"Sikushinikizwa kumpeleka mwanangu uwanjani"- Baba mzazi wa Ismail

HELLO JF ,THESE ARE SOME OF INDICATORS THAT WE MUST BE RESPONSIBLE TO TAKE ACTIONS TO RESCUE OUR NATION DIGNITY!

Polisi wamtelekeza mtoto waliyempiga risasi Send to a friend Saturday, 15 January 2011 08:58 0diggsdigg

Editha Majura
POLISI wanatuhumiwa kumtelekeza mtoto Juma Hamza (12) waliyempiga risasi na hivi sasa hali ya mtoto huyo ni mbaya kiasi cha kumlazimu kutolea haja kubwa katika kidonda kilichotokana na jeraha la risasi hiyo.Baada ya kupigwa risasi, utumbo ulitoka nje na sasa sehemu ya utumbo uliokatika ndio unaotumika kutoa haja kubwa nje.
Tuhuma hizo zimekuja wakati polisi wakigubikwa na tuhuma nyingine za kufanya mauaji kwa kutumia risasi za moto dhidi ya raia katika mikoa ya Arusha na Mbeya.Januari 5, mwaka huu polisi waliwaua kwa risasi watu watatu wakati wakizuia maandamano ya wafuasi wa Chadema mkoani Arusha na juzi walimuua mkazi wa kata ya Ubaruku, Mbarali mkoani Mbeya baada ya kutokea mabishano baina yao na wananchi.

Lakini Mwananchi limebaini kuwa Juma ambaye ni mwananfunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Makole mkoani Dodoma, alipigwa risasi usiku wa kuamkia Oktoba 24, mwaka jana katika tukio ambalo hadi sasa limezua utata kutokana na polisi kutoa maelezo yanayokanganya.
Tukio hilo lilitokea eneo la Keko Molemo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika tukio ambalo polisi wanadai kwamba walikuwa wakisaka watuhumiwa wa unyanganyi, karibu na ukumbi unaojulikana kama Jumba la Dhahabu.
Wakati polisi wakitoa madai hayo, wananchi wanapinga nao wakidai kwamba eneo hilo hakuna ukumbi wenye jina hilo lililotajwa na polisi na kwamba waliokamatwa katika msako huo walivamiwa kisha kumatwa na wakiwa wamelala kwenye nyumba zao.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa tangu Oktoba mwaka jana hadi sasa mtoto Juma hajapata matibabu ya kuridhisha yanayoweza kufanya kupona jeraha lililotokana na kupigwa risasi, zaidi ya kuwekewa mpira kwenye kidonda ambao anautumia kutolea haja kubwa.

Mpira huo ambao gharama yake ni Sh 5,000 hubadilishwa kila siku, na gharama hizo ni mbali na gharama nyingine za tiba ambazo familia ya mtoto huyo inalazimika kuzibeba ili kumwezesha kuendelea kuishi.
Babu wa mtoto huyo, Khamis Lulange alisema mjukuu wake alilazwa kwenye wodi ya Kibasila namba 11 baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia utumbo wake kutolewa nje kwa risasi na kwamba aliporejewa na fahamu, akamudu kuzungumza hivyo aliruhusiwa ili awe anapelekwa kuchunguzwa kadri anavyoendela.
Lulange alisema muda mfupi baadaye afya yake ilianza kuzorota hivyo kulazwa katika kituo cha afya cha polisi kilichopo Mgulani, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kwa ahadi kwamba polisi wangempa huduma za tiba na mahitaji mengine.Kwa mujibu wa Lulange, mtoto huyo alilazimika kurejeshwa nyumbani ambako anaugulia hadi sasa kutokana na kukosekana kwa chakula katika kituo hicho cha afya cha Polisi.

