Simba yaifanyia mauaji Prisons

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
TIMU ya soka ya Simba imeweza kuendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifunga Prisons ya Mbeya mabao 3-1 katika mchezo uliomalizika dakika chache zilizopita katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kona iliyochongwa na beki Ramadhan Wasso katika dakika ya pili ya mchezo huo iliweza kuunganishwa vyema na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na kuiandikia Simba bao la kwanza katika mchezo huo.

Baada ya kuingia kwa bao hilo, Prisons walikuja juu na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 27 lililofungwa na Yona Ndabila baada ya kuiwahi pasi ya Osward Morris na kufunga kirahisi.

Simba ilipata penati katika dakika ya 30 iliyofungwa vizuri na Mussa Hassan ‘Mgosi’. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Simba waliopata bao la tatu katika dakika ya 57 lililosababishwa na raia wa Nigeria Izuchukwu.

kocha wa Simba Patrick Phiri alifurahia ushindi huo kwa kusema; “Vijana wangu wameanza kunielewa”.

Habari zaidi NIFAHAMISHE dot com
 
Ni ajabu maana sijawahikusikia marehemu ana kesi ya kumuua marehemu.
Sasa hapa leo kuna kesi ya marehemu mnyama kamuua marehemu mfungwa:D
 
Simba yaani kushinda leo tu kero tupu! Mbona mna tofauti za pointi karibu 20 na Yanga!

Team nayoihofia Ni Kagera Sugar..ajabu nao wamelala 2-0 kwa Toto Africa kule Kaitaba!

Hakuna wa kumkaribia Yanga!
 
Last edited:
Yayaya Yeboyebo mwaka huu hana mpinzani kwa kweli, Mnyama simba ni sawa na mtu alie pata division four kwnye darasa la watu wenye division one , then wakatangazwa wamefaulu, lakini division four ni sawa na msindikizaji tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Back
Top Bottom