Simbachawene kalidanganya bunge?

On a serious note,

Nadhani ametumia tafsida, chai ni rushwa kwa hiyo ana maana hakuna Mtanzania anayeshindwa kupokea rushwa.


Kwa hiyo hajadanganya bunge hata kidogo
Kweli kila mtu ana tafsiri yake ya chai.
 
Simbachawene anastahili kuwaomba radhi wananchi wa jimbo la Kibakwe na watanzania wa tabaka la chini kwa maana kauli yake haiongelei hali halisi ya wananchi wa tabaka la chini na km ukiwekwa into account inaweza kumnyima rizki masikini ambaye amepewa shibe ya kwenye jukwaa ili hali hali ni tete kabisa kiuhalisia
 
Simbachawene anastahili kuwaomba radhi wananchi wa jimbo la Kibakwe na watanzania wa tabaka la chini kwa maana kauli yake haiongelei hali halisi ya wananchi wa tabaka la chini na km ukiwekwa into account inaweza kumnyima rizki masikini ambaye amepewa shibe ya kwenye jukwaa ili hali hali ni tete kabisa kiuhalisia

Awaombe radhi kwa lipi? yeye si alichaguliwa kwa vijisent vyake? yeye na wapiga kura wa kibakwe walishamalizana kwenye uchaguzi huu ni muda wake wa kurudisha salio.
Bio data ya Simbachawene: ni mmiliki wa bar inayoitwa TITANIC iko pale vingunguti na ni mcheza pool mahiri. kusikia na yeye ni mbunge siku hizi inaondoa hata maana halisi ya kuwa na bunge.
 
hana tofauti na wabunge wanaosema wanaiunga hoja mkono lakini katika maelezo yao matatizo
kibao sasa kuunga kwao hoja sijui huwa wamesimamia upande gani?unafiki tu
 
Huyo jamaa amechanganyikiwa na posho. Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Yaani kelele zote zinazopigwa hata na wabunge wenzake wa magamba hazieleweki. Huyu ni miongoni mwa wale wanaolala ndani ya bunge. Malizeni Budget muje huku vijijini mtatukuta . Wananchi wameandaa bakora, peoples power itawashughulikia.
u
najua viongozi wa CCM wakikuona unatembea bila viatu basi wanajua umevisahau nyumbani.....
 
Yeye kama binaadam Nadhani aliteleza ulimi tu, nina uhakika atakuwa alikuw anawazungumzia watanzania wa Jimboni mwake, na atakuwa alikuwa anamaanisha maji yaliyochemshwa kwa mchai-chai, na siyo kama alivyokosea kwa kusema chai ile ya majani na sukari......ameteleza tu jamani.....
 
Hana aibu hata kidogo uongo mchana kweupee,chai imekuwa ni kiburudisho sehemu nyingi za nchi kwani wengi hawawezi kuipata ebu wabunge wa CCM wafumbe macho kidogo wawaonee wananchi huruma kama Zitto alivyosema
 
Hii ndio tatizo la kuchagua wabunge ambao ni wachumia tumbo na masharobaro, huyu inabidi asikilizishwe wimbo wa NYUMBANI NI NYUMBANI HATA KAMA KICHAKANI wa TMK WANAUME FAMILY. NANI kakwambia WAGOGO wanapiga tea wagogo hawahawa wanao omba hata vipande vya nyama pale MNADANI DODOMA? yaani wale wa town ni ombaomba balaa je wa huko KIBAKWE?

Huyo mbunge anaona aibu kujulikana kwamba jimboni kwake kibakwe watu hawanywi chai hivyo anadhani akisema wanakunywa ndio tutaona kunamaendeleo saaaaana. DAR kwenyewe CHAI utata itakuwa kibakwe? aende akawadanganye wapiga kura wake maana ndio walio zoea kudanganywa ndio maana wanamchagua huyo msema uongo(sharabaro/ bishoo) maana ni mabishoo na masharobaro ndio uona haya/aibu kueleza ufukara wa kwao maana wanataka kuonekana wao ni matawi ya juu
 
......mhhhhhhhhhh kachemsha, kwanza pale tu vingunguti anapoishi kama bado anaishi huko kuna majirani zake wengi hawanywi chai.
 
Kiufupi ni kwamba wabunge wa CCM wana 'sera bendera',wanaongea lugha moja kana kwamba walifundishwa cha kuongea kabla ya kuzama mjengoni.
 
Bila samahan usemalo ni kweli.......wakat wa uchaguz hupewa pilau,flana na khanga tu
Jimboni kwake wamechoka tu kule..wagogo wana shida sana..tatizo akili zao zimekaa kuomba omba tu (samahani sana watani zangu wagogo, ila ndio ukweli). Nimewahi kuwa Kibakwe kule hadi Wota kule mlimani kwa wagogo wahehe (huko wanajua ushirikina tu!!)
 
Back
Top Bottom