Alisema tangu wakati huo afya yake imeendelea kudhoofu kutokana na kunyimwa huduma za afya na kwamba hata walipokweda Muhimbili wamekosa huduma hizo kwa madai kwamba faili lake halionekani. “Novemba 23, mwaka jana jina lake liliitwa wakatuelekeza chumba cha kumpeleka, walihudumiwa wagonjwa wote isipokuwa sisi tukaambiwa faili halijapelekwa pale, mmoja wao akasema, “mwandikieni tarehe nyingine huyo.”
Tukaambiwa turudi Disemba 31,” alieleza Lulange.Lulange alisema hata walipompeleka tena Desemba 31, alikosa tiba kwa maelezo kwamba faili lake halionekani hivyo kupangiwa kwenda tena Februali 2 mwaka huu.
“Hofu yetu kubwa ni kwamba hatufahamu hatma ya afya ya mtoto wetu, kwa sababu mpaka sasa anatumia mfuko kutolea uchafu (haja kubwa) tumboni,” alisema Lulange.Alisema kinachowashangaza ni ukimya wa polisi wa kutotekeleza ahadi yao ya kumuhudumia, hivyo kuiacha familia ikibeba mzigo wa tatizo hilo peke yao.
Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, alipohojiwa na Mwananchi kuhusu lilipo faili la mtoto huyo alisema, hawezi kuzungumzia suala hilo ila atafuatilia kumbukumbu zinazohusu mgonjwa huyo na kutoa ufafanuzi mapema iwezekanavyo.
Maelezo ya mtoto JumaNaye mtoto Juma akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao Keko, alielezea kusikitishwa kweke na kubadilishiwa mfumo wa maisha kwa kupewa ulemavu na kumfanya ahisi kwamba atashindwa kutekeleza ndoto zake za kuwa rais au mrusha ndege (Rubani).
Juma katika shule yake ya Makole anadaiwa kwamba alikuwa akifanya vizuri darasani kwa kushika nafasi ya kwanza mpaka ya tatu, lakini tangu akumbwe na mkasa huo hajawahi kurejea darasani.Alisema askari aliyempiga risasi, akimuona anaweza kumtambua na kwamba hajamsamehe kwa sababu hajawahi kumuomba radhi.

“Natamani sana kusoma kwani naamini ndiyo njia pekee ya kunikomboa kimaisha lakini sifahamu kama naweza kutokana na maumivu makali ninayoyapata kwenye kidonda,” alisema Juma na kuongeza:“Ninaumia sana ninapomuona mdogo wangu akienda shule... naumia lakini nitafanyaje maana sijui kama naweza kukaa muda mrefu kwasababu ya maumivu ni makali.
.”.Ilikuwaje akapigwa risasi ? Akizungumzia tukio hilo, mjumbe wa nyumba kumi shina Namba 33, Shaban Mashua, alisema Oktoba 23, 2010 kulikuwa na sherehe za uzinduzi wa kikundi cha kusaidiana cha kinamama kiitwacho Wanadafana, zilizopata kibali kutoka kwa ofisi za serikali ya mtaa huo.Alisema kibali hicho kiliruhusu sherehe hizo kuanzia saa 10:00 jioni mpaka saa 2:00 usiku Oktoba 24, 2010. Alisema watu walijumuika nyumbani kwa baba wa mtoto huyo aitwaye Hamza Juma.
Alisema majira ya saa 9:00 usiku, akiwa miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, waliyokuwa mbele ya nyumba hiyo wakisherehekea kwa kucheza muziki, alifuatwa na mke wa Hamza akimueleza kuwa mume wake (Hamza Juma) amekamatwa na Polisi kutoka chumbani mwao walimokuwa wamelala na kufungwa pingu.
Alisema alipofika kwenye ukumbi wa nyumba hiyo, alikuta polisi hao wakiwa wamevunja mlango wa chumba kingine na kumfunga pingu mpangaji mwingine, Mohammed Mpile. Alisema alijitambulisha na kuhoji sababu ya watu hao kukamatwa na kwamba badala ya kujibiwa, askari hao walianza kuwasukuma waliofungwa kuwatoa nje ya nyumba.
Wanafamilia hizo mbili, ndugu na majirani waliamua kufuata askari wakiongozwa na Mashua pamoja na kibali cha kufanya sherehe hiyo, kwa imani kwamba ndugu zao walikamatwa kutokana na sherehe hiyo.
Tofauti na matarajio, Mashua alisema walipofika kwenye kituo cha mafuta cha Oil Com, askari waliamuru wananchi hao wasisogelee gari walimowekwa ndugu zao ama wangepigwa risasi.Alisema katika kamatakamata hiyo, polisi waliwatia mbaroni Abdallah Abdullahman Bakari ambaye ni mgonjwa wa akili, Khadija Issa Bakari (mke wa Mpile), Chiku Abdullahman Bakari aliyekuwa mjamzito na Msafiri mtoto Mohammed Idd mwenye mwaka mmoja na miezi tisa.

