Alfu Lela Ulela
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,255
- 77
Baba mzazi wa kijana Ismail aliyepigwa risasi na kuuawa na polisi huko Arusha, katika mapambano kati ya Jeshi la polisi na wafuasi wa CHADEMA amesema kuwa hakukuwa na shinikizo lolote kupeleka mwili wa mwanae viwanja vya NMC kwa ajili ya ibada ya kumuaga.
Mzazi huyo amesema uamuzi wa kupeleka mwili huo viwanjani NMC ulikuwa ni uamuzi wa familia na hakukuwa na shinikizo lolote kutoka nje ya familia kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapo awali.
"Yalikuwa ni maamuzi ya familia kuwa mwili wa Ismail upelekwe viwanjani kuagwa na hakukuwa na shinikizo lolote kama inavyodaiwa." alisema mzazi huyo na kuongeza
"Tuliamua kufanya hivyo ili kuuonesha ulimwengu ukiukwaji haki uliyofanywa na jeshh la polisi"
Taarifa hii inakuja siku chacie baada ya kuenea uvumi kuwa wazazi wa Ismail walishinikizwa kupeleka mwili wa marehemu viwanja vya NMC kwa ajili ya ibada ya mazishi.
Uvumi huo ulizidi kupaizwa na vyombo vya habari, na kukihusisha chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusika kuishinikiza familia kuileta maiti ya Ismail uwanjani NMC.
Kwa maana hiyo taarifa ya mzazi wa Ismail inakisafisha chama cha CHADEMA kutokana na kupakaziwa na kuchafuliwa na taarifa za uvumi zilizotolewa awali.
Vilevile taarifa hii inaonesha wazi namna baadhi ya watu wenye nia mbaya wanavyopika habari na kuzivumisha, huku wakichafua wengine kwa alili ya maslahi yao wenyewe.
Pongezi kwa mzazi wa Ismail aliyeamua kueleza ukweli. Pongezi CHADEMA kwa kuruka kiunzi cha kutaka kuchafuliwa kwenye kazi njema mliyoianza.
SOURCE:Radio One.