LAZIMA UTAVUNJIKA TU! VIASHIRIA NI VINGI MNO!
1. Malalamiko ya wazenji ni mengi mno - mara ooh tunaonewa!, mafuta yakigunduliwa yetu (kelele nyiingiii kabla ya ugunduzi, yakigunduliwa itakuwaje?
2. Wameshakamilisha hatua zote za kujitenga - wana Rais, wana katiba yao, wana wimbo wao wa Taifa, wana serikali yao, wana bendera yao, wana timu yao ya taifa, wana mashirika yao, wana majeshi yao, Zanzibar ni nchi kwa mujibu wa katiba yao, n.k. Je, kimebaki nini? Tanganyika ina nini cha kipekee? Vyote vya Muungano. Yaani Zanzibar ina CHANGU na CHETU, lakini Tanganyika imemezwa na kusikika kwa mbali kwenye CHETU!.
Tenende,
Katiba ya Zanzibar ni batili. Lakini usiwaambie waache wajidanganye. Ili katiba yao kuwa halali lazima ipitishwe na bunge la serikali ya muungano wa Tanzania kwa theluthi mbili za kura. Upo hapo? Waache wajidanganye.