Alisema hakuna aliyezuia askari kufanya kazi yao bali yeye ndiye aliyeomba maelezo ya kilichojiri, tena baada ya kujitambulisha kwao lakini badala yake askari mmoja alipiga risasi hewani, watu wakaanza kukimbia ovyo kisha askari mwingine akawa anawalenga na kuwashambulia kwa risasi, moja ikampata mtoto Juma.
Alisema hata baada ya kumuokota mtoto huyo akiwa hajitambui, utumbo ukiwa nje na kumpeleka kwenye gari la askari hao lililokuwa limeegeshwa kwenye kituo cha mafuta cha Oil Com kusudi wamkimbize hospitali, askari hao walikataa kutoa msaada badala yake waliingia kwenye gari kisha kuondoka.
Alisema walisaidiwa na gari jingine la polisi lililokuwa likifanya doria na kwamba wakati wakiendelea kumuhudumia ili apelekwe hospitali, askari waliyojeruhi walifika kituo cha polisi cha Chang’ombe na askari waliotoa msaada wakawaamuru waendelee kumuhudumia kwa sababu ndio waliyosababisha hayo.
Mgonjwa walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alianza kupatiwa matibabu.
Alisema wote waliokamatwa waliwekwa rumande Chang’ombe bila kuelezwa kosa lao na kwamba kesho yake, mlezi wa familia ya Hamza, Lulanje alitakiwa kuwasilisha kitambulisho chake cha kazi ili awadhamini wote waliyowekwa ndani kwa madai kwamba wanatuhumiwa kwa unyang’anyi.
Maelezo ya polisi Oktoba 26, 2010 Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidiz wa Polisi David Misime, alikaririwa na vyombo vya habari akisema mmoja wa polisi wa kituo cha Chang’ombe alimjeruhi kwa risasi Juma Hamza wakati wakijihami wasipigwe mawe na wananchi.
Alieleza kuwa awali Polisi walipokea taarifa kuwa mtu mmoja (hakutajwa jina) aliporwa kamera kwenye makutano ya barabara ya Chang’ombe na Mandela, baada ya kutishwa kwa panga na vijana wawili.
Alisema polisi saba wakiwa ndani ya gari walifanya msako na kuwakamata watuhumiwa wanne akiwemo mwanamke mmoja (hawakutajwa majina).
Misime alikaririwa akisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa karibu na ukumbi wa Jumba la Dhahabu na kwamba wananchi waliyokuwa ndani ya ukumbi huo walitoka nje na kuwashambulia kwa mawe askari ili wasiwakamate watuhumiwa hao. Alisema hakuna askari aliyekamatwa kwa kwa kumpiga risasi Juma, kwama maelezo kwamba lilikuwa ni tukio la bahati mbaya
 
Mzee wa Ismail ni Jasiri! Mfano mzuri wa Mtanzania wa sasa! Huwezi kumwekea maneno mdomoni.

Nakubaliana nawewe mkuu, lakini kwa kuwa ameiumbua serikali, na vinyamkera wote waliokuwa wakiongea kishabiki, nina wasiwasi RPC Arusha anaweza kutangaza kuwa amepata taarifa za KIINTELIJENSIA kuwa baba wa Ismail si raia wa TZ. Haaha haa haa!
 
tunaambiwa usalama wa taifa walifuata familia zote wakawatisha na kuwakataza wasithubutu kupeleka marehemu wao uwanjani. badala yake wawazike kimyakimya ili kuuficha uhalisia wa mambo. tunashukuru familia zote mbili walielewa dhamira ya serikali kwamba ni kuuficha ukweli na kukata agizo la serikali.

Lakini mkuu, huoni familia imejiweka matatani, coz serikali itaanza kuifuatilia ili kulipiza kisasi kutokana na kukataa agizo la usalama wa taifa (ambao kwa sasa ni usalama wa Ccm) na pili familia kiumbua serijali.
 
Angalau redio one pamoja na kuwa ni mali ya mwana CCM ktk hili wameamua kusimamia kwenye haki.

Naunga mkono hoja ya kumsaidia huyu Mzee ushauri wa kisheria.
Na aambiwe kuna faida ya kuchukua hatua za kisheria kwamba mbali na kuwafedhehesha watawala kuna ziada kama akishinda madai yake atalipwa fidia na hao waliochapa hiyo habari ya kizushi
 
Unajua tusishabikie mambo bila kujua kwa sheria za kiislam hairuhusiwi mtu kuagwa, Pia maiti ikifa izikwe haraka, haya ndo mambo ya kuzingatia ila kwa nyie cdm mnaona ushindi kwa wanafamilia wamemtesa maiti wao na wamepata Laana kwa Mungu maana asipozikwa musilam kwa mafundisho MwenyeziMungu hushusha laana kwa waislam wa mji wote. Ndo maana kina sheikh shaabani kuogopa hilo walimfuata mzee naye alikataa kuogopa chadema kwa maneno yake
 
Source: Habari Leo

Habari Leo limejishushia heshima mbele ya jamii, japo hata hivyo halikuwa na heshima yoyote kabla.
Kitendo cha kumlisha maneno baba mzazi wa Ismail kinadhihirisha kuwa hata hao wengine wanaodaiwa kuwa atributed nao walilishwa maneno. Habari hii ni ya kupikwa. Shame upon Daily News. Shame on their Editor. Shame on minister of Information. Shame upon Jk. Hawana adabu kabisa.
 
