Simanjiro: Walimu walalamikia kunyimwa kushiriki kwenye zoezi la sensa

FRANK MICHAEL

Senior Member
May 17, 2011
151
46
kumekuwa na malalamiko ya walimu wa shule mbali mbali walio zungumza kwa masharti ya kutotajwa kutohusishwa na zoezi la sensa, ikiwa ni adhabu ya kushiriki kwenye mgomo wa walimu, nini tfsiri ya vitendo hv?
 
Hii ni uthibitisho kwamba hii ni Serikali DHAIFU ambayo inatenda kazi zake kwa kuwakomoa wananchi wake ambao hawakubaliani na Serikali katika maamuzi mengi. Walimu wanaweza kushinda mchezo huu wa "kukomoana" kwa walimu wote nchini kugomea kushiriki katika sensa hii.

kumekuwa na malalamiko ya walimu wa shule mbali mbali walio zungumza kwa masharti ya kutotajwa kutohusishwa na zoezi la sensa, ikiwa ni adhabu ya kushiriki kwenye mgomo wa walimu, nini tfsiri ya vitendo hv?
 
Panueni fikra zenu kiuchumi walimu! Ili mfike mahali pakuacha kutunga nyimbo za kusifu tu! Funguka ticha.
 
Kulilia kudharauliwa utu wako ni hatari kwa haki zako we mwl. Unayelilia sensa.
 
Ni sahih kiongozi'hawa walalamikao ni wale wale walimu ambao hawakugoma na kusimamia sensa wamepotezewa so cku nyingine acheni kujipendekeza'mlidhani usaliti wenu ungewapa First Priority' Jifunzeni'mbona si wengine tumechili tu?
 
Hivi walimu wasipo enda sensa hawawezi kufanya mambo mengine? Hivi ni kweli kwamba ilitakiwa walimu wote walioomba wa sensa ilikuwa ni lazima wapatiwe? Maoni yangu: hizi favour ndio zinafanya serikali iwadharau maana inajua jinsi ya kuwagawa tena kirahisi sana.
 
Maisha ya mwalimu yanaweza kusonga mbele bila kushiriki katika zoezi la kuhesabu watu. Sensa hufanyika kila baada ya miaka kumi, kwa kipindi hicho walimu wanaishije? Walimu wasiendekeze njaa. Kama hawajateuliwa si basi jamani kwani lazima?
 
kumekuwa na malalamiko ya walimu wa shule mbali mbali walio zungumza kwa masharti ya kutotajwa kutohusishwa na zoezi la sensa, ikiwa ni adhabu ya kushiriki kwenye mgomo wa walimu, nini tfsiri ya vitendo hv?
Nakubali mna madai ya msingi lakini hamkuwa imara kwenye mgomo!niijuavyo serikali hii kwa kweli mateso mtayapata kwa sababu tu ya unyonge mliooneshaSasa kivumbi kinawajia, Hamkuwa na msimamoanyway Upo Simanjiro ipi wewe Loswaki, Ork au Namalulu?
 
Huku ni kudhalilishana, ndio maana mimi hata sikuomba hiyo kazi, ni upuuzi mtupu, mtu na elimu yako, hata kama ni ngazi ya certificate, unakuwa mtumwa wa shilingi lakii tatu? Ndiyo maana kwenye mgomo wengine mlitusaliti ili tu mpate sensa? Ushenzi sana huu na kwa mtindo huu walimu wengi mtakufa maskini kwa kusubiri vijisenti vya uchaguzi na sensa. Mi niko zangu shamba napiga work kama kawa. Kalaga bhao....!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom