Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...

Asante Lizzy.
umeongea kama mama yangu alivyoongea,
nilijaribu sana kumshawishi kuwa ni bahati mbaya lakini haamini.

Aisee ni vigumu sana kuamini kama ni bahati mbaya.Maana angekuwa hakukusudia basi asingekuumiza kwa kiasi kikubwa,angalau angekukwangua juu juu tu kutokana na nguvu kutumika kidogo.Mimi nilishashuhudia mtu ameng'atwa **** mpaka damu kuchuruzika na mgonjwa wa HIV hivi hivi.Pole sana,Mungu amekuepusha!
 
FirstLady1 somo thread yake vizuri, yeye kapima mara moja tu :biggrin1:
fazaa sasa hicho kidude chenye kucheka kinamaanisha kuwa umefurahia sababu nimepima mara moja hivyo ninaweza kuwa nina ukimwi au kinamaanisha unafurahia nini mkuu?
Jf wanyanyapa ni wengi sana!sijaona comment yoyote inaotia moyo wa athrika wa ukimwi nyienyie ndio wataalam wa jukwaa la MMU.takwimwi za mzumbe last year kati ya madent 3000 na ushee wanafunzi zaid ya 200 wameshapigwa danger.

Makubwa haya!!
Hivi tunajua maana ya kunyanyapaa au tunasema tu.
Mi nijuavyo kama unamnyanyapaa mtu wala huwezi kukaa naye mkala chakula alichopika na kuandaa yeye achilia mbali kulala naye room moja.
 
Last edited by a moderator:
kwa iyo wale ambao tumepima tukakutwa tumeathirika Mungu hatupendi na sio mwema kwetu..si ndio!!
in this life jaribu kujifunza kwamba kila kitu kinatokeakwa sababu ambazo wewe au mimi hatuzifahamu.......hakuna mtu asiependa uhai wake;wewe ulienusurika kuambukizwa haimaanishi ndio mwisho wa kutoambukizwa.........utaishi utasahu na litatokea lingine tofauti na hilo n aukajikuta upo positive......mshukuru Mungu kwa kila jambo.
watu wenye upeo na uelewa wa mambo kama wewe hatutegemei kuanza stigma na kujiona ndio bora kuliko hao walio positive....
ujumbe wangu:
hata walioathirika walikua Negative kama wewe!

hongera kwa kua negative...hata ukikutwa positive miaka 6 ijayo....umshukuru Mungu pia.. na maisha yaendelee!!

Mkuu wangu funguo kwanza kabisa kama kweli umeathirika nashukuru maana unajua kuwa kuwa kuwa na HIV sio mwisho wa maisha,na hiyo ni spirit nzuri na Mungu azidi kukupigania,sikupi pole maana nitakua kama nakuvunja moyo na kukufanya ujisikie vibaya.

Ila mkuu nimejifunza kuwa hapa JF mtu akiamua kupinga chochote ulichoandika hatakosa cha kukosoa na kukupinga,kama wewe,hapo kati unaniambia TUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO,kule juu nimemshukuru Mungu kwa kuniepusha na balaa kwa kusema Mungu ni mwema kwangu umekasirika,sasa hata ningeandikaje nadhani ungekosoa tu maana humu kuna watu wao wako makini kutafuta kitu cha kukosoa tu.

Hapo pa zambarau ndio yale yale ninayosema wewe lengo lako lilikua kunikosoa tu,faida unazozipata kwa kufanya hivyo unazijua mwenyewe,anayejiona bora angeacha kitanda cha hoteli akalale chini?Anayejiona bora kwa kuwa yuko negative angeenda kulala na kula nyumbani kwa mtu anayejua kabisa kuwa ni muathirika?Hapa naona umenihukumu.

Mwisho wa yote nakutakia kila la kheri na pia Mungu ni mwema kwako pia,angekuwa si mwema kwako sidhani kama leo hii ungekua na nguvu za kuperuzi pamoja nasi hapa JF.Ubarikiwe.
 
Last edited by a moderator:
]

Ukimwi & cancer.........haya magonjwa yanatisha jamani!!

