Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo

Kundi hilo linalopinga adhabu hiyo ndilo kundi linaloshirikiana na wauaji majambazi sugu ambao wizi na utekaji wa mali za wananchi wanaupata kwa kutekeleza mauaji.
Kundi hilo linalopinga ni kundi hatari sana hapa duniani (Mafia) limetapakaa dunia nzima na hilo wanalolitetea kwa muda huu ni azimio lao kuwa likipita watakuwa salama katika mikono ya serikali endapo watakamatwa.
Hukumu ya muuaji ni kuuliwa tu hakuna mbadala.Na kama wakifanikiwa kuifuta raia itabidi tufanye Upinda ,papo kwa papo.Akuna kufikishana polisi wala mahakamani. Hongera Pinda huna haja ya kutoa machozi wananchi walikuwa awajaona ulipopaona.


Nadhani ni hivyo Mkuu!
Sidhani kama unahitajika mjadala mrefu hapa!
Auaye kwa upanga atakufa kwa upanga!
 
Kundi hilo linalopinga adhabu hiyo ndilo kundi linaloshirikiana na wauaji majambazi sugu ambao wizi na utekaji wa mali za wananchi wanaupata kwa kutekeleza mauaji.
Kundi hilo linalopinga ni kundi hatari sana hapa duniani (Mafia) limetapakaa dunia nzima na hilo wanalolitetea kwa muda huu ni azimio lao kuwa likipita watakuwa salama katika mikono ya serikali endapo watakamatwa.
Hukumu ya muuaji ni kuuliwa tu hakuna mbadala.Na kama wakifanikiwa kuifuta raia itabidi tufanye Upinda ,papo kwa papo.Akuna kufikishana polisi wala mahakamani. Hongera Pinda huna haja ya kutoa machozi wananchi walikuwa awajaona ulipopaona.
.
Asante Mwiba, huu ndio uhuru wa kutoa maoni/mawazo yako, na kanuni za heshima, nayaheshimu mawazo yako.
 
Jamaa alitoa ushuhuda tumepanga vizuri tutaongea nae man to man, ile kumaliza tuu shughuli, jamaa simuoni tena, sijui kalala mbele!.
 
Nadhani ni hivyo Mkuu!
Sidhani kama unahitajika mjadala mrefu hapa!
Auaye kwa upanga atakufa kwa upanga!
Na hivyo ndivyo inavyosema sheria ya Musa kwenye Taurati/Kumbukumbu la Torati.
Ila Masiya naye alikuja kuikamilisha akisema, atakayekupiga shavu lako la kulia, mgeuzie na la kushoto, au asiye na dhambi ndia na awe wa kwanza kumtupia jiwe mwanamke mzinifu.
 
Mheshimiwa Pasco,

Nakubaliana nawe kwamba jawabu la kudumu ni kushughulikia chanzo cha watu kutaka viungo vya ma-albino, eti ili watajirike haraka. Lakini, kwa heshima na taadhima, uhamasishaji na elimu haviwezi kuondoa kwa haraka wimbi hili la aibu lililotukumba siku za karibuni ili ma-albino watulizane.

Ingawa pia nakubali kwamba hukumu ya kumnyonga mtu mpaka afe ni ukatili, naamini kwamba ufahamu kwamba adhabu ya mtu aliyeua mwenzake kwa maksudi, ni yeye pia kuuawa inakuwa ni deterent.

Katika mazingira ya ugumu wa maisha kama tuliyo nayo sasa hapa kwetu, ni vizuri tuwatishe watu walio desperate kwamba wakiuwa maksudi, nao pia watauawa. Ama sivyo, vibaka au majambazi wengi wakiambiwa adhabu ni kifungo cha maisha tu, wataingia mitaani na kuanza kuuwa wananchi wenye kipato. Unavyofahamu, vibaka wengi wanadiriki hata kusema eti Segerea wana hakika ya mlo wa siku, ambapo wakiwa Sinza ni kubabaisha tu. Wakifungwa kwa maisha si wataona ni uhondo?

