Simba ijilaumu ikishindwa kuing’oa Mazembe

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KUNAmambo mawili katika soka; mosi, ni maendeleo ya soka katika mpangilio wa ukuzaji wa vipaji, pili ni kushinda mchezo bila kujali mpangilio wa maendeleo ya soka.

Na kocha Jose Mourinho wa Real Madrid anaingia kundi la pili, ndiyo maana timu zinazotaka
kushinda mechi zinamtaka sana, lakini wale wanaohitaji mpangilio wa maendeleo ya soka kwa ukuzaji wa vipaji hawamtaki.

Vitu hivi viwili ni tofauti sana katika soka ingawaje vina maana ya jambo moja tu, soka. Unaweza kushinda mechi lakini usiwe na mpangilio wowote ambao unakupa maana ya maendeleo ya soka.

TP Mazembe wanaweza kuwa wana mpangilio mzuri wa maendeleo ya soka, lakini je wanaweza
kushinda mechi zote? Jibu ni hapana.

Je, TP Mazembe inacho kikosi bora kama Raja Casablanca ya miaka ya mwanzoni mwa 2000? Jibu ni hapana. Je TP Mazembe wana kikosi cha kazi kama Al Ahly ya Misri iliyotwaa ubingwa wa Afrika mfululizo? Jibu ni hapana.

Je, TP Mazembe ina kikosi kikali kama Enyimba kilichotwaa ubingwa wa Afrika mfululizo? Jibu ni hapana. Je, TP Mazembe wana kikosi kikali kama cha Simba kilichoitoa Zamalek ya Misri mwaka 2003? Jibu ni hapana.

Ndugu zangu hakuna jambo baya katika soka kama unatumia muda mwingi kujikosoa badala ya kujipanga kushinda mechi. Unaweza kujikosoa katika mpangilio wa maendeleo ya soka,
kwa mfano tunajua Simba hawana kikosi cha Simba B wala C.

Tunajua Simba hawana uwanja wa soka, hawana mpangilio wa mambo ya soka la kisasa. Tunajua Simba hawana mpangilio kama wa Azam FC. Je, suala la kushinda mechi lipoje?
Ukiangalia TP Mazembe utaona ukweli kwamba vikosi vya timu zilizotajwa hapo juu hawavifikii wala kufua dafu.

Ukweli ndiyo huo kwa sababu TP Mazembe wameweza kushinda mechi licha ya kuwa na mpangilio wao wa maendeleo ya soka. Je, kushinda mechi kuna uhusiano wowote na mpangilio wa maendeleo ya soka?

Jibu linaweza kuwa ndiyo na wakati huohuo hapana. Tazama timu anazofundisha Mourinho, akiondoka ni ovyo tu, kwa sababu anachojua ni kushinda mechi. Hata hivyo anajijengea heshima na kutakiwa na timu nyingi.

Samba ifuate sera hii dhidi ya TP Mazembe. Simba imefungwa mabao 3-1 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini ukiangalia soka lenyewe la timu iliyoshinda hakuna kitu kinachoshtua akili za watu makini.

TP Mazembe imeshinda kwa sababu mbili tu; kwanza walikuwa nyumbani Lubumbashi, katika dimba lao la Stade de Kenya na jambo la pili ni makosa ya kiuchezaji ya klabu ya Simba. Nafikiri Patrick Phiri ameona walipoteleza.

TP Mazembe haikushinda kwa sababu ilikuwa timu bora dimbani la hasha, bali ilishinda kwa sababu ilitumia makosa ya kiuchezaji ya klabu ya Simba. Kwa upande wa Simba nafasi ya
kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji ilibaki mno nyuma wakati viungo wa TP Mazembe walipokaribia eneo la 18, hivyo Juma Kaseja alizibwa kwa mabao mawili ya awali.

Hili lilikuwa kosa kwa klabu ya Simba kuwaachia TP Mazembe hatua tano au 10 kukaribia eneo la 18. Bao la kwanza lililofungwa na Patou Kabangu watakubaliana nami halikuwa na kitisho wala kusema TP Mazembe ni tishio, kwa sababu ni kosa la kiuchezaji na goli halikutokana
na ufundi wowote.

