Sikubaliani na Pinda kuhusu Dowans

Kauli ya waziri mkuu Pinda aliyoitoa jana kupitia Star Tv kwamba serikali itafuata msingi wa utawala wa sheria wa dhana ya utawala bora kuilipa dowans sikubaliani nayo. Kwanza nampinga Pinda kwa kuangalia utawala bora katika ngazi ya juu tu kuhusu kesi inayoamuliwa na taasisi ya kimataifa ya biashara kati ya Dowans na Tanesco. Pili nampinga Pinda kwa mtazamo wake kuwa anayetarajiwa kulipa ufisadi wa Dowans siyo serikali bali ni sisi wananchi- raia wa Tanzania. Tatu, Pinda anakwepa ukweli kwamba rushwa si mojawapo ya misingi ya utawala bora.

Pinda amepotoka kwa sababu haiwezekani auone utawala wa sheria katika taasisi ya kimataifa inayoamua kesi wakati huohuo anakwepa ukweli kwamba kimsingi mkataba kati ya Dowans na Tanesco au wananchi wa Tanzania si halali kisheria- ni wa kifisadi. Dowans ilirithishwa mkataba feki na kampuni hewa ya Richmond. Utawala bora wa sheria unatoka wapi katika hali hii? Pinda pia anatundanganya watanzania eti serikali ndiyo inayotarajiwa kulipa ufisadi wa Dowans hali akijua pesa za serikali zinakamuliwa kutoka kwetu wananchi, hatutaki ufisadi huu. Mwisho, Pinda hawezi kuzungumzia utawala bora katika mkataba anaojua fika kuwa ni wa rushwa. Rushwa ni kipimo cha kukosekana kwa utawala bora. Lowasa, Msabaha na karamagi walijiuzuru baada ya bunge kubaini rushwa ilitumika katika kuipa Richmond kazi ya kuzalisha umeme. Pinda anajua kuwa Richmond haipo katika mafaili ya kampuni zilizowahi kusajiliwa na Brela hapa Tanzania. Uhalali wa kisheria na utawala bora katika mkataba wa Dowans unatoka wapi mzee Pinda?

Pinda asitufanya wananchi hatuelewi. Anataka kuhalalisha ufisadi wa Dowans na kutubebesha wananchi madeni ya kifisadi kwa manufaa ya kuwalinda mafisadi wa serikali ya CCM katika mkataba wa Richmond na Dowans. CCM ikihalalisha mzigo huu kwa wananchi itaendelea kukabiliana na hasira kali za wananchi, wananchi tumechoka kunyonywa na kunyanyaswa na CCM.

Kila ninaposikia kauli na kuona matendo ya watawala wa nchi hii naona kama vile wamechoka kutawala na kuongoza nchi hii. Watoa kauli na kufanya matendo yanayo wachochea watu kukaa na kufikiria kuwasaidia.Kweli kiongozi unayeongoza serikali ambayo hata kutoa huduma za kuridhisha kwa wananchi wake ni taabu, lazima uchanganye na misaada ndio mambo yaende japo kwa shida, waweza kutoa kauli kama hizi. Tusubiri tutaona mwisho wa hii mienendo tata.
 
jamani mnataka wamSamweli Sitta...?jamani ombeni na msali tu miaka mitano iishe haraka hatuna kiongozi...petroli elfu mbili....
 
Sijawahi kusikia hili la utawala bora wa kulipa deni la kampuni ambayo iliingia nchini kwa kuidanganya Serikali. Tukumbuke kwamba kampuni hii ilidanganya kwamba HQ yake iko Houston, Texas na ina utalaamu katika kufua umeme. Hii haikuwa kweli bali ilikuwa ni kamuuni ya ndani kifisadi ya ndani ya briefcase na haikuwa na utaalamu wowote ule katika kufua umeme.

Pamoja na kampuni hii kupewa mkataba ule wakati nchi ikiwa imegubikwa kwenye giza la kutisha haikuweza kufua hata tone moja la umeme kwa visingizio mbali mbali.

Sasa iweje kampuni ya kitapeli/kifisadi ambayo iliidangaya Serikali leo hii ivune shilingi 185 billioni na Waziri Mkuu ambaye anatakiwa asimame kuhakikisha pesa za walipa kodi haziguswi hata senti moja leo atoe kauli eti kwa kufuata utawala bora basi Serikali itawalipa Richmond/Dowans pesa ambazo hazistahili.

Utawala bora huu kama unafuatwa mbona wale Wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki bado wanazungushwa kwa zaidi ya miaka 30 katika kudai haki ya mafao yao toka EAC? Utawala bora kama kweli upo kwanini Serikali haitaki kuwalipa Wafanyakazi kima cha chini ambacho kimeombwa na Jumuiya ya Wafanyakazi kinachoendana na hali halisi ya ghrama za maisha? Au huu utawala bora unakuwa na umuhimu pale tu ambapo mafisadi kama Rostam wanapohusika ndiyo Serikali inaona umuhimu wa utawala bora? Hakuna utawala bora wowote kwa kuilipa kampuni iliyoingia nchini kifisadi na kupata mkataba kifisadi huu ni wizi wa mchana kweupe.

Pinda acha usanii! Tetea maslahi ya Watanzania badala ya kutetea maslahi ya Mafisadi. Hukupewa uPM ili kutetea maslahi ya mafisadi bali kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.

Pinda anayejiita mtoto wa mkulima anawezaje kuwaza na kutaka kuwatendea kinyume watanzania wa kawaida anaodai kuwawakilisha? Kwa nini mtoto wa mkulima Pinda uruhusu mwendelezo wa unyonyaji wa mafisadi wa CCM kwa maskini raia wa Tanzania?
 
This is what i can say;

A number of YOU Voted for KLEPTOMANIACS, Don't ever complain for what You are now getting!!!! :embarrassed::embarrassed::embarrassed::embarrassed:
 
Sidhani kama huyu PM yuko makini ama na misingi ya kazi yake au na mustakabali wake kisiasa. Sina neno zuri la kiswahili lakini, kwa kifupi, he is simply mediocre and out of touch with reality. He's not smart. Labda ndio maana wajanja wanamtuma kutoa hadharani kauli kama hiyo ya kuilipa Dowans. Wao wanajua kisiasa ni kauli mzigo! Katika nyakati hizi, ni mjinga tu au mwanasiasa asiyejijali ndiye anayeweza kujitokeza mbele kutoa kauli hiyo huku akiwa macho makavu. And worse still, it is doubtful if at all he is among the beneficiaries of the payment! Labda ndiyo gharama ya kupewa u-PM inayomlazimu awe tayari kubeba taka zote za mafisadi! A nice person? Probably yes; but they've made him an empty and useless PM!
 
Back
Top Bottom