Uhamasishaji na juhudi za dhati za kutuondolea umaskini na ujinga viendelee. Lakini tuendelee kuwa na Sheria inayotishia mtu kunyongwa mpaka afe, endapo atatoa maisha ya mwenzie kwa maksudi. Rais awe na discretion to commute a death sentence, kama ilivyo sasa. Isiwe ni lazima Rais atangaze kwamba muuaji amepata commutation ya death penalty na kupewa kifungo cha maisha. Uamuzi huu uwe ni siri yake na taifa.
 
Ukiuua kwa Makusudi mfano i.wauaji wa albino, majambazi (juzi tu waliua mfanyakazi mwezangu) hao wote hukumu ya o kifo..tusilee wajinga na watu ambao hawastahili kuishi
kama wewe hudhamini maisha ya ndugu yako au mtoto wake then ..sisi tukudhamini una nini!
 
Ukiuua kwa Makusudi mfano i.wauaji wa albino, majambazi (juzi tu waliua mfanyakazi mwezangu) hao wote hukumu ya o kifo..tusilee wajinga na watu ambao hawastahili kuishi
kama wewe hudhamini maisha ya ndugu yako au mtoto wake then ..sisi tukudhamini una nini!

Kundi hilo linalopinga adhabu hiyo ndilo kundi linaloshirikiana na wauaji majambazi sugu ambao wizi na utekaji wa mali za wananchi wanaupata kwa kutekeleza mauaji.
Kundi hilo linalopinga ni kundi hatari sana hapa duniani (Mafia) limetapakaa dunia nzima na hilo wanalolitetea kwa muda huu ni azimio lao kuwa likipita watakuwa salama katika mikono ya serikali endapo watakamatwa.
Hukumu ya muuaji ni kuuliwa tu hakuna mbadala.Na kama wakifanikiwa kuifuta raia itabidi tufanye Upinda ,papo kwa papo.Akuna kufikishana polisi wala mahakamani. Hongera Pinda huna haja ya kutoa machozi wananchi walikuwa awajaona ulipopaona.

maneno sawia kabisa.

Anaeua nae auwawe hakuna mjadala
 
Tunaweza kujua ni wangapi wamehukumiwa kifo kwa kutazama kumbukumbu za Mahakama Kuu. Lakini idadi ya walionyongwa mpaka kufa haijulikani, kwani ni Rais tu mwenyewe anatia saini, na haitangazwi kuwa ametia saini au ameamua mtuhumiwa akae kifungoni kwa maisha.
 
Salaam,

Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo.
Maadhimisho ya kitaifa yameandaliwa na Mtandao wa Mashirika ya Utetezi wa Haki za Binaadamu kwa nchi za Kusini mwa Afrika tawi la Tazania-SAHRINGON na yafanyika ndani ya ukumbi wa Saba Saba, Kilwa Rd.

Hii ndio ratiba yake

MARKING THE WORLD DAY AGAINST DEATH PENALTY IN TANZANIA


PROGRAMME, OCTOBER 10, 2009


Sabasaba International Trade Fair grounds, Ngorongoro hall, Dar es Salaam


07:00-Arrival and registration-Secretariat
08:30-Peaceful Match from Kituo cha Uhasibu to Viwanja vya Sabasaba-Participants
09:30-The Guest of Honour Welcomes Matchers-Hon. Chief Justice Barnabas Samatta (Retired)
09:45-Introductory remarks-Chairperson Board of Directors of SAHRiNGON Tanzania Chapter
09:55-Objective of the Day against Death Penalty-Executive Director - LHRC
10:05-Statement on Death Penalty in Tanzania-Hon. Chief Justice Barnabas Samatta (Retired)
10:25-Launching of NGO Report on the Implantations of the International Covenant on Civil and Political Rights in Tanzania & Concluding observations of the UN Human Rights Committee -Hon. Chief Justice Barnabas Samatta (Retired)
10:35-Testimony-William Mwaikambo Kaleba
10:45-Discussion and Sharing of Experience from Abolitionists-All
11:00 -Break
12:00-1st Presentation; Status of Implementations of International Instrument in Tanzania -Ms. Juliana Masabo
2nd Presentation; Challenges for Abolishing Death Penalty in Tanzania-Mr. Harold Sungusia
13:10-Discussion-All
13:40-Closing Remarks-National Coordinator SAHRiNGON Tanzania Chapter-Mrs. Martina M. Kabisama