Hilo tusiivimbishe kichwa TP Mazembe. Bao la pili lilipatikana kutokana na kasumba ileile ya
wachezaji kuwafundisha vibaya juu ya sheria ya kuotea(matokeo yake tunamlaumu Oden Mbaga).

Kabla Narlise Ekanga hajapachika bao alipata pasi murua kutoka upande wa kulia, ambako wachezaji wa Simba walikwishaanza kuashiria kwamba mchezaji aliyetoa pasi kwa mfungaji alikuwa ameotea (lilikuwa kosa hilo hutakiwi kumwamini mwamuzi kwa mechi ile).

Katika jukumu la msingi la kushinda mechi unapaswa kuhakikisha kila jambo linalindwa na
wachezaji wenyewe hivyo hakuna suala la kumwachia mwamuzi, linaweza kuigharimu timu.
Wakati bao la tatu la TP Mazembe lilipotinga wavuni, bado nililazimika kucheka kwa sababu Simba ilikuwepo mchezoni lakini kilichowaangusha ni umakini na makosa madogo madogo tu.

Kicheko changu kilisababishwa na namna uchezaji wa TP Mazembe usioshawishi na kuiweka imani yangu kuwa kikosi chao hakina ubora wowote kama Raja Casablanca, Al Ahly, Asec Mimosas, Enyimba au Esparence na Club African ya miaka kumi iliyopita.

Yaani hata Mamelodi Sundowns iliyotikisa miaka ya 1990. TP Mazembe wanashinda kutokana
na udhaifu na makosa ya wapinzani wake, na zaidi kwa sasa kikosi hicho kimechoka hakiwezi
kutetea ubingwa wake tena. Kazi kwenu Simba.

Ukiangalia mchezo huo unakupa taswira kwamba uwezo wa TP Mazembe si wa kutisha isipokuwa wamekuwa wakitumia sana mbinu za kujenga mazingira ya kuwatisha wapinzani wao.

TP Mazembe ilikuwa bora msimu uliopita, lakini sasa haina ubora wowote, huo ndiyo ukweli
hivyo Simba wakishindwa kuichapa mabao 3-0 jijini Dar es Salaam wajilaumu wenyewe.
Kwanini? Simba ina hazina watu wawili wanaoweza kukaa na mpira; Emmanuel Okwi na Patrick Ochan.

Pia Simba inayo hazina kubwa ya kiungo mkabaji ngangari Abdulhalim Humoud au hata akipangwa Jerry Santo si mbaya. Lakini Abdulhalim alihitajika sana katika pambano lao na TP Mazembe pale Lubumbashi.

Sababu; unapoweka timu yako inatumie muda mwingi kukaba na kupunguza uwanja kwa lengo la kuwadhibiti wapinzani, basi unatakiwa kufanya mambo mawili. Mosi, kusuka beki na pili kusuka nafasi ya kiungo.

Nyongeza inakuwa ni kusuka nafasi ya ushambuliaji kwa kuwa na mshambuliaji mmoja tu anayejua kazi ya kupambana na mabeki wa timu pinzani. Kama hilo halitoshi basi unatakiwa
kuifanya timu yako icheze kama gurudumu, yaani inazunguka (total football) kila kona na wachezaji wanabadilishana nafasi ndani ya dimba.

Kwa hiyo Simba iliweza kucheza kutoka nafasi ya ulinzi hadi kiungo lakini ikashindwa kumudu nafasi ya ushambuliaji. Si vibaya.

Laiti Simba wangelikuwa makini tangu kipindi cha kwanza basi wangeliweza kupata bao au mabao mapema sana katika dakika 45 za kipindi cha kwanza. Lakini kutokana na mpango wa kujilinda ilikuwa vigumu kwa dakika hizo kuweza kupata mabao.

Mechi zote za TP Mazembe mara nyingi inatayarisha ushindi mwanzoni mwa kipindi cha kwanza na mwishoni mwa kipindi cha pili. Hili lilijitokeza katika pambano lao la fainali ya klabu bingwa dhidi ya Esparence mwaka jana.

