Sikuamini kama ni yeye………!

Pole rafiki, ndo maisha!

Mtambuzi asante kwa hiki kisa cha opereta, kina mafunzo mengi ndani yake, funzo kubwa wazazi tuwe na tabia ya kutenga muda na kukaa na watoto wetu.

Lakini mtambuzi, wewe hupata wapi hivi visa?

Nimehisi uchungu sana hasa kwa mimi ambae sijalelewa na mama yangu mzazi!
 
Mkuu, kumbe ulipopigwa ndoa ya mkeka Ulikuwa umemuacha mama Marry Tabora. I hope ulimwambia yaliyokusibu ukiwa kama Dj MT. :)
 
Pole rafiki, ndo maisha!

Mtambuzi asante kwa hiki kisa cha opereta, kina mafunzo mengi ndani yake, funzo kubwa wazazi tuwe na tabia ya kutenga muda na kukaa na watoto wetu.

Lakini mtambuzi, wewe hupata wapi hivi visa?
ramn mie huwa nasimuliwa tu na ndio naweka hapa.................
Hata wewe kama una kisa chako nisimulie nami nitakiandika kwa umahiri na kukiweka hapa.
Hivi visa ni marejeo ya visa tulivyokuwa tunaviandika katika gazeti la Jitambue kabla halijafa
 
Last edited by a moderator:
sijui Ni kwanini navutiwa na simulizi za mtambuzi? nilikuwa nasinzia lakini baada tu ya kuona jina lake kwenye hii thread usingizi ukapaa! simulizi zako zina mafunzo mengi
 
duh nasoma huku nikitafakari sana juu ya hiki kisa, watoto wanahitaji malezi ya ukaribu sana kwa wazazi wote.
 
Mfalme Mtambuzi

Nikija Tanzania ntakutafuta. There are 8 types of intelligence. Wewe ni genius when it comes to linguistic intelligence. Ungeishi katika nchi sahihi na wakati sahihi ungekuwa milionea wa kutupa (kama George Lucas wa Lucas film)

Wewe ni moja kati ya rasilimali za taifa (national treasure).
 
Kwangu ni mwiko kuiruka thread ya Mtambuzi,nazidi kuelimika kupitia kwako.Big up bro!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
very touchy, emotional and educative,

on a serious note, mkuu Mtambuzi kwanini usiendeleze kipaji chako cha utunzi/uandishi kwa kuandika vitabu na kuuza? Soko ni kubwa na nina uhakika watu wanakosa waandishi wazuri
 
nakumbuka nilikuwa mpenzi sana wa gazeti la Jitambue, lilikuwa na ukurasa wa visa kama hivi unavyoleta jamvini mara kwa mara, nakumbuka pia katika baadhi ya visa ulivyowahi kutoa hapa vilishawahi kutoka katika gazeti la Jitambue. Kipindi hicho nilikuwa mwanafunzi na sikuweza kuwa napata kila nakala ya Jitambue...Kuna uhusiano wowote kati ya visa unavyotoa humu jamvini kuwa ni marudio ya visa vilivyowahi toka katika gazeti la Jitambue? Tueleze tu ukweli....
 
Back
Top Bottom