NB. Pia nimepata statement ya EU Naiambatanisha

Uhai ni kitu kitakakatifu (SACRED). Na yeyote mwenye kuukatisha uhai wa binadamu bila ya haki (yaani aidha katika kulipiza murder, au kuondosha ufisadi katika ardhi) basi adhabu iliyo sawia kwake (halali, justifiable, balanced, fair na vyovyote utakavyo kuielezea ) is EXECUTION (kifo). Na hii lazima ifanywe na state, sio mtu binafsi, ijapokuwa wakati mwengine state inaweza kumpa mmoja wa waliohujumiwa ndugu yao nafasi na upanga/bunduki/button pressing, etc. kuitekeleza adhabu hii, ndio mchango wao kuondosha ufisadi ardhini na kusafisha kisasi.

And whoever takes his/her own out of arrogance, then he/she will find him/herself in the fire of hell, constantly and miserably commiting the same act again and again, forever and forever, the pain of it ever increasing, punishmanet on the punishment. Eeee Allah, zinusuru hatima zetu, na usiachie huzuni itufike ambayo hatuwezi kuihimili. Tunusuru waja wako.

Wanaopinga!!! Hebu fikiria mdogo, kaka,dada,mama, shangazi yako zeruzeru ameuliwa kwa kukatwa viungo. Binti yako au hata mvulana wako wa miaka 10 amelawitiwa au kuingiliwa na jibaba. Can you make sense of that??? Angalia hapa sikutaja makosa ambayo pamoja na kwamba vilevile nayo yanastahili kifo, lakini ambayo we can debate and differ, leave them aside for a moment. We are talking about pure murder and fasada. Mnanaopinga, mnaopinga, tafadhalini, hizo lobbying grants mnazozipata kutoka huko kwa hao ambao life means nothing unless with celebrity, wealth or power attached to it, give us a break, take the money and go.

Hakimu (judge) katika uadilifu hana makosa. Yaani akipatia sawa sawa hukumu yake anayoitoa kutokana na ushahidi uliokuwa presented mbele yake, na kwamba yes the accused commited the crime and hence sentenced the convicted accused according to the law, then to God Almightly, he is DOUBLEY rewarded. In the case that he honestly misses it in the similar honest process, he gets SINGLY rewarded. Honest judge never miss the reward. We are all human. Then, for a shaky are unconfidence judge, it seems to me that he/she may merely know his/her proffesionalism, and does not ethically understand the duties and responsibilities bestowed on him/her by the God Almighty.
 
email.gif
E-mail this to a friend
print.gif
Printable version
1211.jpg
Honourable Ponsiano Damiano Nyami [CCM]
Nkasi ConstituencySession NoPrincipal Question NoTo the Ministry ofSectorDate Asked1348HOME AFFAIRSSecurity31 October 2008 Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, wapo wafungwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa bado wanasubiri adhabu hiyo na hata wengine kubembeleza wanyongwe baada ya kukaa muda mrefu:-

(a) Je, ni wafungwa wangapi mpaka sasa bado wanasubiri kunyongwa?

(b) Je, wafungwa wa aina hiyo waliokaa kwa muda mrefu sana gerezani wamekaa miaka mingapi?

