Siku timu ya Taifa ilipocheza vifua wazi

PongLenis

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
427
133
chuma.jpg

Kwa kweli tumetoka mbali sana... hii ni timu ya Taifa ya miaka ya 1970's. Hapa mgeni rasmi akipeana mikono na wachezaji ilikuwa Uwanja wa Taifa.

Pichani ni aliyekuwa Rais wa Sudan, Bwana Jaafar Mohammed Numeir (Wa kwanza Kulia Mwenye Suti) akiongozwa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Bwana Abdulrahman Juma (Katikati Mwenye Kaptula Nyeupe) kusalimiana na Mchezaji wa Nguli wa Taifa Starz Bwana Omar Zimbwe huku Wachezaji wa Taifa Starz wakiwa Vifua wazi bila Jezi.

Wa Kwanza Kushoto anayeangalia ni Mchezaji Mohamed chu
ma "Shoto" na wanaonekana nyuma ya Nahodha Abdulrahman ni Wachezaji Mashuhuri Kitwana Manara "Popat" na Abdallah "King" Kibaden Mputa, hapa ilikuwa katika Uwanja wa Uhuru (Uwanja wa Zamani wa Taifa, Jijini Dar es salaam).

Watu wengi wanapenda kuandika kuwa Mechi hii Taifa Stars walicheza vifua wazi (Bila Jezi) na sudan baada ya kukosekana jezi, Lakini ukweli wa mambo haukuwa hivyo bali kilichotokea ni kuwa Timu zote Mbili zilikuja Uwanjani zikiwa na Jezi zinazofanana.

Kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Shirikisho la Soka Duniani, FIFA ni kwamba kunapotokea Timu mbili zina jezi zinazofanana basi ile ambayo iko nyumbani (Wenyeji) ndiyo inatakiwa ibadilishe jezi, Taifa Stars hawakwenda Uwanjani na Jezi za Ziada.

Mara baada ya Ukaguzi uliofanywa na Rais Jaafar Mohammed Al- Numeir wa Sudan Starz waliletewa Jezi Nyengine na ndipo Mpira ukaanza huku Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa Uwanjani hapo kushuhudia Aibu hiyo ya Mwaka.

Hii ilikuwa mechi kati ta Taifa stars na timu ya Sudani.

Kama kawaida ya maafisa wa Serikali ya Tanzania mapuuza ni jadi yao. Mtu aliyetakiwa kuleta jezi aliingia mitini kwa hiyo timu ikaingia tumbo wazi uwanjani huyu anayekagua timu ni Rais wa Sudani, Jafar Nimeiri.

Stars ilishinda kwa goli tatu bila, nadhani Wasudani walikuwa wanashangaa manyoya va vifua wachezaji wa Stars!

Teh teh teh...!!
 
acha wewe 70's kitu cha jezi kilikuwepo hiyo ni mechi tu ya mchangani ya kipindi hicho umeona utuwekee kutuzuga ka ni kweli ni taifa stars nipe majina yao
 
hii ilikuwa mechi kati ta Taifa stars na timu ya sudani. kama kawaida ya maafisa wa serikasli ya Tanzania mapuuza ni jadi yao. mtu aliyetakiwa kuleta jezi aliingia mitini kwa hiyo timu ikaingia tumbo wazi uwanjani huyu anayekagua timu ni rais wa sudani Jafar Nimeiri. na stars ilishinda kwa goli ytatu bila. nadhani wasudani walikuwa wanashangaa manyoya va vifua wachezaji wa stars!!!! teh teh teh

Ni kweli mechi ilichezwa U/Taifa jezi zililetwa baada ya halftime. Marehemu Baba wa Taifa pia alikuwepo uwanjani booonge la aibu! ila yamepita hayo! Siku njema.
 
acha wewe 70's kitu cha jezi kilikuwepo hiyo ni mechi tu ya mchangani ya kipindi hicho umeona utuwekee kutuzuga ka ni kweli ni taifa stars nipe majina yao

mkuu unahistoria ya soka ya taifa letu kweli..?!
 
Kilichosababisha taifa stars kuwavifua wazi ni kwamba jezi zao zilifanana na za wasudani na hakukuweko za rangi nyingine
 
Pichani ni aliyekuwa Rais wa Sudan, Bwana Jaafar Mohammed Numeir (Wa kwanza Kulia Mwenye Suti) akiongozwa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Bwana Abdulrahman Juma (Katikati Mwenye Kaptula Nyeupe) kusalimiana na Mchezaji wa Nguli wa Taifa Starz Bwana Omar Zimbwe huku Wachezaji wa Taifa Starz wakiwa Vifua wazi bila Jezi.
attachment.php

Wa Kwanza Kushoto anayeangalia ni Mchezaji Mohamed chu
ma "Shoto" na wanaonekana nyuma ya Nahodha Abdulrahman ni Wachezaji Mashuhuri Kitwana Manara "Popat" na Abdallah "King" Kibaden Mputa, hapa ilikuwa katika Uwanja wa Uhuru (Uwanja wa Zamani wa Taifa, Jijini Dar es salaam).

Watu wengi wanapenda kuandika kuwa Mechi hii Taifa Stars walicheza vifua wazi (Bila Jezi) na sudan baada ya kukosekana jezi, Lakini ukweli wa mambo haukuwa hivyo bali kilichotokea ni kuwa Timu zote Mbili zilikuja Uwanjani zikiwa na Jezi zinazofanana.

Kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Shirikisho la Soka Duniani, FIFA ni kwamba kunapotokea Timu mbili zina jezi zinazofanana basi ile ambayo iko nyumbani (Wenyeji) ndiyo inatakiwa ibadilishe jezi, Taifa Stars hawakwenda Uwanjani na Jezi za Ziada.

Mara baada ya Ukaguzi uliofanywa na Rais Jaafar Mohammed Al- Numeir wa Sudan Starz waliletewa Jezi Nyengine na ndipo Mpira ukaanza huku Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa Uwanjani hapo kushuhudia Aibu hiyo ya Mwaka.
 
Attachments

  • vifua.jpg
    vifua.jpg
    12.4 KB · Views: 92
Huo ndio wakati wa Nyerere. Halafu bado watu wanamsifia.
 
Dah hiyo inaonekana ilikuwa kitambo sana...ila mie nimekunwa na jina Kitwana Manara "Popat'...
Hakika familia ya kina Manara walikuwa wanatisha, kuanzia kwa Kassim, Kitwana na Sunday
 
Ndiyo wakati huohuo timu yetu ya taifa ilicheza michuano ya nchi huru za Africa, Nyerere anastahili sifa na pongezi.
Timu ya Taifa kukosa jezi ni UZEMBE WA FAT

Uzembe ulikuwa nchi nzima, si kwenye mpira tu, hata kula ilikuwa ya shida. Mpaka ukae foleni kungoja kilo moja ya sukari kwa wiki kwa kaya.
 
Ulivyo na chuki na Nyerere inaonyesha hata ukitema mate yako lazima yana sumu kama ya nyoka.

Si chuki ni ukweli, ni kipi ambacho unapinga kuhusu nnayoyasema ya Nyerere? kuwa huo ulikuwa wakati wake na ulikuwa ni wakati wa uzembe?
 
Back
Top Bottom