Elections 2010 Siku kumi kuelekea uchaguzi mkuu,vyombo vya habari fanyeni hili......

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
napendekeza badala ya kuwapa wananchi taarifa za mikutano mbalimbali
ya kisiasa wakati wa taarifa za habari tu na tena usiku,ni vyema vyombo vya habari wakatenga muda wa wiki hii na haswa mchana kwa wale watakaokuwa hawabanwi na majukumu na marudi jioni kuwapa nafasi wale wa makazini,na vipindi vihusishe mtazamo na malengo yao kwa tz ya kesho yenye neema,watu wawapime wagombea wote na kufanya maamuzi sahihi,wito kwa tv zetu za umma na binafsi,taifa letu sote tuwasaidie watu wawajue viongozi watakaotutoa kwenye msiba huu wa umasikini,tuweke uzalendo mbele
 
Vioindi vyoote vya tamthilia,vichekesho,maigizo na vingine vinavyofanana na hivyo viwekwe likizo na watu waonyeshwe mtazamo na hoja mbalimbali za wagombea ili kufanya maamuzi sahihi.tukumbuke,tukiboronga sasa ni hadi miaka mitano ijayo ndio tutapata nafasi tena kama hii
 
Back
Top Bottom