Simu ya mkononi

kashata

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
529
536
Wadau nimewahi kusikia kua kuna simu sijui ya kampuni gani ambayo inauwezo wa kusave sms hata kama umezifuta inbox au sent sms.Naomba anayefahamu anitajie ni simu ya kampuni gani na code number yake nataka nikainunue.
 
mkuu pesa yako itakuja kukuua kwa presha.

mi nakushauri hiyo sim usije inunua, coz naisi unataka kununua alaf umpe mpenzi wako!!!!

shauri yako
 
sajafahamu unataka msg za mpaka muda gani huko nyuma? wiki, mwezi au mwaka? nakushauri km una Mtandao wa Voda fika katika ofisi zao utapata maelekezo yote hata na watu uliowapigia, sms, M-Pesa nakadhalika, au chomoa sim-card kwa muda km siku moja halafu irudishie autaziona sms zako na km unamtindo huo jaribu ku-save katika phone
 
Wadau nimewahi kusikia kua kuna simu sijui ya kampuni gani ambayo inauwezo wa kusave sms hata kama umezifuta inbox au sent sms.Naomba anayefahamu anitajie ni simu ya kampuni gani na code number yake nataka nikainunue.

binafsi nafahamu mitindo ya aina mbili ya uhifadhi ujumbe wa maandishi...hii hutegemeana na jinsi simu ilivyoelekezwa.
1. Ujumbe wa maandishi unaweza kuhifadhiwa kwenye kitunza kumbukumbu cha simu...
2. Ujumbe wa maandishi unaweza hifadhiwa katika kipande cha SIM(line ya simu)...

zaidi kama una ujumbe wa muhimu uliufuta basi huna budi kufika katika mtandao husika wa simu
 
Mmmmhh nimetoka mtupu kabisa, kama unataka kuweka mtego umekwisha
 
Nataka nimnunulie mke wangu kuna ukweli nautafuta
 
Wadau nimewahi kusikia kua kuna simu sijui ya kampuni gani ambayo inauwezo wa kusave sms hata kama umezifuta inbox au sent sms.Naomba anayefahamu anitajie ni simu ya kampuni gani na code number yake nataka nikainunue.

Ili ukame shemeji....kwi kwi kwi....
 
Nataka nimnunulie mke wangu kuna ukweli nautafuta

nilijua tu!sasa si unataka kuujua ukweli jiulize haya yafuatayo kabala hujafanya lolote utakaloamua kulifanya
1.Ni mara ngapi unafanay mawasiliano ambayo unajua si salama kwa ndoa yako?
2.Ni mara ngapi unafanya jitihada mkeo asijue umewasiliana na nani?
3.Ukishapata jibu jiulize tena,kwa kufahamu huo ukweli unaotaka kuufahamu unamuacha huyo mke?
4.Ikiwa hujapata huo ukweli unaoamini upo utaamini 100%kuwa mkeo alikuificha kitu?
5.Ikiwa ni ukweli unautafuta huoni kuwa tayari umeshaamini upo bila kuuchunguza?i mean umeshamuhukumu huyo mke?
malizia na ukweli kuwa mwanadamu ni kiumbe complex sana sana yani kuliko unavoweza kuamini!
 
Hata yeye angeamua kupata record ya sms zako just za wiki 4 past lazima angekuta sms isio salama kwa ndoa yenu.
NB:Kama unamtafutia sababu ya kumuacha endelea na zoezi lako la kutafuta hiyo simu. Ila kama unampenda hebu achana na utoto unataka kufanya.NDOA inataka watu waliopevuka kiakili na mwili.
KAMA ANABEHAVU VIBAYA KWENYE MAMBO YA SIMU KAA NAE CHINI KWA USTAARABU UMWELEZE TABIA UNAZOZIPENDA ILI AZIENENDE MAISHA SIO KUTAFUTANA MAISHA KUJIJENGA BWANA.
 
Wadau nimewahi kusikia kua kuna simu sijui ya kampuni gani ambayo inauwezo wa kusave sms hata kama umezifuta inbox au sent sms.Naomba anayefahamu anitajie ni simu ya kampuni gani na code number yake nataka nikainunue.

Mkuu never try to touch the phone of your lover or wife, it is very dangerous
 
Wadau nashukuru kwa ushauri wenu nampenda sana mke wangu ila anakatabia cha kupenda kuchat kupita kiasi mpaka napata presha ndio maana nataka niwe naziona meseji anazochat ili nijilizishe kama ndege wangu yupo salama
 
Back
Top Bottom