Siku Nilipomsikia Nyerere Akilitangazia Taifa Kifo Cha Edward Moringe Sokoine

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

KUNA wengi tunaokumbuka tulikuwa wapi siku ile ya tarehe 12 Aprili, 1984 wakati Mwalimu Nyerere alipolitangazia taifa kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine kilichotokana na ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar.

Kwa bahati mbaya, vijana wengi waliozaliwa baada ya 1984 hawajui sana habari za Edward Moringe Sokoine . Mimi nilikuwa Kidato cha Pili tu pale Sekondari ya Tambaza. Nakumbua ilikuwa majira ya saa kumi jioni. Nilikuwa natembea kwa miguu kutoka Kinondoni ’ A’ kuelekea nyumbani Kinondoni Biafra. Nilipofika maeneo ya jirani na Msikiti wa Mtambani nikasikia wimbo wa taifa unapigwa.

Nilihisi haraka kuna jambo kubwa la kitaifa limetokea. Nikasogea kwenye duka la jirani. Wapita njia wengine nao walisogea mahali hapo. Wimbo wa Taifa ulipomalizika, nikamsikia Mwalimu akianza kutamka kwa sauti ya huzuni; ” Ndugu Wananchi, leo hii…” Kilichofuata ni historia ambayo hapa nashiriki kuiandika.

Naam, Sokoine alikuwa kiongozi wa kweli ambaye daima alisimama upande wa umma. Ni Sokoine aliyetufanya hata tuliokuwa sekondari wakati huo, tuwe na imani na uongozi wa nchi. Tuwe na matumaini ya maisha bora kwa siku za baadae.

Ndio, ukitoka kwa Mwalimu, ni Sokoine pia aliyechangia katika kutufanya watoto wa wakati huo, tuamini na tuipende siasa. Alikuwa mfano wa kuigwa. Alishi kama alivyohubiri. Siyo tu hakujilimbikizia mali, halipunguza hata mali zake ili apate nafasi zaidi ya kututumikia Watanzania.

Itakumbukuwa, kwenye kikao cha Bunge cha mwezi Aprili, 1984, Sokoine alikabiliana n ahoja za wabunge kutaka kuongezewa posho na marupurupu yao. Sokoine alitamka;

” Ndugu Spika, niko tayari kuwaongezea wabunge posho ya chakula chao, lakini kamwe sitakuwa tayari kuwaongezea mishahara na marupurupu mengine.” Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye Edward Moringe Sokoine. Alikuwa kiongozi wa kanuni na mwenye msimamo usioyumba.

Sokoine alielewa, kuwa ukiwalinganisha na wananchi walio wengi, wabunge walikuwa na hali bora zaidi kimaisha. Alikuwa tayari kuchukiwa na wabunge kwa kutetea maslahi ya wanyonge, kuliko kupendwa na wabunge kwa kujali zaidi maslahi yao.

Baada ya kikao kile cha Bunge, Edward Sokoine, badala ya kupanda ndege ya Serikali kumrudisha Dar es Salaam, aliamua kurudi Dar Es Salaam kwa njia ya barabara, afanye hivyo ili mle anamopita apate nafasi ya kuona shughuli za maendeleo zifanywazo na wananchi. Sokoine hakufika Dar Es Salaam, mauti yakamchukua kwa ajali ya gari pale Wami- Dakawa, Morogoro.

Leo tuna viongozi wa wananchi wenye kutanguliza mbele maslahi yao binafsi. Viongozi wasiotosheka na posho ya elfu sabini ya kikao. Viongozi wenye kufikiria tu ’ kamuhogo kao’. Wanafikiri magari na marupurupu yao badala ya masuala yenye kuwahusu wananchi wa kawaida.

Je, Sokoine angefufuka leo ingekuwaje?
Bila shaka angefufuka na kufa tena ndani ya siku saba. Maana, Sokoine angeshangaa kuwaona wabunge wa leo wakichukua posho ya kikao cha siku moja sawa na mshahara wa miezi miwili au mitatu kwa Watanzania walio wengi.

Sokoine angeshangaa kuona wabunge hawatembelei tena Landrover za bei nafuu bali magari ya kifahari huku wananchi walio wengi bado wanaishi kwenye nyumba za udongo na nyasi. Kwamba bado kuna wanyonge wengi wasio na hakika ya kula yao ya leo na kesho huku wananchi wakiambiwa, tena na Spika wa Bunge, kuwa Bunge ni eneo la umasikini!

