Simbachawene ni mchapa kazi na Muadilifu, kwa vyovyote vile akiwa Waziri atalifaa Taifa letu, I hope Mkuu atapepesukia upande wake...
magamba at work....kaka hamisi umechafuka tangu ulipoenda against umma pale rev square muhimbili
Simbachawene ni mchapa kazi na Muadilifu, kwa vyovyote vile akiwa Waziri atalifaa Taifa letu, I hope Mkuu atapepesukia upande wake...
Jamaa yuko Udom anaongeza Elimu, kutokana CCM kuwa na Wabunge wengi Vilaza huyu anafaa kupewa Uwaziri, sisemi hivi kwa sababu ya kufahamiana naye ila jamaa ni Gentleman ambaye akipewa fursa anaweza kulitumikia Taifa, nadhani hata akiwaga Mwenyekiti wa Bunge huwa anamzidi hata Spika Makinda kwa kuliendesha Bunge.
Huyu huyu kwa kauli yake alisema ni kheri raia wafe kuliko polisi kujeruhiwa au kufa!
Akimaanisha raia kupigwa risasi ni sawa tuu
Nakumbuka aliposema hayo na miwan yake usoni
Huyu huyu leo awe waziri kazi tunayo
Wakuu!
Kweli mna moyo wa chuma. Hivi ni nani msafi ndani ya Chama Cha Mafisadi kiasi kwamba mna matumaini makubwa kiasi hiki?
Huyo mteuaji mwenyewe anashindwa amuweke nani maana akiaangalia wote ni wale wale. Kwamba ana fanana nao!!!!!!!!!!!
Umenena mkuu jamaa ni mnafiki kwisha kazi huwa anauma na kupuliza kama hauko makini unawezazani ni bonge la mzalendo kumbe ndo walewale chama kwanza.Nchi hii unafiki unalipa...nimekua nikimsililiza katika mijadala mbalimbali anavyojifanya kutetea sera za CCM kwa hoja zisizo na mashiko na zinazomfichua kama mtu wa kujipendekeza kwa watawala. Sioni namna mtu kama huyu anavyoweza kuchangia katika kuleta ukombozi wa mwananchi wa tanzania kutoka katika lindi la dhuluma, udhalilishaji, maradhi na ujinga.