Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya kwanza jijini Dar

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by katawa, Oct 7, 2012.

 1. k

  katawa Senior Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 103
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ilikuwa ni tar 17-12 1988 nilpopata taarifa kuwa siku tatu baadaye nitasafiri kuelekea 'dizim' Dar es salaam.Maandalizi ya nguvu yakaanza ikiwa ni pamoja na kuazima nguo bila kusahau chupi.Rafiki yangu mpendwa Asuvisye akaniazima chupi aina ya vipi.
  Siku ikawadia mimi na kiongozi wangu wa msafara tukapanda basi la Zainabu.Njian nilikuwa kero kwa abiria kwa kuwa nilishangaa mambo mengi na nilikuwa nauliza maswali bila kikomo ukizingatia ni mara ya kwanza kupanda basi ktk umri huo wa miaka kumi na nne.

  Siku inayofuata tukafika dar mchana.Tulipofika magomen kiongozi wangu akanitwisha kiroba cha mchele yeye mbele mimi nyuma,akajitokeza muungwana kunisaidia nikampa kiroba mwenyeji wangu akiwa mbele yangu.Alipofika nyumbani kugeuka anaona sina kipeto aliponiuliza kiko wapi nageuka nyuma sikumuona muungwana aliyenipokea.

  siku ya pili ilikuwa ijumaa ktk tembea yangu nikapita eneo ambalo watu wengi waliovaa nguo nyeupe na kofia walikuwa wanaingia na kutoka ilikuwa majira ya jioni.nikapata shauku ya kujua kuna nini huko ndani,nikaingia nikiwa nimevaa raba aina ya DH.Kumbe ni msikiti nimeingia na viatu na watu walikuwa kwenye swala kilichotokea unaweza ukakihisi.

  Siku nyingine nikapelekwa feri na watoto wenzangu.Nilipoulizwa iwapo najua kuogelea nikakubali ili nisionekane wakuja, nikajitosa kwenye maji kwa nguvu.Washukuriwe wavuvi waliokuwepo eneo lile.

  Ndani ya muda mfupi Dar niliyokuwa naiota na kuitamani ikanikifu nikamlazimisha mwenyeji wangu anirudishe kwetu Uyole Mbeya ambako utulivu ni kama Mbinguni.

  Je mwanajamii mwenzangu hebu nijulishe wewe ilikuwaje siku ya kwanza jijini DAR?
   
 2. AKILImuchknow

  AKILImuchknow JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 216
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio wote wakuletwa wengine ni borntown!
   
 3. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 7,555
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Sisi tumepata akili tukiwa Dar na bado tupo sana tu
   
Loading...