(c) Kwa mara ya mwisho hukumu ya kifo imetolewa lini na mtu wa mwisho kunyongwa alinyongwa mwaka gani?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #48 SESSION # 13
1356.jpg
Answer From Hon. Kagasheki, Ambassador Hamis Suedi
HOME AFFAIRSNAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napeda kujibu swali la Mheshimiwa Ponsiano Damiano Nyami, Mbunge wa Nkasi, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia tarehe 1 Oktoba, 2008 idadi ya wafungwa waliohukumiwa hukumu ya kifo ambao bado wanashikiliwa katika Magereza mbalimbali nchini ni 286. Kati ya hao, idadi ya wafungwa wanaume ni 277 na wafungwa wanawake ni 9.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, mfungwa wa kunyongwa aliyekaa gerezani kwa muda mrefu ni miaka 22 (tangu 1986).

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, amri ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa mara ya mwisho ilitolewa mwaka, 1994.
 
Habari za Kitaifa

Adhabu ya kifo ni 'msalaba' kwa majaji
Imeandikwa na Na Simon Nyalobi; Tarehe: 10th October 2009 @ 23:59 Imesomwa na watu: 249; Jumla ya maoni: 0





JAJI Mkuu mstaafu Barnabas Samatta amesema majaji nchini wamekuwa ‘wakilazimishwa' kutoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa mbalimbali na kushauri Serikali na Bunge kuipa Mahakama Kuu mamlaka itoe adhabu mbadala.

Wakati Jaji Samatta akitoa rai hiyo kuna taarifa kuwa Rais Jakaya Kikwete amebadilisha hukumu 400 za kifo kuwa za kifungo cha maisha.

Jaji huyo mstaafu alisema wakati mwingine jaji aliyetoa adhabu ya kifo kwa mshitakiwa na kamati maalumu inayomshauri Rais juu ya utekelezwaji wa adhabu za kifo zilizotolewa mahakamani, hupendekeza kwa Rais kuwa adhabu hiyo isitekelezwe na badala yake mshitakiwa apewe adhabu nyingine na mara nyingi ikiwa ni kifungo kirefu.

Samatta alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wanaharakati wa haki za binadamu katika maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani yaliyofanyika Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

"Kwa nini sheria imbebeshe jaji mzigo wa kutoa adhabu ya kifo wakati anaamini, na kila mpenda haki angeamini kuwa siyo haki kwa mshitakiwa, siyo haki kwa ndugu wa marehemu na siyo haki kwa jamii na kuwa nyufa iliyopo kati ya adhabu hiyo na uovu wa mshtakiwa haizibiki hata utaalamu wa juu ukitumika?" Alihoji Samatta.

Alisema pia washtakiwa wa kifo wamekuwa wakiteseka kisaikolojia wakati wakisubiri hatima yao katika kipindi cha kati siku ambayo jaji anatoa hukumu ya kifo na siku ambayo Rais anapunguza adhabu hiyo ya kifo.

Kwa mujibu wa Samtta dunia imekwishaanza safari ya kufuta adhabu ya kifo na kuisisitizia Serikali na Bunge, kama wanaona ugumu kushiriki katika safari hiyo katika kipindi kifupi kijacho, kwa nini wasianze kuipa Mahakama Kuu mamlaka hayo?

Akifafanua hoja yake hiyo, Samatta alitumia hoja za wanaotetea kufutwa kwa adhabu hiyo kwamba, kwa kuwa haki ya binadamu ya kuishi na kuzaliwa haitolewi na katiba, wafalme au watawala basi hakuna mwanadamu mwingine mwenye mamlaka ya kusitisha haki hiyo katika mazingira yoyote yale.

Alisema pia kuna hatari ya adhabu hiyo kutolewa kwa makusudi au kwa makosa kwa mtu ambaye hana kosa na kwamba ikitumika hivyo hakuna njia yoyote ya kumrudishia marehemu huyo maisha yake.

Katika kutetea hoja hiyo, alinukuu maneno ya mwandishi wa Kifaransa, Nicolas Chamfort aliyepata kusema katika hadithi, "asubuhi leo tumewahukumu watu watatu kunyongwa.

