Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Nimekuwa nikifatilia kwa karibu mwenendo wa soka latu hapa Tz, kwa muda mrefu nimekuwa nikiona kabisa (kwa mtazamo wangu) kuwa hizi timu mbili za Simba na Yanga huenda zinachangia sana kudidimia kwa mchezo huo. Nasema hivyo kwa nini? Nguvu nyingi katika uwekezaji katika soka kwenye ngazi ya club zaidi kufanyika katika timu hizi mbili. Nakumbuka mwaka jana tu TBL walitoa udhamini kwa Simba na Yanga na kuzipatia mabasi madogo mawili kila timu. Juzi TBL walitoa vifaa vya michezo kwa timu hizi eti ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi. Najiuliza hivi hawa wadhamini/wafadhili hawawezi kwenda kuwekeza kwenye timu nyingine tofauti na Simba au Yanga? Huko mikoani kuna timu zenye wachezaji wazuri sana lakini nyingi hufikia kufutika ramani ya soka Tz kwa kukosa uwezo. TFF kama vinara wa soka nchini hebu jaribuni kuwashauri hao wafadhili basi wabadirike basi na kufadhili na timu nyingine ili kuweza ku-balance rasilimali na hatimaye kukuza soka letu......