BTW; hofu ni mbaya jamani, unaweza jikuta unaugua kitu ambacho hata hukukitegemea
Pole queenkami!

Ukiwa na hofu mwili wote unakupa dalili kuwa mambo sio shwari.
vimagonjwa ambavyo hujawahi pata hata vitakapotokea hutapajua.
Mi nadhani hofu yenyewe ni ugonjwa,inaweza kukuua.
 
Duh! Pole kwa mateso na msongo wa mawazo!

mtoto umenisitua

Ukimwi & cancer.........haya magonjwa yanatisha jamani!!

BTW; hofu ni mbaya jamani, unaweza jikuta unaugua kitu ambacho hata hukukitegemea
Pole queenkami!

story yako na mimi imeshanikuta.mwanamme wangu wa kwanza,baada ya muda tukaachana.jamaa mwenyewe alikuwa hajatulia.baada ya kuachana,kuna mtu alimuona akaniambia amepungua,mimi moja kwa moja nikachukulia ameathirika,hata kumuona sikumuona.na mimi nikasema kimoyo moyo ninao,nikawa sina raha,na nikawa naumwa mara kwa mara kwa ile hofu tu.nikasema mbona sina bahati,mwanamme wangu wa kwanza katika maisha yangu amenipa huu ugonjwa.siku niliojikokota kwenda kupinda,niliharisha hatari.wakati nasubiri majibu,nilijua tayari majibu ni positive.sikuamini nilivyoambiwa ni negative,magonjwa yote yaliisha,it was 12 years ago.nchi niliyokuwepo nilifanya full medical check up again,kila kitu ok.ila somo nililopata i really respect mtu ambae ni hiv positive,stress za mwanzo mwanzo hizo wanazozipitia,mimi nimeshazipitia.na tatizo la huu ugonjwa,upate support maana kuna wengine wanakuhesabia kabisa miaka,na wanakuambia pole mbele yako,ila pembeni story huwa ni tofauti

Mi nakwambia nimeshajifunza kuwa hofu ni ugonjwa na wenyewe unaweza kutoa roho ya mtu.
Ndo maana watu tunasisitizwa kupima,bora mtu upime ujue kuwa sina au ninao kuliko leo unawaza labda sina kesho ukitokewa hata na kaupele unajua tayari hata kula huwezi.
Pia nimejifunza kuwa kumbe wengi tunaishi na ukimwi wa kuumba kichwani kumbe kihali halisi mt huna.
Pole kwa kuendesha siku ya kupima mi nilikua kama nusu mfu,nadhani ningeambiwa ninao ningefaint sababu saikolojia yangu haikuwa tayari kuyakubali majibu mabaya.
 
kwakweli nimepata funzo hapa.

Nafurahi kama umejifunza kitu kitakachokusaidia.
Mi pia hii expirience imenifundisha vitu vingi na hata mtazamo wangu juu ya maisha umebadilika juu ya mambo fulani fulani.
Ndo maana unaambiwa usimnyooshee mwezio kidole na wala usihukumu,mtu yeyote anaweza kupata huu ugonjwa.
 
Cantalisia una roho ya upendo sana.
Unawezaje kumfukuza mtu akiwa mgonjwa namna hiyo.
Unaambiwa mtenda wema hulipwa na Mungu na ndio maana pamoja na kuwa katika risk akakuepusha usiambukizwe.
Pole na wewe kupitia hali ya kujihisi,inatesa.
Nafurahi kusikia huyo mpendwa anaendelea vizuri.
Mama mkubwa wangu yeye bado anateseka kwa magonjwa nyemelezi sababu hataki hizo dawa.
Inaumiza kuona akiteseka wakati dawa zipo ila ndo huwezi kumlazimisha.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana queenkami hofu inaweza kukubadili na kusababisha kifo. Mpe pole ma'mkubwa kumbuka anahitaji sana faraja yako.
 
Last edited by a moderator:
Aisee ni vigumu sana kuamini kama ni bahati mbaya.Maana angekuwa hakukusudia basi asingekuumiza kwa kiasi kikubwa,angalau angekukwangua juu juu tu kutokana na nguvu kutumika kidogo.Mimi nilishashuhudia mtu ameng'atwa **** mpaka damu kuchuruzika na mgonjwa wa HIV hivi hivi.Pole sana,Mungu amekuepusha!
ktk hali hiyo kuna uwezekano wa kutoambukizwa.
 
