siku ya majonzi

=FREDOMFIGHTER;Mkubwa una kihere here kama mbunge wa Same Mashariki, mbona tarehe 26 FEBRUARI bado?

hii inaonyesha wewe unaishi somalia ndio maana unayakumbuka ya trh 26 feb
 
Kwani leo ni tarehe 26?


kwa tarehe hiyo 26 labda mabomu somalia ,hapa kwetu ilikuwa 16 tujalibu kuweka kumbukumbu sawa, sio unaandikaa tu kila kitu kipo kwenye mtandao ungejushughulisha kidogo tu ungejua ilikuwa tareha ngapi
 
Inafadhaisha sana, Lol, nashukuru Mungu sikuwapo Dar es salaam siku hiyo, maana mabomu ya Mbagala yalinikuta Msikitini naswali

430793_188678904571576_100002884020414_273573_173849656_n.jpg
 
Nami yalinikuta yanayokaribia kufanana na mtoa mada, nilikuwa ughaibuni na wakati huo nilikuwa ndio kwanza tunaingia hotelini toka kuzurula na wenzangu ndipo kijana wangu akanitumia msg kuwa wanakimbia kuna mabomu g/mboto. Wakati ananitumia msg huku bongo ilikuwa saa 6 usiku, maana nilipokuwa ilikuwa saa 4.
Wakati ananitumia msg alikuwa na nduguye mmoja tu, wengine hajui wameelekea upande gani yaani wamepotezana. Ikanibidi nianze kazi ya kuwatafuta wengine kwa msg maana ilikuwa hawezekani kwa simu mawasiliano hayakuwa mazuri, nawasiliana na hawa na kuwaambia wenzeo wako wapi halafu narudi kwa hawa mpaka waliposema kumetulia ilikuwa saa 6 saa za ughaibuni. Yaani we acha tu, kuchanganyikiwa si kuchanganyikiwa, kuendesha si kuendesha ili mradi ilikuwa tafrani ya namna yake.
Poleni sana mlioathirika kwa namna moja au nyingine na kasheshe lile.
 
Back
Top Bottom