Siku kama ya leo ukuta wa Berlin uliangushwa.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin na kusababisha Ulaya yoote kuambukizwa mfumo wa kibepari na kuwa mwisho wa mfumo wa kijamaa.

Ukuta huo uliangushwa tarehe 9 mwezi November mwaka 1989 jambo ambalo lilisukumwa sana na mabepari wa Ulaya magharibi.

Ukuta wa Berlin una urefu wa kilometa 155 na ulisimamishwa katika mji wa Berlin uliopo magharibi mwa ili kuzuia watumwa wa ubepari kuvuka kwenda katika miji ya kibepari.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za kukumbusha tukio hilo la kihistoria.

5_Germany_Wall_Anniversary_.sff_300.jpg

Tarehe 11 November 1989 picha ikionesha askari wa mpakani upande wa Ujerumani Mashariki wakiwa wamesimama kwenye geti liitwalo Brandenburg.

4_Germany_Wall_Anniversary_.sff.jpg

Askari wakishangaa baada ya nguvu za wananchi kuangusha sehemu ya ukuta huo.

3_Germany_Wall_Anniversary_.sff_300.jpg

Wananchi wa Berlin wakishangalia

2_Germany_Wall_Anniversary_.sff.jpg

Wananchi wakishangilia na kucheza juu ya ukuta siku hio.


1_Germany_Wall_Anniversary.sff.jpg


Jana watalii wakiangalia ukuta huo mjini Berlin.

Leo pia kutakuwa na kumbukumbu ya wale waliopoteza maisha yo kutokana na kugombea kuingia kupitia ukuta huo, watu 136 walikufa.

Viongozi wa mataifa yote 27 wa umoja wa Ulaya akiwemo raisi wa Russia Dmitri Medvedev, wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo.

Leo pia ni siku ya kumkumbuka mwanasayansi maarufu Albert Einstein ambae tarehe kama ya leo alitunukiwa tuzo maarufu ya Nobel ihusuyo Physics mwaka 1921.
 
Back
Top Bottom