Aisee ni vigumu sana kuamini kama ni bahati mbaya.Maana angekuwa hakukusudia basi asingekuumiza kwa kiasi kikubwa,angalau angekukwangua juu juu tu kutokana na nguvu kutumika kidogo.Mimi nilishashuhudia mtu ameng'atwa **** mpaka damu kuchuruzika na mgonjwa wa HIV hivi hivi.Pole sana,Mungu amekuepusha!

Asante ni kweli nimenusurika kwa msaada wa Mungu wetu wa huruma.
Kwa kweli hayo namuachia yeye na Mungu wake mwaya,
kama alikusudia kuniambukiza kwa makusudi au la mimi sitaki kuchuma dhambi kwa kukisia,
mradi nimenusurika acha niendelee kuamini kuwa ni bahati mbaya japo mama yangu anasisitiza nikae mbali naye.
Mungu pekee ndiye anayejua ukweli Lizy 11
 
Last edited by a moderator:
queenkami nimefurahi sababu umetoka mzima, si unajua navyo kupenda.

kweli nimeamini zipo aina nyingi za kuonesha kuwa unampenda mtu mkuu fazaa.
Yaani umesisitiza nipime mara tatu ikiwa unamaanisha kuwa kipimo cha kwanza kinaweza kuwa kimekosea.
Mi ulivyocheka mwenzio nilidhani unanikejeli kumbe unaonesha jinsi unavyonipenda LOL.
Halafu mi nilidhani kudhani mtu anaweza kuwa kawa kaathirika ni jambo la huzuni kumbe wengine lina wachekesha.
Napenda kukuhakikishia kuwa queenkami is HIV NEGATIVE.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo umekuja kujisifu kwamba wewe ni salama zaidi na kufanya unyanyapaa kwa mama yako, utakufa wewe na mama yako utamuacha........!!!
 
kweli nimeamini zipo aina nyingi za kuonesha kuwa unampenda mtu mkuu fazaa.
Yaani umesisitiza nipime mara tatu ikiwa unamaanisha kuwa kipimo cha kwanza kinaweza kuwa kimekosea.
Mi ulivyocheka mwenzio nilidhani unanikejeli kumbe unaonesha jinsi unavyonipenda LOL.
Halafu mi nilidhani kudhani mtu anaweza kuwa kawa kaathirika ni jambo la huzuni kumbe wengine lina wachekesha.
Napenda kukuhakikishia kuwa queenkami is HIV NEGATIVE.
quuenkami Sasa ulitaka mimi nilie sababu umetoka mzima? Afu kumbe nikicheka unakasirika, basi wacha kuanzia leo nikiwa najibu thread zako niwe nalia :A S cry:
 
@ mtoa mada kuna kitu kinaitwa "PEP", Unakifahamu?

Ndio mkuu Ninaweza ninakifahamu.
It stands for Post Exposure Prophylaxis(hope sijakosea spellings).
Ni matibabu ambayo mtu anaweza kuyapata masaa ishirini na nne baada ya kujihisi ameambukizwa na yasizidi masaa 72 ambayo ni sawa na siku tatu.
Dawa wanazotumia hapa ni anti-HIV drugs ila mkuu PEP sio guarantee ya kutopata UKIMWI.
Unaweza fanya PEP ambayo ni kutumia hizo dawa kwa kama wiki nne hivi na bado vijidudu vikangangania mwilini.
Hata hivyo naomba niseme ukweli,kipindi kile sikua najua kuwa kuna hii kitu,nilijua kirusi kikiingia kimeingia hakuna wakukitoa.
 
