Siku hizi vyama vya wafanyakazi vimekuwa haviheshimu mahakama

Unaniuma UFISADI wa kula hela za Walimu wanyonge unaofanywa na CWT. nimepata habari kuwa walimu wa Teachers Colleges wanataka kujitoa CWT kutokana na wimbi kali la ufisadi unaofanywa na jamaa kwa kujali matumbo yao wakidai wanatetea walimu

Mkuu makame, mimi niko salama kabisa Ni serikali pekee ndiyo inayopeleka Raia wake waloiweka madarakani kuwateka na kuwatesa mabwepande nashukuru Mungu anatupigania tupo salama

NILIKUWA NAMAANISHA HIZO PESA NI MICHANGO YETU HATA KAMA INGETUMIKA BILIONI 1 KWA AJILI YA HUU MGOMO SIO TABU AS LONG AS IMEPITISHWA NA WAJUMBE WENYE NGUVU YA KISHERIA YA KUPITISHA.

WEWE AMBAYE SIO MWANACHAMA UNAPATA TABU YA NINI KWA PESA AMBAZO SIO YAKO? KINA KUUMA NINI?
 
Mkuu

Hoja kwa Hoja ndio mwendo wetu jamvini.

Hoja hii niliitoa nilipoongelea suala la Generalization vs Individuals.

Nikasema Individuals ndio wanaodhalilisha Mahakama. Kama sasa wanavyodhalilisha Bunge Tukufu.

Ukasema hapana, Mmoja akioza wote wameoza; ndio nikakwambia hata kwa walimu kunanuka. Na huo ndio ukweli wenyewe. Dawa sio kuiwajibisha Serikali; dawa ni kuwawajibisha hawa wezi vikali. Mimi huwa nashangaa Mwizi wa Simu anavyopigwa mpaka kuchomwa moto; lakini ngeleja anapokelewa kama shuja; na wenzake mnawanyenyekea nyinyi walimu na kuhesabu na kulinda kura zao ikiwemo kuwapigia kura.

HUO NDIO UKWELI

Naomba usininukuu vibaya, sijataja walimu kuwa sio waadilifu ila nimetaja VYOMBO VYA DOLA na nimetoa mifano ikiwemo mahakama na Polisi... Na pia sina hakika na tuhuma unazozitoa kuhusu walimu lakini umeshindwa kutoa tuhuma kuhusu mahakama, Bunge Ikulu Jeshi PCCB na vingine

NA HATA KAMA HIZO TUHUMA NDIZO NI NANI MWENYE WAJIBU WA KUZISIMAMIA NA KUHAKIKISHA ZINATOKOMEZWA KABISA? NA KAMA HAKUFANYA HVO NA BADO TUHUMA UNAZOZITOA ZINAENDELEA KWA NINI HII SERIKALI ILOSHINDWA KUMALIZA TUHUMA ZA RUSHWA ISIWAJIBISHWE?

UKWELI UNAOUSEMA HAPO NI UPI?

MY TAKE: TUJIBU HOJA KWA HOJA.
 
LASIKOKI

Naamini ulikuwa umechoka; hivyo sikulaumu.

Kunichapa huwezi, hapa matumla akiniona anakula kona

:hat:
yaani huyu mleta mada anakera na kuudhi haswa!

Mara CHADEMA, mara majaji wanatoa hukumu kwa haki....yaani ungekuwa karibu ningekuchapa vibao vya kutosha kwa kuandika upuuzi wote huuzzzzzz!

Walimu gomeni, gomeni hadi mwisho.....haki haishi kirahisi, tupambane sote
 
Tuheshimu Sheria na Katiba iliyopo sasa; hicho ndio kipimo cha ustaarabu wetu.

Tunaendelea na mchakato wa Katiba Mpya; hilo wazo ni ZURI na itafaa zaidi lizingatiwe, ila kwa sasa tuendelee na kuheshimu utaratibu uliopo.

Mahakama hazitaheshimiwa, wala hazistahili kuheshimika kwa sababu ya mfumo wa sasa, tukumbuke kuwa viongozi wa mahakama ni wateule wa serikali. Hapa ndipo tunapoona hitaji la kuwa na katiba mpya.
 
