamaanisha wale 20%. Wale 80% si Watanzania katika wanaostahili huduma bali walipa kodi, wasiostahili kula matunda ya madini na mali asili mbalimbali za Taifa.

Hapa ndipo tulipofikia sasa, kwasababu ya kuongozwa na matajiri wasijali wanyonge.
 
Back
Top Bottom