Sokoine angeshangaa kusikia kuwa uongozi siku hizi unanunuliwa, na hata yeye akijaribu tena kuingia Bungeni atalazimika agawe ’ Vimuhogo’ kwa watakaompitisha kwenye kura za maoni. Sokoine angeshangazwa pia kusikia, kuwa kuna mawaziri na watendaji wakuu serikalini wanaokaa mahotelini kwa kukosa nyumba za serikali kwa vile umepitishwa uamuzi wa kuziuza, kisha kujenga nyingine na kuziuza tena!

Lakini, Sokoine angeshangaa zaidi kuona Watanzania aliowaacha mwaka 1984 wamechelewa sana kuamka na kupambana kuibadili hali iliyopo.

Naam, Sokoine angefufuka leo, angesononeka sana kuona pengo pana lililopo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kati ya viongozi na wananchi.

Edward Moringe Sokoine, Daima Tutakukumbuka.

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Ndugu zangu,

KUNA wengi tunaokumbuka tulikuwa wapi siku ile ya tarehe 12 Aprili, 1984 wakati Mwalimu Nyerere alipolitangazia taifa kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine kilichotokana na ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar.

Kwa bahati mbaya, vijana wengi waliozaliwa baada ya 1984 hawajui sana habari za Edward Moringe Sokoine . Mimi nilikuwa Kidato cha Pili tu pale Sekondari ya Tambaza. Nakumbua ilikuwa majira ya saa kumi jioni. Nilikuwa natembea kwa miguu kutoka Kinondoni ' A' kuelekea nyumbani Kinondoni Biafra. Nilipofika maeneo ya jirani na Msikiti wa Mtambani nikasikia wimbo wa taifa unapigwa.

Nilihisi haraka kuna jambo kubwa la kitaifa limetokea. Nikasogea kwenye duka la jirani. Wapita njia wengine nao walisogea mahali hapo. Wimbo wa Taifa ulipomalizika, nikamsikia Mwalimu akianza kutamka kwa sauti ya huzuni; " Ndugu Wananchi, leo hii…" Kilichofuata ni historia ambayo hapa nashiriki kuiandika.

Naam, Sokoine alikuwa kiongozi wa kweli ambaye daima alisimama upande wa umma. Ni Sokoine aliyetufanya hata tuliokuwa sekondari wakati huo, tuwe na imani na uongozi wa nchi. Tuwe na matumaini ya maisha bora kwa siku za baadae.

Ndio, ukitoka kwa Mwalimu, ni Sokoine pia aliyechangia katika kutufanya watoto wa wakati huo, tuamini na tuipende siasa. Alikuwa mfano wa kuigwa. Alishi kama alivyohubiri. Siyo tu hakujilimbikizia mali, halipunguza hata mali zake ili apate nafasi zaidi ya kututumikia Watanzania.

Itakumbukuwa, kwenye kikao cha Bunge cha mwezi Aprili, 1984, Sokoine alikabiliana n ahoja za wabunge kutaka kuongezewa posho na marupurupu yao. Sokoine alitamka;

" Ndugu Spika, niko tayari kuwaongezea wabunge posho ya chakula chao, lakini kamwe sitakuwa tayari kuwaongezea mishahara na marupurupu mengine." Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye Edward Moringe Sokoine. Alikuwa kiongozi wa kanuni na mwenye msimamo usioyumba.

Sokoine alielewa, kuwa ukiwalinganisha na wananchi walio wengi, wabunge walikuwa na hali bora zaidi kimaisha. Alikuwa tayari kuchukiwa na wabunge kwa kutetea maslahi ya wanyonge, kuliko kupendwa na wabunge kwa kujali zaidi maslahi yao.

Baada ya kikao kile cha Bunge, Edward Sokoine, badala ya kupanda ndege ya Serikali kumrudisha Dar es Salaam, aliamua kurudi Dar Es Salaam kwa njia ya barabara, afanye hivyo ili mle anamopita apate nafasi ya kuona shughuli za maendeleo zifanywazo na wananchi. Sokoine hakufika Dar Es Salaam, mauti yakamchukua kwa ajali ya gari pale Wami- Dakawa, Morogoro.

Leo tuna viongozi wa wananchi wenye kutanguliza mbele maslahi yao binafsi. Viongozi wasiotosheka na posho ya elfu sabini ya kikao. Viongozi wenye kufikiria tu ' kamuhogo kao'. Wanafikiri magari na marupurupu yao badala ya masuala yenye kuwahusu wananchi wa kawaida.

Je, Sokoine angefufuka leo ingekuwaje?
Bila shaka angefufuka na kufa tena ndani ya siku saba. Maana, Sokoine angeshangaa kuwaona wabunge wa leo wakichukua posho ya kikao cha siku moja sawa na mshahara wa miezi miwili au mitatu kwa Watanzania walio wengi.

Sokoine angeshangaa kuona wabunge hawatembelei tena Landrover za bei nafuu bali magari ya kifahari huku wananchi walio wengi bado wanaishi kwenye nyumba za udongo na nyasi. Kwamba bado kuna wanyonge wengi wasio na hakika ya kula yao ya leo na kesho huku wananchi wakiambiwa, tena na Spika wa Bunge, kuwa Bunge ni eneo la umasikini!

Sokoine angeshangaa kusikia kuwa uongozi siku hizi unanunuliwa, na hata yeye akijaribu tena kuingia Bungeni atalazimika agawe ' Vimuhogo' kwa watakaompitisha kwenye kura za maoni. Sokoine angeshangazwa pia kusikia, kuwa kuna mawaziri na watendaji wakuu serikalini wanaokaa mahotelini kwa kukosa nyumba za serikali kwa vile umepitishwa uamuzi wa kuziuza, kisha kujenga nyingine na kuziuza tena!

Lakini, Sokoine angeshangaa zaidi kuona Watanzania aliowaacha mwaka 1984 wamechelewa sana kuamka na kupambana kuibadili hali iliyopo.

Naam, Sokoine angefufuka leo, angesononeka sana kuona pengo pana lililopo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kati ya viongozi na wananchi.

Edward Moringe Sokoine, Daima Tutakukumbuka.

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Well said brother Mjengwa.
 
Asante Mjengwa kwa kutukumbusha machungu ya siku hiyo.
Mimi nilikuwa , of all the places, Chakecake, Pemba.

Ulipopigwa wimbo wa Taifa , kwa miaka hiyo, ilikuwa inaashiria "danger", kitu cha kutisha sana kitakuwa kinatangazwa.
Bahati nzuri nilikuwa nyumbani kwangu pale machomanne.
Ile habari ilikuwa ya kutisha, kusikitisha na hata kuleta wasi wasi mkubwa.

Pale Machomanne , ni karibu na kambi ya Jeshi, na mara moja likaingia Stand-By.
Ni siku ambayo sito isahau.
 
duh, kumbukumbu muhimu sana hiii.... nakumbuka nilikuwa nimetoka shule, shule niliyokuwa nasoma ilikuwa mbali kidogo na nyumbani hivyo wakati wengine wanarudi mchana manyumbani kwao kupata msosi sisi tulibaki pale, ila baada ya masomo ya mchana sisi tulikuwa tunaruhusiwa kuondoka saa 9.30...... nakumbuka ilikuwa ni saa 10.55 ndio wimbo wa taifa ukapigwa, kilichofuata ni sauti, ambayo kama hukuwa makini sana unaweza sema sio sauti ya Mwalimu tuliyokuwa tumeizoea.... lakini ndio ukawa mwisho wa mzee weyu......Nisingependa kusema nilikuwa wapi, ila kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu, tuliambiwa hakuna kuwasha taa yeyote usiku ule na ndio tukalala giza
 
Kweli ni huzuni sana. NA kama ulivyosema kuwa akifufuka leo anaweza kuzimia tena ndani ya siku saba kutokana na hali ilivyo na aliyoiacha 1984.

Nakumbuka siku ile nilikuwa Shuleni pia, na majira ya saa SABA KASORO; tulikusanyika wote na Mwalimu Mkuu kwa huzuni alitangaza taarifa ya Kifo cha PM mpendwa Sokoine.

Nakumbuka wakati ule magazeti yalikuwa ni ya Chama na Serikali tu (Uhuru, Mzalendo, Daily News, Sunday News) KWa jinsi wananchi walivyoguswa na ule msiba nakumbuka kulikuwa na Foleni kubwa sana kila asubuhi katika vituo vya kuuza magazeti, na wengi walikuwa wanakosa.

Nakumbuka siku ya kusafirisha kwenda Arusha - Tulikuwa tunaishi Mbezi juu DSM, hivyo RTD walipotangaza kuwa ndege ndio inapaa uwanjani, na sisi ambao hatukuwa uwanjani tuliishuhudia ndege ya JESHI ikipaa hivyo tuliipepea mikono kwa huzuni kubwa ile ndege ikipaa na kuondoka.

NI HUZUNI SANA!!!!!!!!!!

Nashindwa kuendelea kwa uchungu!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Umesomeka Maggid.
Kwa sasa ni kheri tuweke chizi awe kiongozi wetu kuliko kuweka hawa wasomi ndo hapa walipo tufikisha kwa kujaza matumbo yao bila kuwa na huruma kwa wananchi walio wapa ridhaa ya kutawala.
 
Mi nakumbuka nikiwa na maruweruwe kichwani. Nilikuwa nasikia kupitia redio watu wakilia na wimbo maarufu 'Edward Sokoine kwaheri...' sikujua kwa uwazi ni nini hasa kinaendelea. Miaka miwili baadae nilianza darasa la kwanza
 
Ahsante Maggid kwa kutujuza!! Sokoine alifanya vitu ambavyo vinaishi hata baada ya kifo chake bado watu wanamkumbuka kwa matendo yake. Miaka 6 baadae ndiyo nilianza kujua kusikiliza redio, enzi hizo hata kiswahili kilikuwa hakipandi (Sasa naongea lugha 5 tofauti).
 
Its so sad and painful! Kwa sasa siyo rahis sana kupata kiongozi kama huyo mana wengi wanajua madaraka ni kujipaitia utajiri na siyo kuwatumikia waliowachagua! Eh Mungu isaidie Tanzanie !
 
Nilikua tumbon mwa mama yangu,hiyo miezi,nilizaliwa mwez waTisa 84,
ILA LEO UKINIULIZA KUHUSU SOKOINE
1.Huyu alifunika watanzania kwa kupendwa na zani ata baba wa taifa hamfikii,akua mbinafsi,nyerere anamzid jambo moja sokoine,kua muasisi tu(eshimu mawazo yangu)
2.nilisoma kitabu cha historia ya marehem nikiwa darasa la nne,machozi yalinitoka sana
 
Wengine tulikuta historia yake tu! Ila nakumbuka wakati nipo darasa la nne tulipata mwalimu wa uraia mzuri sana, alikuwa haishi kutusimulia matendo ya Edward sokoine! Na ilikuwa ikifika tarehe aliyotoweka, tunaimba nyimbo nahisi zilizoimbwa wakati wa kifo chake! Huwezi amin, kwa ile tu kuoneshwa picha zake na kusimuliwa historia yake, wengi wetu tulilia kama vile ametoweka siku hiyo! Eee Mungu, ibariki Tanzania izae mbegu za kina Moringe na Nyerere!
 
1984 dah! mimi nacheza tu ukuti ukuti miaka hiyo sina hata habari, ila nakumbuka kulikuwa na hali tete sana ya sukari, kuipata kama kupata magendo.
 
Kaka big up sana, kwa kutukumbusha wapigania haki za wanyonge na moja ya miamba mikubwa sana ya siasa hapa TZ na Afrika mashariki. kuna kitu naanza kujifunza kwa watanzania ambacho siku za nyuma sikuwahi kuzisikia. Kimsingi mtu yeyote anapotaka kubadilika kutoka hali aliyonayo kwanza ataanza kurejea historia yake ambayo itamfanya agundue ni wapi alipojikwaa na kuanguka ili ajirekebishe. Hili naliona kwa Watanzania wengi sasa. Ni historia pekee, na hali iliyopo kwa sasa ndio inayoweza kubadili uelekeo wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Hakika kwa hili naona mbele kuna mwanga kwa watanzania.

Walale pema waasisi wetu na watetezi wetu Nyerere and Sokoine
 
Back
Top Bottom