[h=3]WALIMU IRINGA WAKACHA MGOMO, WAIGEUZIA KIBAO CWT, WATAKA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI YA MICHANGO YAO[/h]Na BONGO LEAKS WALIMU wa shule za msingi mjini Iringa wamekigeuzia kibao Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakipinga mgomo wake wa walimu ulioanza nchini kote leo na badala yake wametaka waelezwe kwanza mapato na matumizi ya michango yao ya kila mwezi kwa chama hicho.

“Tunasikia kuna majengo ya walimu yanajengwa nchi nzima, makatibu wa cwt wananuliwa magari, sasa kuna mpango wa kuanzisha benki, lakini hatupewi taarifa ya mapato na matumizi, na hata magari waliyopewa makatibu hayana msaada kwa walimu ambao ndio wenye mali hata kama wakiumwa,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mtwivilla,. Sidified Mapunda.
Alisema mgomo huo unawapa umaarufu viongozi wa chama hicho na hauna maana yoyote kwa walimu wa kawaida kwasababu taratibu za kuongeza mishahara ya walimu hazina tofauti na za watumishi wengine wa umma.Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi y a Wilolesi ambayo pia walimu wake wote walisusia mgomo hu, George Kameka alisema kabla ya kumgomea mwajiri wao, wanataka kufahamu tangu kutoka kwa chama chao hicho cha wafanyakazi tangu walimu nchini kote waanze kukatwa asilimia mbili kwa ajili ya kukichangia, mapato na matumizi yake yakoje.Alisema kuna taarifa zisizo rasmi kwamba CWT iko katika mstari wa mbele kudai maslai ya walimu ili mishahara yao ikipandishwa na wao wapandishe michango yao.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.

ndugu, muhimili huo umejishushia hadhi wenyewe kwa kuwa wala rushwa, wasiotenda haki, na sasa kutumika na serikali kila wanaponaa wamebanwa, ku kumbilia huko na kusingizia jambo liko mahakamani,
 
Mimi sio mtetezi wa serikali

natetea sheria

natetea utulivu

natetea amani

natetea haki

mahakama ni chombo chetu

mahakimu na majaji ni wasomi wanaotoa uamuzi kwa uhuru wa utaalamu wao

tuheshimu amri za mahakama

maana chadema wamekuwa mstari wa mbele kushabikia vurugu

tufikirie maendeleo jamani

sio kila siku vurugu za migomo

bila ya maendeleo hizo fedha za kuboresha maslahi zitatoka wapi??

Wewe unalo jambo na chadema maana kila jibu umeng'ang'ania kwel..
Ndo njia mpya mliyofundishwa ya kutuletea mada chafu juu ya CDM nin!!
Kaa na familia yako mjadili maendeleo, sisi acha tugome na ikizidi kukuuma katufungulie kesi nyengine... Umeelimishwa na kila mchangiaji ila kwa kichwa chako hicho kazi bure...
Masaburi mkubwa wew...
 
Nimeelimishwa nini Chi-Boy??

do you believe in Quality or Quantity??

Umeona Walimu wa Iringa walivyo na Busara?? wanaulizia taarifa ya matumizi na mapato.

CWT wamekuwa mafisadi

Wanafuja michango ya wanachama
\
na kuhusu chadema; inakuuma sana nikitaja sio chama bali KUNDI LA MASHABIKI WA MIGOMO?? Hiyo ndio taswira waliojijengea CHADEMA

Wewe unalo jambo na chadema maana kila jibu umeng'ang'ania kwel..
Ndo njia mpya mliyofundishwa ya kutuletea mada chafu juu ya CDM nin!!
Kaa na familia yako mjadili maendeleo, sisi acha tugome na ikizidi kukuuma katufungulie kesi nyengine... Umeelimishwa na kila mchangiaji ila kwa kichwa chako hicho kazi bure...
Masaburi mkubwa wew...
 
ninapata ugumu kuchangia kwani ''Makame'' post yake imekaa kiumbeumbea vile!.
Vyama vya wafanyakazi ni vile vilivyosajiriwa kwa kufuata taratibu zote kama inavyoainishwa kwenye Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini No.6 ya 2004 na kwapamoja vinaunda shirikisho ambalo ni TUCTA, CWT-kinavigezo vyote ktk hilo lakini Madaktari labda wewe MAKAME unakielewa vipi:
Lakini kama hiyo haitoshi mpaka Walimu kufikia hatua ya kuitisha mgomo kumbuka ni hatua zipi zilifuatwa hadi kupelekea Mahakama-''Division ya kazi'' kupitia CMA kutoa FOMU No.5 ambayo sijui we ''Makame'' unajua maana yake, kama ujui basi uliza wataalamu wakwambie nini ufuata mara baada ya FOMU No.5 kutolewa alafu ndo uje na hoja yako ya kwamba ''Vyama vya wafanyakazi havieshimu Mahakama''
 
PrN-Kazi

Naona umekupuka.

umeona michango kwenye thread?

Nicolaus kasikika akisema kuwa utaratibu bado haujatosheleza ku warrant MGOMO. kWANZA MKOBA KA SIGN KITABU!

ninapata ugumu kuchangia kwani ''Makame'' post yake imekaa kiumbeumbea vile!.
Vyama vya wafanyakazi ni vile vilivyosajiriwa kwa kufuata taratibu zote kama inavyoainishwa kwenye Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini No.6 ya 2004 na kwapamoja vinaunda shirikisho ambalo ni TUCTA, CWT-kinavigezo vyote ktk hilo lakini Madaktari labda wewe MAKAME unakielewa vipi:
Lakini kama hiyo haitoshi mpaka Walimu kufikia hatua ya kuitisha mgomo kumbuka ni hatua zipi zilifuatwa hadi kupelekea Mahakama-''Division ya kazi'' kupitia CMA kutoa FOMU No.5 ambayo sijui we ''Makame'' unajua maana yake, kama ujui basi uliza wataalamu wakwambie nini ufuata mara baada ya FOMU No.5 kutolewa alafu ndo uje na hoja yako ya kwamba ''Vyama vya wafanyakazi havieshimu Mahakama''
 
Kwa kuwa naona Mahakama inatoa maelekezo lakini wanayapinga. Au ndio chachu ya kusema nchi isitawalike?

  1. Madaktari --hawakuheshimu maamuzi halali ya mahakama;
  2. Walimu ----- wamesema hawatoheshimu.

kitendo cha kwenda kinyume na amri za mahakama sio ishara njema, na kitatufanya tuwe kama majahili. hatuna majadiliano, hatuna heshima, hatujui mamlaka wala hatuna ustaarabu.

Tuheshimu MAHAKAMA

PHP:

Ni vyema tunapoanzisha Topic tuanze kwa kuomba ushauri kabla ya kutoa shutuma dhidi ya kundi la jamii ay mtu fulani. Topic yako imenisikitisha sana hasa nikizingatia kuwa Serikali inapotosha ukweli alafu baadhi ya wana JF tunapokea upotoshaji huo bila hata ya kuuchambua kikamilifu. Mleta mada, tafadhali angalia yafuatayo:

1. Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004, inaeleza wazi kuwa "NI CHAMA CHA WAFANYAKAZI KULICHOSAJILIWA PEKEE NDICHO CHENYE HAKI YA KUITISHA MGOMO" Kwa upande wa Madaktari, wao walivunja Sheria tangu awali pale walipotumia Chama cha Wanataaluma ya Udaktari (MAT) kuitisha mgomo badala ya kutumia chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa. Mahakama ilikuwa na haki ya kuzuia mgomo ule kutokana na ukiukwaji huo mkubwa wa Sheria.

2. CWT wanaongea wakiwa kifua mbele juu ya kutositishwa kwa Mgomo uliopo kutokana na sababu zifuatazo:
a) Sheria inaelekeza kuwa, inapotokea mgogoro wa 'MASLAHI' Conflict of interest, Chama cha Wafanyakazi kinachohusika, kitaomba kukutana na Mwajiri na kufikisha madai husika. Iwapo majadiliano hayatafikia hatua ya makubaliano, Chama kitapeleka shauri CMA (Commission for Mediation and Arbitration) ambao wanatakiwa kusuluhisha mgogoro ndani ya siku 30. Baada ya kipindi hiki kwisha na pande mbili zikashindana mbele ya Msuluhishi, Upande wa Chama unaweza kuanza mchakato wa kuitisha mgomo.

b) Kama Mahakama inaendeha kesi inayohusu madai ya Walimu, mbona Mahakama yenyewe haitoi zuio la Mgomo!? Hii inatokana na ukweli kuwa Mahakama imeona Mgomo wa CWT umezingatia vigezo vyote na hivyo hakuna sababu za kuwazuia wasigome.

Kumbuka, mgomo ndiyo silaha ya mwisho kwa mfanyakazi, hivyo kama kila njia ikishindikana, wafanyakazi wanalazimika kutumia silaha hii..

naomba tuwaunge mkono walimu ili haki itendeke
 
Unapaswa kufahamu kuwa si kila amri/hukumu ya mahakama ni halali, mahakama za serikali ya JK ni haramu kwani zimekuwa mhimili wa kuvunja haki za binadamu. Haki hizo zipo kwenye Bill of Rights iliyomo kwenye Katiba ya Tanzania. Hukumu haramu haiwezi kuheshimiwa kama ambavyo mahakama zenyewe na majaji wake walivyokosa heshima mbele ya jamii. Asiyejiheshimu hastahili kuheshimiwa. NI nguvu ya Umma tu inayofanya kazi sasa
 
Wakati Mahakama inatoa HUKUMU in favor of John John Mnyika; Wakati inatoa Mahakama in favour of Heche na ilipomuangusha Mbunge wa CCM Sumbawanga je Hukumu hizo hazikuwa halali??

Unapaswa kufahamu kuwa si kila amri/hukumu ya mahakama ni halali, mahakama za serikali ya JK ni haramu kwani zimekuwa mhimili wa kuvunja haki za binadamu. Haki hizo zipo kwenye Bill of Rights iliyomo kwenye Katiba ya Tanzania. Hukumu haramu haiwezi kuheshimiwa kama ambavyo mahakama zenyewe na majaji wake walivyokosa heshima mbele ya jamii. Asiyejiheshimu hastahili kuheshimiwa. NI nguvu ya Umma tu inayofanya kazi sasa
 
SOLOMO

Unachezea technicalities.

Tunafahamu kwamba taratibu zimefuatwa; ila kwa kuwa pande hizi 2 ziliwasili Mahakamani Ijumaa na kuagizwa zikamilishe maelezo yake by 31st July 2012; kilichotegemewa ni kwamba Pande hizi mbili zingefuata mwongozo huo wa Mahakama.

Kilichotokea, ni kwamba CWT haikutaka kufuata utaratibu huo na instead wakatangaza mgomo in 48 Hours.

Kwa hilo mimi sidhani kwamba ni sahihi.

Kwani wangesubiri, wakawasilisha maelezo yao; na MAHAKAMA ingetoa ruling in their favor ingekuaje?
Ni vyema tunapoanzisha Topic tuanze kwa kuomba ushauri kabla ya kutoa shutuma dhidi ya kundi la jamii ay mtu fulani. Topic yako imenisikitisha sana hasa nikizingatia kuwa Serikali inapotosha ukweli alafu baadhi ya wana JF tunapokea upotoshaji huo bila hata ya kuuchambua kikamilifu. Mleta mada, tafadhali angalia yafuatayo:

1. Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004, inaeleza wazi kuwa "NI CHAMA CHA WAFANYAKAZI KULICHOSAJILIWA PEKEE NDICHO CHENYE HAKI YA KUITISHA MGOMO" Kwa upande wa Madaktari, wao walivunja Sheria tangu awali pale walipotumia Chama cha Wanataaluma ya Udaktari (MAT) kuitisha mgomo badala ya kutumia chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa. Mahakama ilikuwa na haki ya kuzuia mgomo ule kutokana na ukiukwaji huo mkubwa wa Sheria.....
 
