Siku Tano za Magufuli

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Naomba kujua kama siku tano zimeisha na agizo limetimizwa au kauli zingine ni za kwenye TV tu.

ATOA SIKU TANO


Dk. Magufuli, alisema mkoa wa Dar es Salaam ndio unaoongoza kwa kuvunja sheria za barabarani na kusababisha msongamano wa magari usio wa lazima.

Kutokana na tatizo hilo, Dk. Magufuli alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuwafukuza wafanyabiashara waliovamia barabara ndani ya siku tano.
“Kwa mujibu wa kifungu namba 26 cha sheria namba 13 ya mwaka 2007, TANROADS ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia sekta ya barabara nchini.
“Kwenye ‘Service roads’ zote kumejaa wafanyabiashara na gereji bubu, hawa ndio wanaoendelea kuharibu barabara zetu na kusababisha msongamano usio wa lazima.

“Hata mkikuta hata bendera za CCM ndani ya barabara mzivunje, au bendera za CHADEMA, sheria ifuate mkondo wake kwa sababu haya ndiyo matatizo ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom