siku ya mlaji duniani

Mar 9, 2010
9
0
March 15 ni maadhimisho ya siku ya mlaji duniani. Nami kama Mtanzania ni mara yangu ya kwanza kusikia maadhimisho ya siku hii katika taifa letu. Nakiri kuwa sijapata nafasi ya kutosha kujua nini maana ya siku hii na ni jinsi gani mimi kama mlaji nalindwa dhidi ya bidhaa na huduma ambazo nanunua kila siku madukani na katika taasisi mbalimbali.

Ni mara nyingi nemenunua bidhaa nikakuta ziko chini ya kiwango na hata huduma nyingine . Mfanojuzijuzi nimenunua mkoba dukani kwa bei kubwa na baada ya siku 2 mkono ukaanza kukatika. Jana nilipeleka gari yangu kwa fundi akatengeneza chini ya kiwango cha makubalianao yetu. Nilijikuta napishana nae lugha kwa sababu alishachukua fedha na nisingeweza tena kumlipa fundi mwingine amalizie kazi kwa kiwango kile tulichokubaliana

Naomba kama kuna mtaalamu wa elimu hii ya haki za mlaji anifahamishe haki za mlaji na wajibu wangu pale haki yangu inapodhulumiwa ikizingatiwa kuwa mambo mengi hapa Tanzania yanafanyika kienyeji sana kutokana na elimu ndogo ya watumiaji wa bidhaa. Kila wakati tunasissitizwa kuchukua risiti ukifanya malipo lakini hata kama huduma ni mbovu na risiti unayo sijawahi kuona watoa huduma wakiwajibishwa kwani hata mamlaka zinazohusika hazieleweki kwa wengi wetu.

Nisaidieni tafadhli wataalamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom