Sikutamka kufutwa Chadema - Tendwa

DOOKY

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
370
50
Tendwa katika mkutano wake wa juzi wakati akiongea na waandishi wa habari alisema, hakutamka kufutwa kwa Chadema bali alisema wanahabari waliandika vibaya(story iliandikwa katika gazeti la Mwananchi), kuwa amesema Chadema.

Hata hivyo taarifa za ndani za Mwananchi zilisema ni kweli hakusema hivyo na anashangaa mwandishi mwenzake kuandika hivyo.

My take waandishi wanaweza kukuza mambo ambayo yatahatarisha amani ya nchi.
 
Kwa nini akatoa kauli ya kufutwa kwa chama cha siasa mara tu mauaji ya Daudi Mwangosi yalipotokea?

Wakatiwa uchaguzi mdogo Igunda nako kulitokea mauaji, kwanini Tendwa hakutoa kauli za kufuta chama/vyama vya siasa? Au kwa sababu CCM walikuwepo kwenye eneo la tukio?

Ninachoweza kusema ni kuwa Tendwa (as a person) hana credibility tena ya kuendelea kukalia kiti cha msajili wa vyama vya siasa. Hana. Kauli zenye utata na zinaashiria biasness zimekuwa zinaongezeka siku hadi siku ni wazi kabisa sasa ameamua kusimama upande mmoja na sio katikati. The best thing he ca, kwa manufaa ya nchi is, to step down and do politics as he pleases. Vinginevyo atabakia kuwa msajili wa CCM.
 
Wakati anatoa kauli ya kufuta 'chama cha siasa' alikuwa anazungumzia nini vile??!!
Nafikiri mwandishi alitumia implication zaidi siyo maneno yaliyotamkwa.
 
nilimsikia kwenye kipima joto ITV anasema 'wakati mwingine inabidi ukumbushe...' so, infact anadai alikuwa anatishia, hakuwa serious anataka 'wakumbuke...wafuate sheria'...
anadai yeye ni 'mlezi' wa vyama vya siasa..na kama 'mlezi' ni lazima kumkumbusha 'mtoto' kwamba anakoelekea siko.
 
Hivi ajira yake au uteuzi wake hauna mwisho??naona kama watafute mtu mwingine sasa imetosha apumzike!!au anataka kuondolewa kwa aibu?kama kula amekula vya kutosha!!apumzike sasa!!Tanzania/ofisi ya msajili wa vyama itaenda tu hata kama Tendwa asipokuwepo!
 
Tendwa, ni kweli kusoma hatujui, lakini hata kuangalia picha nako kunatushinda jamani! Mpaka ubanwe na CDM ndo uje na kauli ya kukanusha! Kibri yako yote sasa mfukoni.
 
Hana jipya huyo mzee hata kama amekuwa misquoted bado hayo yalikuwa moyoni mwake!!!!
 
(1) Msajili wa vyama anayeteuliwa na Mwenyekiti wa chama kimoja hawezi kusimama katikati.

(2) Tendwa analaumu CDM wakati polisi wanapoua raia wanaotumia uhuru wao kuhudhuria mikutano ya amani ya CDM. Huu ni uhuni.

(3) Mkakati wa CCM wa kutumia watu kama Tendwa na Bana kudhibiti CDM naona unashindikana. Wametingisha kiberiti wakakuta kimejaa.

(4) CDM does not exist at the pleasure of Tendwa. Yeye ni Msajili (Registrar) na sio Mlezi (Patron) wa vyama. CDM should never take orders from Tendwa.
 
Back
Top Bottom