Siku ya habari ya daudi mwangosi

we gule

Senior Member
Jun 30, 2012
136
18
Ndugu wanahabari wenzangu nakuja na pendekezo siku ya tarehe 2.9 ya kila mwaka iwe ni kumbukumbu ya marehemu DAVID MWANGOSI yaani SIKU YA HABARI YA DAVID MWANGOSI kwa siku hiyo waandishi wa habari kufanya yafuatayo:
1.Tafakari ya changamoto zinazo wakabili waandishi wa habari Tanzania.
2.Mafanikio yaliyofikiwa.
3.Nini kifanyike kuondoa changamoto zilizo jitokeza.
Naomba kuwasilisha.
 
Mimi naongezea kuwa ndiyo iwe siku ya utetezi wa haki kwa watanzania wote. Kwani marehemu Daudi Mwangosi alikufa akitetea haki ya kupata habari kwa watanzania na ulimwengu mzima.
 
Ndugu wanahabari wenzangu nakuja na pendekezo siku ya tarehe 2.9 ya kila mwaka iwe ni kumbukumbu ya marehemu DAVID MWANGOSI yaani SIKU YA HABARI YA DAVID MWANGOSI kwa siku hiyo waandishi wa habari kufanya yafuatayo:
1.Tafakari ya changamoto zinazo wakabili waandishi wa habari Tanzania.
2.Mafanikio yaliyofikiwa.
3.Nini kifanyike kuondoa changamoto zilizo jitokeza.
Naomba kuwasilisha.

Nisingefikiria kuweka siku nyingine ya wanahabari wakati ipo siku hiyo tayari ambayo inaadhimishwa iwe ya kitaifa au kimataifa. Siku kama hizo zimewekwa kwa ajili ya mengi ikiwemo kuwakumbuka wahanga wa habari nchini na duniani. Kma kila tukio, madaktari nao wataweka siku yao, basi utitiri huo utachosha.
 
Iwe siku ya kukumbuka na kulaani UKATILI WA VYOMBO VYA USALAMA DHIDI YA UBINADAMU NA USHINDI DHIDI YA UONGO NA PROPAGANDA CHAFU.

Ni tukio la kikatili, la aibu, lililotendeka mchana kweupe, huku kiongozi mkuu wa polisi (RPC) akishuhudia na hivyo kulibariki. Serikali ya CCM kupitia viongozi na vyombo vyake (maofisa wa polisi, waziri, msajili wa vyama, makada wa chama, TBC, n.k.) vya ngazi mbali mbali wakazusha uongo wao kama walivyozoea lakini kwa
damu ya Mwangosi ushindi ukapatikana na kila mtanzania kufumbuliwa macho.

Naunga mkono hoja - SAY NO TO LIES!
 
Back
Top Bottom