Wawili kati yao kwa kweli walistahili kupewa adhabu hiyo." Samatta pia alitoa mfano wa tukio aliloliita kuwa la kusikitisha lililotokea wiki iliyopita huko Uingereza ambapo mfungwa mmoja aliachiliwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 jela kwa kosa la mauaji ya kukusudia baada ya kugundulika kuwa hakuhusika kwa namna yoyote ile na mauaji hayo kwa kuwa marehemu aliuawa na mtu mwingine.

"Mtu huyo ana bahati sana kuwa adhabu ya kifo haitumiki huko Uingrereza kwa kosa la mauaji. Isingekuwa hivyo, huenda angekuwa marehemu zaidi ya miaka ishirini iliyopita," alisema Samatta.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za haki za Binadamu Kusini mwa Afrika (SAHRINGON), Dk Emmanuel Kandusi alisema adhabu ya kifo ni ya kulipa kisasi na kwamba si suluhisho la tatizo la mauaji duniani na kupendekeza elimu iongezwe zaidi kukomesha mauaji mbalimbali.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, Tanzania inakadiriwa kuwa na wafungwa 2,246 ambao wanasubiria utekelezaji wa hukumu ya kifo katika magereza mbalimbali nchini huku watu 232 tu wakiwa ndio walitekelezewa hukumu hiyo tangu 1961.
 
Hivi Tanzania ni watu wangapi waliokwisha hukumiwa kifo toka tupate Uhuru?
.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, Tanzania inakadiriwa kuwa na wafungwa 2,246 ambao wanasubiria utekelezaji wa hukumu ya kifo katika magereza mbalimbali nchini huku watu 232 tu wakiwa ndio walitekelezewa hukumu hiyo tangu 1961.

Na zilizowasilishwa bungeni Dodoma ni hizi

From Hon. Kagasheki, Ambassador Hamis Suedi
HOME AFFAIRSNAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napeda kujibu swali la Mheshimiwa Ponsiano Damiano Nyami, Mbunge wa Nkasi, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia tarehe 1 Oktoba, 2008 idadi ya wafungwa waliohukumiwa hukumu ya kifo ambao bado wanashikiliwa katika Magereza mbalimbali nchini ni 286. Kati ya hao, idadi ya wafungwa wanaume ni 277 na wafungwa wanawake ni 9.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, mfungwa wa kunyongwa aliyekaa gerezani kwa muda mrefu ni miaka 22 (tangu 1986).

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, amri ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa mara ya mwisho ilitolewa mwaka, 1994.

Jamaa ametoa ushuhuda ameshuhudia live kwa macho yake watu 35 wikinyongwa gereza la Isanga, Dodoma alikokaa kwa miaka 15, toka 1994, ametoka mwezi April 2009. Serikali inadai mwisho wa kunyonga ni 1994.
 
Tanzania sio mwanachama wa mkataba wa kimataifa, kuhakikisha adhabu ya kifo inondolewa kabisa.
Ni aibu kwa Tanzania, haijaridhia mkataba huu mapaka sasa. Kuna nchi 25 zikiongozwa na Marekani, China na nchi za kiarabu ambazo bado zinaua.

Ni heshima kwa Tanzania na aibu kwenu nyinyi na umoja wenu wa mataifa msiochambua na makosa gani na gani yana adhabu ya kifo na yepi yana adhabu nyenginezo. Nyinyi mnataka kuiondoa tu. Maisha ya wanaodhulumiwa nyinyi kwenu hayana uzito wowote.