Labda tuseme kidogo tatizo la Simba; klabu hii inakabiliwa na uhaba wa mshambuliaji namba moja. Ali Ahmed ‘Shiboli’ anaonekana kumudu nafasi hii lakini anahitaji mechi nyingi ili aweze kupambana na kupata uzoefu, pia makocha wake wamwongezee utundu zaidi.

Ni kweli msimu huu Simba inacheza vema na inaongoza ligi lakini hakuna mshambuliaji kamili.
Hata hivyo, mchezo wa marudiano ndio msingi maana hatuna haja ya kuangalia nyuma.
Nilishauri katika makala moja kuwa ili kuidhibiti TP Mazembe unatakiwa kuhakikisha pasi zote zinazotoka upande wa kushoto na katikati ya dimba zinadhibitiwa.

Kwa sababu pasi hizo huwa zinamfikia Given Singuluma ambaye ni mchezaji hatari. Hata hivyo
kocha wa TP Mazembe, Lamine Ndiaye aliiogopa sana Simba, ilishangaza kuwapanga viungo wengi huku Given Singuluma akimweka benchi.

Hilo lilikuwa jibu kuwa Simba inaogopwa lakini wakichezea kamari hii vibaya kazi kwao. TP
Mazembe walianza na viungo Reinford Kalaba, Patou Kabangu na Bedi Mpenza.

Ndugu zangu tuulizane swali, unafikiri TP Mazembe watakuja na mbinu gani? itajibu hivi; TP Mazembe walimweka benchi Given Singuluma kwa sababu ya kuongeza uimara wa nafasi ya kiungo ili kulinda lango lao.

Na mechi ya marudiano watampanga tangu mwanzo wakiazimia kushambulia muda wote wa
mchezo ili kupata bao mapema. Kwa kuwa wanafahamu kuwa Simba inaweza kupata mabao 2-0 na kuipokonya ubingwa wake Afrika kwa hiyo lazima waje kucheza nguvu-kazi.

Kwa Simba, bado tunalo tatizo la stamina. Patrick Ochan amekamilika kwa hili. Mbwana Samatta anapaswa kujifua kuimarisha stamina. Sina shaka na Musa Mgosi.

Sasa mechi hii hapa Simba wafanye nini? Patick Phiri anatakiwa kuisuka sana safu ya kiungo kucheza mitindo yote miwili; ‘zonal marking’ na ‘man to man’ kwa sababu Given Singuluma anacheza sana katika nafasi (akabwe kwa ‘zonal marking’).

Simba watazame mchezo wa marudiano baina ya TP Mazembe na JS Kablie ya Algeria kwenye hatua ya makundi msimu uliopita, pambano lililofanyika pale Algiers waone timu hiyo ikiwa ugenini inafanyaje.

Lilikuwa pambano kali. Endapo viungo wa Simba watafanikiwa kuwa na nidhamu ya mchezo ikiwa wataagizwa kucheza mitindo hiyo basi nafasi ya Bedi Mpenza na chipukizi Reiford Kalaba
kuichachafya ngome ya Simba ni adimu.

Mabeki wa pembeni wanatakiwa kucheza kwa kasi muda wote wa mchezo. Simba hawatakiwi
kushindana ubavu na TP Mazembe bali wanaweza kucheza katika nafasi ili kuruhusu aina yao ya soka kupata ushindi.

Ndugu zangu, tuseme ukweli, Juma Kaseja, Emmanuel Okwi na Patrick Ochan wanao ufunguo wa ushindi wa Simba hivyo kocha Patrick Phiri ahakikishe timu inakuwa na nidhamu ya mchezo.

Wala wasihangaike kulazimisha mfumo utafanyaje kazi, bali waangalie wachezaji wataufanyiaje kazi mfumo uliopo. Simba ikishindwa kuing’oa TP Mazembe wajilaumu wenyewe
kwani kushinda mchezo hakutokani na TP Mazembe kushiriki kombe la dunia ngazi ya klabu.

*Mwandishi ni mchangiaji makala anapatikana kwa simu selula: +255 764 93 66 55.
 
*Mwandishi ni mchangiaji makala anapatikana kwa simu selula: +255 764 93 66
55.

Well said,kama mpo hapa wahusika fanyieni kazi ushauri huu wa bure
 
Back
Top Bottom