Unajua tusishabikie mambo bila kujua kwa sheria za kiislam hairuhusiwi mtu kuagwa, Pia maiti ikifa izikwe haraka, haya ndo mambo ya kuzingatia ila kwa nyie cdm mnaona ushindi kwa wanafamilia wamemtesa maiti wao na wamepata Laana kwa Mungu maana asipozikwa musilam kwa mafundisho MwenyeziMungu hushusha laana kwa waislam wa mji wote. Ndo maana kina sheikh shaabani kuogopa hilo walimfuata mzee naye alikataa kuogopa chadema kwa maneno yake

Dr Omar Juma (R.I.P) alikuwa dini gani maana nae aliagwa.

Ingefaa pia azikwe bila uchunguzi?? Kama ni laana kutoka kwa mwenyezi Mungu mbona watanzania tunafanya mengi yenye kustahili laana hata bila ya kumtesa maiti.

Maswala ya dini magumu sana jamani esp hizi dini tulizoletewa (ukristo na uislam)
 
Upotoshaji wa vyombo vya habari umekuwa jambo la kawaida. Hakuna anayelikemea. Hiyo tume/kamisheni inayosimamia tasnia ya habari imekaa kimya kama Raisi na Viongozi wengine wanavokaa kimya. Habari Leo, Uhuru, Mzalendo, Daily News, Tanzania Daima, Mwanahalisi n.k kuna upande yanaegemea! Ukinunua unatarajia habari itakayokuwa imeandikwa inamuelekeo fulani! Waandishi wa habari wanaandika ili mradi kuwafurahisha wamiliki kwa kupotosha ukweli au uchochezi! Hii hali sio ya kuachwa iendelee!

Naunga mkono hoja!
 
mi nadhani hoja ya msingi hapa iwe hali halisi ilivyokuwa pale arusha, wakati mwingine hata sheria zinaweza kuwekwa kando kidogo ili kuweza kutumia busara na some kind of situational reasoning. ndo maana hata unaweza kuskia".......mahakama kwa kutumia busara yake, imeonelea........"

case ya ismail, tusifungwe sana kuitizama kwa upande wa hitaji la kidini wakuu, it was a special case that, in my opinion, was supposed to be accorded a special treatment. It was wise for the family of Ismail (or whoever) to display their dissatisfication by doing an act that will make the whole public to sense their agony. Na hata hivyo, yote yale yalikuwa maumivu ya kila mpenda mageuzi, regardless dini wala imani yake. Tusijifunge sana wakuu na mambo ya Imani, MUNGU WETU NI WA HURUMA SANA, HUTUCHUKULIA MADHAIFU YETU YOTE NDUGU ZANGU.

REST IN PEACE ISMAIL & OTHERS
 
Kwa kuwa tunalijua hili, basi nawaombeni tuwe waangalifu sana tunapoongelea masuala ya dini zetu. Tendo/kauli moja la musilam lisiwe ni sababu ya kuonekana ndivyo waislam wote walivyo, halikadhalika tendo/kauli moja la wakristo lisichukuliwe kama ndiyo tendo la wakristo wote.

Katika jitihada zetu hizi za kuutaka ukweli, haki, demokrasia na maendeleo, mbinu mbalimbali za wasiotaka mabadiliko zitatumika, ikiwemo udini, ukabila, n.k. Sisis tuzishinde hizo zote kwa kuzidi kushikamana zaidi. Kukitokea muislam au waislam wenye kuulaani ukristo au wakristo, kabla ya wakristo hawajahamaki na kuingia kwenye mtego wa kuanzisha mijadala ya udini, watazameni wale waislam walio wengi mnaoishi nao, mnaofanya nao kazi, wali ndugu zenu, marafiki, wake, watoto, wapenzi wenu, n.k., na muone kama kweli kauli hiyo inawawakilisha hao, kama si hivyo ipuuzeni. Halikadhalika kwa waislam nao wafanye hivyo hivyo.