Fikira za watu kama WaTZ wanaopinga ni shallow hata kiasi cha kutokuona na kuelewa makusudi ya hao wanaokuleteeni hii mivundo mengine. Hebu weka wazi "one single, one single" underlying reason ambayo mnaiona nyinyi kwamba kuwepo kwake kunaweza kunampelekea mtu kwa dhamira au ajali/bahati mbaya kumuua mwenziwe kutokana na uzeruzeru wake, ambapo baada ya murder kutokea, watu wakiichunguza wanaweza kuiona sababu ile, jinsi inavyoghafilisha na kumpelekea mhalifu yule kufanya mauaji yale? na kwa hivyo kufikia tamnati kwamba mhalifu yule hastahili adhabu ya kifo??? just one single reason. Kumbuka, there is no such a thing here as "temporary insanity" this is calculated and premeditated murder. tengenezeni sababu moja tu tuijadili.

Je nyinyi mumewahi ku-conduct any study na mkawa na ushahidi vinginevyo?, yaani kwamba adhabu ya kifo haina effect/tofauti yeyote katika kupunguza au kwamba inaleta kinyume chake na kuzidisha mauaji ya maalbino??? au basi tu mnadanganya watu kwa kutumia lugha za kitakwimu ambazo hata nyinyi hamna "evidence" othewise. "Ushahidi wenu nyinyi uko wapi? Sifikirii kama kuna maadili ku-conduct study kama hizi "experimentally". Na kutumia Extrapolation au post-hocking ya data za Marekani, Uingereza, na nchi zengine za kimagharibi na kupresent takwimu zao kama zetu ni kudanganya watu bwanaaaa. Hamuwezi ku-describe mazingira yao na yetu kuwa sawa, hata watu wao na wetu kuwa ni sawa, wao wendawazimu sisi tuna akili zetu timamu.

Hamjui kuchambua pumba na mpunga nyie???
 
Sudan Baada ya Jaji kutoa hukumu ya kifo, ndugu wa Marehemu hupewa nafasi ya kuamua kama Hukumu itekelezwe au Muuaji asamehewe. Hii ina mantiki kubwa sana kwa sababu wakati mwingine Muuaji huwa ameondoa Bread Winner and in the process waliobaki(Bread Eaters) nao wanaathirika vibaya pengine hata kufa kwa magonjwa, njaa au kukosa elimu. Madhara ya mtu kuawawa yanaenda mbali zaidi ya kumuathiri mtu mmoja.

Hao wanaopinga adhabu ya kifo sidhani kama hata mmoja wao aliwahi kuwa na ndugu aliyegeuka kuwa Murder Victim. Kama hawataki kuhukumiwa kunyongwa basi wasiue binadamu wenzao.

Hii habari ya kuwa watu wanaosubiri kunyongwa hubadilika na kuwa watu wema sana haingii akilini. Wanakuwa wema kwa vile wanakiona Kitanzi mbele yao na si vinginevyo.
 
Utekelezaji wa adhabu hii ni mauaji pia, hivyo huna sababu ya kutoa adhabu ya kifo kwa muuaji kwa kumuua sio adhabu bali ni kulipiza kisasi au kumkomoa, hamsaidii kitu muuaji, wala haiwasaidii waliofiliwa ndugu yao kwa sababu haiwarudishii uhai wa ndugu yao, sana sana ni kujiplease tuu, 'kamuua ndugu yetu, nae kauliwa'[/QUOTE]

Kulipiza kisasi ndio mahala pake ili na wengine wanaotarajia kuua wajue kuwa " Ukiua na wewe unanyongwa... period.
 
Adhabu ya kifo inafaa, msiwasikie hao wanao weka haki ya mhalifu mbele ya haki ya mtu alie athirika na uhalifu. Kitu muhimu ni sharia ifuate mkondo wake katika hukumu hizi.

Hawa hawa ndio wanashabikia ushoga , wanadhani wanayo yakubali wao ndio yawe sharia ya dunia !
 
Adhabu ya kifo sio kulipiza kisasi bali ni kuondoa mhalifu anae weza kuchukua maisha mtu mwingine mtii sharia na pia ni kuwa kizuizi ( deterent ) kwa wahalifu wengine wana fikiria kufanya unyama wao .
 
Back
Top Bottom