Simu ya kufukuza mbu yazinduliwa tz.

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Waheshimiwa kwa wale wanaosumbuliwa na mbu nyakati za usiku, kuna habari njema ya kufurahisha ambayo nimeikuta mtandaoni. Jaribu nawe upitie HAPA.

KAMPUNI ya Samsung Tanzania, imezindua simu ya Samsung Galax Pocket yenye uwezo wa kufukuza mbu usiku, pindi mtumiaji anapowasha.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Belinda Lawuo ambaye ni miongoni mwa watumiaji watano waliopata fursa ya kutumia simu hiyo siku chache kabla ya uzinduzi uliofanyika juzi.
Lawuo alisema alipopata simu hiyo alifurahishwa na uwezo wake wa kufukuza mbu kupitia programu ya Mosquito Repellant.
Naye Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar alisema simu hiyo inampa mnunuzi thamani halisi ya pesa, kwani inauzwa bei nafuu, huku kukiwa na ofa mbalimbali, ikiwemo kutuma ujumbe bure mara 100 kwa mwezi na kifurushi cha intaneti.


 
Leo ndio unasikia kitu hiki? Kama una simu yoyote yenye uwezo wa kubrowse na kudownload google Getjar, humo tafuta AntiMosquito ni application ya bure tu, download hiyo. Nimetumia hiyo kitu mwaka wa tatu sasa.
Samsung kama wamekuja ni kitu tofauti siwezi ku-comment ila kutumia simu kufukuza mbu sio jambo geni kama wanavyotaka tuamini.
 
cyo simu ni application za simu... huyu jamaa alikuwa anawapaisha samsung tu
 
cyo simu ni application za simu... huyu jamaa alikuwa anawapaisha samsung tu

yah ni application na sio simu nakubaliana na wewe.

Inatoa kamlio flan hivi kanapenya kwenye maskio kiaina mbu wanakua hawaupend
 
Mh.Ndebile na Mh.Aaron mambo haya wapo wasiyoyajua tuendelee kutoa shule zaidi. Mh. Manyanza hao jamaa wanasema simu hizo zinauzwa kwa bei nafuu, mie hapo...du! Mh. Zomba thanks, safi sana kwa hiyo elimu, endelea vivyo hivyo....
 
Leo ndio unasikia kitu hiki? Kama una simu yoyote yenye uwezo wa kubrowse na kudownload google Getjar, humo tafuta AntiMosquito ni application ya bure tu, download hiyo. Nimetumia hiyo kitu mwaka wa tatu sasa.
Samsung kama wamekuja ni kitu tofauti siwezi ku-comment ila kutumia simu kufukuza mbu sio jambo geni kama wanavyotaka tuamini.

Mi natumia nokia 5800 na ninayo hiyo application mwaka wa pili sasa.
 
kinachowa fukuza mbu ni mlio au mionzi??? naomba kuelimishwa hapa

tusije kuuana na radioactive radiations si mnajua tena tbs wamelala ..
 
kinachowa fukuza mbu ni mlio au mionzi??? naomba kuelimishwa hapa

tusije kuuana na radioactive radiations si mnajua tena tbs wamelala ..

Tena wamelala usingizi wa pono. Ebu tuwasubiri Mh.NingaR na Mh.Joshamto na wengine wengi watakujibu suala lako.
 
Many of The applications emitt a very unique high frequency sound (ultra sound) that the insects dislike. The pitch of the sound is so high that most humans will not notice anything.But if that Samsung it doesn't emitt sound instead it emitts other radiations which I can't beleave for a cheap phone to have that technology of emitting radiation. Am recommending We use Apps that emitts Sound (Utra Sound) instead of that Samsung Until it has been explained it uses what to scare the Mosquito
 
Siku hizi inalamba vibayamno yaan 400mb zinaisha haraka tofauti na siku za nyuma.
 
Baadhi ya Apps zinatoa sauti kama ya popo ili kufukuza mbu

hiyo sauti inaitwa utrasonic sound huwa popo anaitumia katika kunavigate na kulocate prey, na sio mbu pekeyake huwa hata wale wadudu wanao ruka nyakati za usiku na kuzunguka jirani na taa au mwanga huwa wana uwezo wa ku track hiyo utrasonic sound inayotolewa na popo hivyo wanakimbia kuepuka kuliwa na popo range yake huwa kati ya 20-80kHz ambayo binadau hawezi sikia, ambapo uwezo wa mwanadamu kusikia ni kati ya 1-15kHz.
 
Hizi app na vifaa (kuna saa zinafanya kazi hiyo hiyo) zinadai kuwa zinatoa sauti ambayo ni sawa na sauti za wanyama au wadudu ambao ni adui kwa Mbu kama popo na Dragon Fly, hivyo Mbu akisikia anakimbia.

HAKUNA USHAHIDI WOWOTE KUWA ZINALETA EFFECT YOYOTE KWA MBU, soo ni danganya toto mostly. Pia zinatoa sauti tu so hazina haja ya kutumia data.
 
Back
Top Bottom