Hatuwezi kufanikiwa kuleta mabadiliko ya nchi hii bila ya kushikamana katika kuyatafuta.

You are so intelligent brother. Hongera. Nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa.
 
Unajua tusishabikie mambo bila kujua kwa sheria za kiislam hairuhusiwi mtu kuagwa, Pia maiti ikifa izikwe haraka, haya ndo mambo ya kuzingatia ila kwa nyie cdm mnaona ushindi kwa wanafamilia wamemtesa maiti wao na wamepata Laana kwa Mungu maana asipozikwa musilam kwa mafundisho MwenyeziMungu hushusha laana kwa waislam wa mji wote. Ndo maana kina sheikh shaabani kuogopa hilo walimfuata mzee naye alikataa kuogopa chadema kwa maneno yake

Acha mawazo mgando wa ajenti wa Ccm. Jadili hoja ktk wide perspective acha kufungwa na udini. Hoja iliyoko mezani ni mzazi wa Ismail kupinga taarifa za uzushi zilizotolewa na vibaraka wa ccm. Sasa hiyo ya kwako, sijui muislam akikaa siku mbili bila kuzikwa familia inapata laana inahusikaje na hoja ya msingi?

Acha utapiamlo wa fikra wewe. Jadili taarifa iliyotolewa na mzazi wa Ismail, hayo mengine sijui kuzikwa kwa kuchelewa that's another business, na ofcourse inawahusu waislamu zaidi.
 
Naomba cdm wanunue muda kwenye main stream waonyeshe mkanda wa maandamano ili dunia ione uhalisia cio ile propaganda ya polisi eti cdm walitaka kuvamia kituo bila silaha

Wazo lako zuri sana!!! LAKINI kwa mapenzi ya vizazi vijavyo wasifanye hayo maana nakuhakikishia nchi nzima itarindima kwa maandamano na fujo. Kibaya zaidi kinachoweza kujitokeza ni kwamba walio wanachama wa CCM watashambuliwa na kuchomwa matairi kama wanavyochomwa VIBAKA Sugu!!!!!!!1
JE, UNATAKA HALI HIYO???!!!!!!!!!!!
Ninashauri haya kwa kuwa hali halisi ilotokea Arusha tuloenda shule tunaifahamu hata bila kuonyeshwa mkanda. We know it from listening all parties [police, ccm, chadema and news]
CCM NI CHAMA KINACHOAMINI TANZANIA NI MALI YAKE BINAFSI/PEKEE WENGINE HAWANA HAKI. KWA HIYO NI SUALA LA KUWAELIMISHA HATUA KWA HATUA HUKU WAKIBANWA MAENEO HATARISHI WANAYOJARIBU KUYAPANDIKIZA ILI BAADAYE WANAPOONDOKA IONEKANE WAO NDO WALIKUWA VIONGOZI WAZURI KWANI WANAJUA SIKU ZAO ZINAHESABIKA NDO SABABU WANAANZA KUVUGA NCHI KWA MAMBO YA UDINI, DARAJA ZA WENYE NACHO NA WASIO NACHO, N.K
 
ndo maana wewe huna mwongozo wakristo hamjaelekezwa namna ya kuzika ndo maana mnatumia Common sense huwezi kutumia common sense kwenye mambo ambayo yako define tayari.
Common sense yako ya Mtoa kamasi itafika wapi?
 
ndo maana wewe huna mwongozo wakristo hamjaelekezwa namna ya kuzika ndo maana mnatumia Common sense huwezi kutumia common sense kwenye mambo ambayo yako define tayari.
Common sense yako ya Mtoa kamasi itafika wapi?

Pumba hivi! Elewa mjadala usiweke wehu hapa
 
Kuna watu hapa walikuwa wanaongea hadi povu mdomoni kwa kujifanya kuijua dini kuliko mashehe walioswalisha tukawaambia watakuja kuwa wapole siku si nyingi sasa bado polisi nao watasema tu.

Mkuu nilipoweka red naomba ufafanuzi kidogo ili kuni prove wrong kua nalowaza silo ulilomaanisha!
 
BabieWana,
Mimi pia ni muislam mwenzako ila ndugu yangu kauli zako zimechongoka sana. Nadhani unatoka nje ya topic alaf zaid unakuwa na jazba kuliko busara mkuu. Wote sisi ni ndugu moja, tumeoleana, tunaishi pamoja, tunafanya kazi pamoja na mengine mengi..

Iweje mwenzetu wewe unatoa kauli tata hivi??? Kaa kwenye hoja ya msingi mkuu. Haya mengine ni yako binafsi
 
Back
Top Bottom