Last edited by a moderator:
quuenkami Sasa ulitaka mimi nilie sababu umetoka mzima? Afu kumbe nikicheka unakasirika, basi wacha kuanzia leo nikiwa najibu thread zako niwe nalia :A S cry:
fazaa kila jambo lina mahala pake.
kuna yanayochekesha na kuna yanayoliza sasa kama siku nitaweka thread kuwa naolewa au nimeshinda bingo bilioni kadhaa halafu ukalia nitakushangaa kwa mara ngingine tena LOL.
Cha msingi fuata ratiba,ikiwa ratiba inahusu jambo la huzuni waungwana huonesha huzuni atakayeonesha furaha jamii humshangaa japo sometimes ni ruksa kuwa tofauti na sio kufuata mkumbo tu.
Ratiba ikiwa inahusu jambo la kufurahisha ukilia jamii itakuona mwanga au mwenye wivu japo kuna machozi ya furaha ila yanajulikana.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu funguo kwanza kabisa kama kweli umeathirika nashukuru maana unajua kuwa kuwa kuwa na HIV sio mwisho wa maisha,na hiyo ni spirit nzuri na Mungu azidi kukupigania,sikupi pole maana nitakua kama nakuvunja moyo na kukufanya ujisikie vibaya.

Ila mkuu nimejifunza kuwa hapa JF mtu akiamua kupinga chochote ulichoandika hatakosa cha kukosoa na kukupinga,kama wewe,hapo kati unaniambia TUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO,kule juu nimemshukuru Mungu kwa kuniepusha na balaa kwa kusema Mungu ni mwema kwangu umekasirika,sasa hata ningeandikaje nadhani ungekosoa tu maana humu kuna watu wao wako makini kutafuta kitu cha kukosoa tu.

Hapo pa zambarau ndio yale yale ninayosema wewe lengo lako lilikua kunikosoa tu,faida unazozipata kwa kufanya hivyo unazijua mwenyewe,anayejiona bora angeacha kitanda cha hoteli akalale chini?Anayejiona bora kwa kuwa yuko negative angeenda kulala na kula nyumbani kwa mtu anayejua kabisa kuwa ni muathirika?Hapa naona umenihukumu.

Mwisho wa yote nakutakia kila la kheri na pia Mungu ni mwema kwako pia,angekuwa si mwema kwako sidhani kama leo hii ungekua na nguvu za kuperuzi pamoja nasi hapa JF.Ubarikiwe.

Jinsi ulivyowasilisha ujumbe wako ni dhahiri kwamba wewe unajiona ni bora kuliko wale walioadhirika, mbona JF siku hizi sio MA-GREAT THINKER, mtu anawasilisha upumbavu kama huu na wengine wakawa wana-support. Naomba utambue wewe unayejiita queenkami wanadamu kabla hajafa hajaumbika na uelewe kwamba kuna magonjwa yanayowatesa wanadamu zaidi ya hiyo hali ya UKIMWI ambayo wewe ndio unaona kwamba ni tishio na wakati kuna watu wanaishi miaka na miaka na maisha yanaenda, wewe uliumwa mafua tu na ukaanza kufa kihoro. Kamuulize SAJUKI, atakueleza kwamba kuna magonjwa yanatesa wanadamu zaidi ya hivyo ujuavyo. Nakusikitikia kwamba una hatari ya kupoteza maisha mapema zaidi kwani utakufa kwa ugonjwa wa KIHORO, yaani kitu kidogo tu kitakusumbua na hofu iliyotawala maisha yako ndio itakayokumaliza. Unahitaji kubadili mtazamo........!!!!???? else...............?????
 
fazaa kila jambo lina mahala pake.
kuna yanayochekesha na kuna yanayoliza sasa kama siku nitaweka thread kuwa naolewa au nimeshinda bingo bilioni kadhaa halafu ukalia nitakushangaa kwa mara ngingine tena LOL.
Cha msingi fuata ratiba,ikiwa ratiba inahusu jambo la huzuni waungwana huonesha huzuni atakayeonesha furaha jamii humshangaa japo sometimes ni ruksa kuwa tofauti na sio kufuata mkumbo tu.
Ratiba ikiwa inahusu jambo la kufurahisha ukilia jamii itakuona mwanga au mwenye wivu japo kuna machozi ya furaha ila yanajulikana.
queenkami niko na wewe, maneno yako ni shule kabisa :poa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom