Simu kujipiga yafichua siri

Pinda alisema hivi,,"ningekuwa mimi ningeshamfukuzilia mbali Jairo!"Sasa na mimi nasema kwamba ningekuwa mimi ningesha mtimulia mbali huyo mamii.
 
Hili ni tukio la kweli juzi jumamosi saa mbili usiku,jamaa alimuaga mkewe mapema kuwa ataenda saluni kunyoa nywele akitoka kazini saa moja usiku,mkewe akamkubalia ila naye akamuomba akitoka kazini kwake anaomba naye apitie saluni jamaa naye kamkubalia mkewe, ilipofika saa moja na nusu jamaa akawa hajamaliza kazi zake ofisini akaona asiende tena sinza kunyoa,ilipofika saa mbili akmpigia mkewe na kumfahamisha kuwa haendi tena sinza kunyoa atarudi nyumbani hivyo amwambia mkewe asiende tena salon ya mbali aje ya karibu na nyumbani mama akakubali,baada ya dakika tano anaona mkewe anampigia akapokea akasikia mkewe naongea na simu nyingine na nimwanaume,alimwambia baba.........kaniambia nisije tena huko hivyo atuwezi kuonana tena leo,jamaa akatulia tuli kusikiliza mama akendelea kuongea na huyo jamaa yake bila mkewe kujua simu ya pili imejipiga,mama akaendelea kusema unajua max na kupenda sana mume wangu leo nilikuwa nimeamua nikupe penzi langu lote,ila njoo nitaenda salun ya hapa karibu,jamaa kusikia hiyo akapanic na kukata simu na kumpigia mkewe kumweleza alichokisika,mkewe alichanganyikiwa na salun hakwenda tena,akaenda moja kwa moja nyumbani kusubiri hukumu,jamaa alipofika vita ikaanza kwa kumbana mkewe tena wa ndoa amweleze ukweli kuhusu huyo jamaa,mama aweka mambo wazi kuwa huyo jamaa walikutana mlimanicity kama miezi 6 imepita na analimuhonga gari aina ya hopa akaikataa na hajawahi kumpa penzi,ila siku hiyo yangetimia,mama kaomba sana msamaha na kwamba hatarudia tena,sasa kaja kwangu kama msimamizi wa ndoa afanyeje amsamehe au ampe kilicho chake aanze mbele,na mimi nimelileta kwenu wanajf mnishauri cha kumweleza huyu jamaa yangu.asanteni
HADITHI YA MFALME; mfalme alipata taarifa kuwa mkewe si mwaminifu, akawatuma vijana wake kufanya upelelezi. Vijana wale hawakupata ushahidi wa jambo walilokuwa wakilichunguza. Wakamjibu mfalme kuwa jambo lile halina ushahidi. Mfalme akajisemea moyoni, japo ushahidi haupo, inatosha kumwacha mkewe na akafanya hivyo.MAANA YAKE NINI: Wnaume hatujaumbwa kuchangia mapenzi, japo kimaumbile wanawake wengi wanaweza kuchangia mwanaume mmoja. Tafadhari wanawake msinishambulie katika hili, hasa AshaDii.Kwa kanuni za kufumania, hapo hakuna ushahidi. Ushahidi ni kuwakuta wanajamiaana na uume umengia ukeni na ukashuhudia mwenyewe kwa macho.Kwa ufupi kusamehe na kutosamehe vyote vinabeba uzito sawa. Jamaa hatokaa amwamini mkewe tena na atalitenda tendo la ndoa kwa mashaka mpaka siku anawekwa kaburini. Kwa wanawake wakati mwingine huwa wanasahau.Ushauri wangu ni kuwa amsamehe mkewe, ila ajue kuwa mke hajatulia. Hata kama akioa mwanamke mwingine, kuna uhakika gani kuwa hatomtenda sawa na hivyo?KWA UFUPI MAISHA YAMEHARIBIKA, TUNAONA ILI MAISHA YAENDELEE NA SIO KUMPATA MKE/MUME MWAMINIFU (japo wachache wapo).SI MJINI WALA VIJIJINI. KAMA JAMAA ANAKAZI ZA NJJE AENDELEE NAZO, KAMA HANA BASI ATAFUTE JAPO KUPUNGUZA UCHUNGU. MKE ALISHAMEGWA MAMA ANAJIFARAGUA TU.Samahani kwa kukuchosha.
 
Duh......afadhali TRA wabadilishe tena mfumo wa kodi za hizi gari ndogondogo kama Vitz,Hopa,nk......maana zimevunja ndoa nyingi na nyingine ziko hatihati.........mabazazi wanazitumia kama kondom!
 
......huyo kaishatiwa sanaaaa!!jamani,why are we geting married wakati hauna kipaji hiko?tunaishia kuumizana tu,hapo ndoa haina amani tena,eh mungu!!
 
Kwa nini wewe uwaambie chakufanya? hujui mtu akiomba ushauri ni backup anatafuta ila uamuzi amesha chukua?
Kwanza: we waweke pamoja uwaulize maswali fulani fulani
Pili: baada ya saa 2 wape ushauri mzito kuhusu hali yetu ya ubinadamu kutokua kamilifu, wakumbushe walikubali kukaa pamoja hadi kifo kitakapo watenganisha na kadhalika.
Tatu: maliza kwa kuwaambia: sasa tumejua ukweli uko wapi nataka kujua: wewe mume bado unampenda mke wako na uko tayari kumsamehe? na wewe mke: unakubali ulio fanya ni kosa kubwa sana na unaahidi hauto rudi tena?
Hapo wakiamua A au B hakuna kusema wewe ndio uliwatenganisha sababu unawapa nafasi yakujiamulia wenyewe. Ila kila mara egemea upande wa kusameeana kuliko upande wa kutengaana
nimekubaliana na ushauri wako sana kazi hiyo naifanya kesho saa 12jioni hivyo jtano nitawapatia matokeo kama imevunjika au la
 
hopa ni gari gani au ni power tiller...au ulikuwa unataka kusema opa???ngelengele na alusha kote kwetu
 
mambo mengine yanachanganya kweli...gf akizingua nadata wife sijui itakuaje
 
Hadisi hii inatufundisha nini watoto?

na huu ndio mwisho wa kipindi chetu cha Mama na Mwana!
 
Hili ni tukio la kweli juzi jumamosi saa mbili usiku,jamaa alimuaga mkewe mapema kuwa ataenda saluni kunyoa nywele akitoka kazini saa moja usiku,mkewe akamkubalia ila naye akamuomba akitoka kazini kwake anaomba naye apitie saluni jamaa naye kamkubalia mkewe, ilipofika saa moja na nusu jamaa akawa hajamaliza kazi zake ofisini akaona asiende tena sinza kunyoa,ilipofika saa mbili akmpigia mkewe na kumfahamisha kuwa haendi tena sinza kunyoa atarudi nyumbani hivyo amwambia mkewe asiende tena salon ya mbali aje ya karibu na nyumbani mama akakubali,baada ya dakika tano anaona mkewe anampigia akapokea akasikia mkewe naongea na simu nyingine na nimwanaume,alimwambia baba.........kaniambia nisije tena huko hivyo atuwezi kuonana tena leo,jamaa akatulia tuli kusikiliza mama akendelea kuongea na huyo jamaa yake bila mkewe kujua simu ya pili imejipiga,mama akaendelea kusema unajua max na kupenda sana mume wangu leo nilikuwa nimeamua nikupe penzi langu lote,ila njoo nitaenda salun ya hapa karibu,jamaa kusikia hiyo akapanic na kukata simu na kumpigia mkewe kumweleza alichokisika,mkewe alichanganyikiwa na salun hakwenda tena,akaenda moja kwa moja nyumbani kusubiri hukumu,jamaa alipofika vita ikaanza kwa kumbana mkewe tena wa ndoa amweleze ukweli kuhusu huyo jamaa,mama aweka mambo wazi kuwa huyo jamaa walikutana mlimanicity kama miezi 6 imepita na analimuhonga gari aina ya hopa akaikataa na hajawahi kumpa penzi,ila siku hiyo yangetimia,mama kaomba sana msamaha na kwamba hatarudia tena,sasa kaja kwangu kama msimamizi wa ndoa afanyeje amsamehe au ampe kilicho chake aanze mbele,na mimi nimelileta kwenu wanajf mnishauri cha kumweleza huyu jamaa yangu.asanteni

Mwambie amsamehe ni shetani tu kapita, wanawake tukikengeuka huwa tunakuwa woga sana hasa soo likishabumburuka basi ujue bye bye!! msomee vipengele vya kwenye biblia (usinambie hujui), mpe mifano hai kuhusu maisha. At the end mwambie kwamba hukumu iko mikononi mwake!
 
Ampige chini haraka huyo hafai, mi nafikiri kwenye ndoa dhambi ya mwisho kabisa mwenzako kukufanyia ni kucheat, kwahiyo kama yeye alikuwa tayari na huo mpango huyo ni kwamba hafai. Hata ukilazimisha kuendeleea kukaa naye kwamba umsamehee tu, ukweli ni kwamba mapenzi yenu hayataweza tena kurudi kama awali, na pengine kero ndio itakuwa kubwa zaidi. kifupi huyo ampige chini.
 
Swaga zao sawa sawa! mimi naona wasameheane wakae kwa amani ya bwana. Blv me huyo mdada akiendelea na huyo jamaa wa nje ujue nikibaka mzoefu! amuonyeshe njia ya kurudi kwao mahenge! lol

Ila wanaume nina ka swali kamoja kwenu, wanaume wengi wamekomaa sana kufukuza hatamuamini tena, hizi ndoa hizi kama wanawake tungekuwa hivyo unafikiri kuna mtu angekuwa na ndoa? Wanaume mmezidi ubaka, mambo yote hadharani, mnarudi na condoms nyumbani ukiuizwa unajibu uharo sisi tunangaalia tu game!! Hii issue ya Mkuki kuwa kwa Nguruwe kwa Binadamu mchungu nahisi imepitwa wakati. Kama wewe ni mwizi basi ukiibiwa kuwa mpole!
 
Maisha ni ghalli kwa maana yanahitaji kuchukuliana ebu suluhisho liwe kuelewana bila kuvunja ndoa.
 
Hiyo gari ya Hopa kwanini ameikataa wakati ni toleo jipya hata mtaani hazijaingia?
 
Ampige chini haraka huyo hafai, mi nafikiri kwenye ndoa dhambi ya mwisho kabisa mwenzako kukufanyia ni kucheat, kwahiyo kama yeye alikuwa tayari na huo mpango huyo ni kwamba hafai. Hata ukilazimisha kuendeleea kukaa naye kwamba umsamehee tu, ukweli ni kwamba mapenzi yenu hayataweza tena kurudi kama awali, na pengine kero ndio itakuwa kubwa zaidi. kifupi huyo ampige chini.

Acha kumshauri mwenzio pumba wewe kama yeye hajawai kumsaliti mwenzie ata siku moja na amwache mkewe
 
Kama hii ndo kazi ya msimamizi wa ndoa, sisimamii tena ndoa...
 
mmh?hapo ngumu kumeza na pia ngumu kutema,hii kitu isikie tu kwa mwenzako,ampe kwanza likizo mke kupisha uchunguzi kabla ya kutengana,hata ivyo jamaa ana moyo wa chuma,lol?
 
Back
Top Bottom