Siku ya kuikomboa Tanzania

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
466
125
Naamini kuwa siku ya kuikomboa Tanzania sio siku ile CCM itakapong'olewa madarakani, au siku ile CHADEMA watakaposhika dola bali siku ya kuikomboa Tanzania ni siku ile watanzania tutakapoanza kuwaza na kufikiri zaidi ya hawa viongozi wetu wa kisiasa, siku ile ambayo wanachadema watawaza na kutafakari zaidi ya Mbowe, Dr Slaa, Lissu, Lema, Zitto n.k na pale wana ccm watakapowaza zaidi ya Dr Kikwete,Lowasa, Nape, Mukama n.k.

siku ambayo wote tutawaza kama binadamu na sio kama watu, siku tutakayowaza kama watanzania wenye uwezo wa kuwaza wenyewe bila msaada wa mtu yeyote.

siku ambayo tutakubali kuyakubali mawazo yote mazuri bila kuangalia yametolewa na nani! SIKU HIYO IKIFIKA NDIYO ITAKUWA SIKU YA KUIKOMBOA TANZANIA, NA SIO HAYA MAIGIZO YASIYO NA FAIDA YA UKOMBOZI YA CCM, CHADEMA, CUF N.K TUNAYOYAONA KILA SIKU.
 
hiyo kweli mkuu,kama misri kwa sasa hakuna aliyejuu ya mwenzake,kilicho bora kinafuatwa
 
Hakuna siku CHADEMA itachukua dola hii kwa structure yake ya sasa!
Hizo ni ndoto tena za mwendawazimu!
Futa topic yako maana unajadili mambo yasiyowezekana!
 
Futa topic yako maana unajadili mambo yasiyowezekana![/QUOTE mwendawazimu ni wewe unaejipa upofu bila kupewa, na roho itakuuma sana cdm inapaa, ukitaka usiione hiyo siku kufa leo au jinyonge chadema inachukua dola utake usitake
 
Hakuna siku CHADEMA itachukua dola hii kwa structure yake ya sasa!
Hizo ni ndoto tena za mwendawazimu!
Futa topic yako maana unajadili mambo yasiyowezekana!

Tatizo lako We Faiza Foxy unawaza CHADEMA kila kukicha. soma vizuri hoja ya mtoa mada utamwelewa
 
Naamini kuwa siku ya kuikomboa Tanzania sio siku ile CCM itakapong'olewa madarakani, au siku ile CHADEMA watakaposhika dola bali siku ya kuikomboa Tanzania ni siku ile watanzania tutakapoanza kuwaza na kufikiri zaidi ya hawa viongozi wetu wa kisiasa, siku ile ambayo wanachadema watawaza na kutafakari zaidi ya Mbowe, Dr Slaa, Lissu, Lema, Zitto n.k na pale wana ccm watakapowaza zaidi ya Dr Kikwete,Lowasa, Nape, Mukama n.k.

siku ambayo wote tutawaza kama binadamu na sio kama watu, siku tutakayowaza kama watanzaniawenye uwezo wa kuwaza wenyewe bila msaada wa mtu yeyote.

siku ambayo tutakubali kuyakubali mawazo yote mazuri bila kuangalia yametolewa na nani! SIKU HIYO IKIFIKA NDIYO ITAKUWA SIKU YA KUIKOMBOA TANZANIA, NA SIO HAYA MAIGIZO YASIYO NA FAIDA YA UKOMBOZI YA CCM, CHADEMA, CUF N.K TUNAYOYAONA KILA SIKU.

Mkuu, ulichokiandika kina ukweli, lakini naomba nitoe angalizo.
Siku hiyo haiji kama manna ya wana wa Israeli kule jangwani, huwa na chanzo chake ambacho tayari kipo lakini pia huwa na waanzilishi ambao nao wapo japo hutaki au unajifanya kutowatambua.
Hakuna vita isiyokuwa na jemadari wake.
 
Hakuna siku CHADEMA itachukua dola hii kwa structure yake ya sasa!
Hizo ni ndoto tena za mwendawazimu!
Futa topic yako maana unajadili mambo yasiyowezekana!

Soma vizuri mkuu. Mtoa hoja hakujadili chadema amejadili binadamu wa kitanzania.
 
Back
Top Bottom