Ni sikukuu ya pasaka. Kila Askofu aliyepata nafasi ya kuzungumza, alizungumzia siasa: katiba mpya, amani na mustakabali wa taifa. Kwanini tafakari za siku muhimu kama hii zisilenge kuwajenga waumini na wananchi wengine kiroho zaidi? kwanini siasa zinachukua sehemu kubwa ya maisha ya wa TZ kama vile ndiyo maisha yenyewe? Tuna muda mrefu wa kujadili siasa, mwaka mzima. Siku hizi chache za sikukuku kwanini tusiimarishe imani? Bila imani (kila mtu ana yake) kuna siasa safi?