nadhani mtoa hoja anatazama upande mmoja na mwingine haangalii. Ili haki itolewe inatakiwa ni lazima kuwe na pande mbili ya mlalamika na mlalamikiwa na wote wanatakiwa kutoa hoja juu ya jambo lililoko mbele ya mahakama na kutoa haki baada ya kupima pande zote mbili. Kwa sasa ni tofauti serikali inakimbilia mahakamani na mahakama bila kuuliza au kusikiliza upande wa pili inatoa mahamuzi kwa msingi wa serikali. Mfano ni rahisi mlalamikaji anapopeleka kesi mahakamani ni jaji bila kusikiliza upande wa pili na akatoa hukumu, hii hukumi inakuwa si ya haki hata kidogo na haikubaliki kwa jamii yoyote ile. Kuna mambo kesi nyingi ambazo zimetia doa na mahakama kushindwa kutoa au kusimamia sheria hasa kwenye kesi ya mgombea huru/binafsi, kesi ya ubunge Arusha na mifano mingine mingi unaweza kutaja. La msingi ni kusimamia haki na mahakama kutenda haki ndio maana mpaka sasa watu wenye huelewa wa juu hawapeleki jambo lolote mahakamani kulingana na haki inavyopatikana isivyo halali. Nawakilisha
 
Wewe MTANYAMALI akili zako ziko sehemu gani?

Kama una hamu ya kuongeza posts; weka zenye maana
Ukweli ni kwamba wewe MAKAME unachoongea ni pumba, kwa hiyo kwa sababu mshahara wako wa upendeleo ni mkubwa unafikiri ni wote, et wafanyakazi waheshimu mahakama so what?
 
Ni vyema tunapoanzisha Topic tuanze kwa kuomba ushauri kabla ya kutoa shutuma dhidi ya kundi la jamii ay mtu fulani. Topic yako imenisikitisha sana hasa nikizingatia kuwa Serikali inapotosha ukweli alafu baadhi ya wana JF tunapokea upotoshaji huo bila hata ya kuuchambua kikamilifu. Mleta mada, tafadhali angalia yafuatayo:

1. Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004, inaeleza wazi kuwa "NI CHAMA CHA WAFANYAKAZI KULICHOSAJILIWA PEKEE NDICHO CHENYE HAKI YA KUITISHA MGOMO" Kwa upande wa Madaktari, wao walivunja Sheria tangu awali pale walipotumia Chama cha Wanataaluma ya Udaktari (MAT) kuitisha mgomo badala ya kutumia chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa. Mahakama ilikuwa na haki ya kuzuia mgomo ule kutokana na ukiukwaji huo mkubwa wa Sheria.

2. CWT wanaongea wakiwa kifua mbele juu ya kutositishwa kwa Mgomo uliopo kutokana na sababu zifuatazo:
a) Sheria inaelekeza kuwa, inapotokea mgogoro wa 'MASLAHI' Conflict of interest, Chama cha Wafanyakazi kinachohusika, kitaomba kukutana na Mwajiri na kufikisha madai husika. Iwapo majadiliano hayatafikia hatua ya makubaliano, Chama kitapeleka shauri CMA (Commission for Mediation and Arbitration) ambao wanatakiwa kusuluhisha mgogoro ndani ya siku 30. Baada ya kipindi hiki kwisha na pande mbili zikashindana mbele ya Msuluhishi, Upande wa Chama unaweza kuanza mchakato wa kuitisha mgomo.

b) Kama Mahakama inaendeha kesi inayohusu madai ya Walimu, mbona Mahakama yenyewe haitoi zuio la Mgomo!? Hii inatokana na ukweli kuwa Mahakama imeona Mgomo wa CWT umezingatia vigezo vyote na hivyo hakuna sababu za kuwazuia wasigome.

Kumbuka, mgomo ndiyo silaha ya mwisho kwa mfanyakazi, hivyo kama kila njia ikishindikana, wafanyakazi wanalazimika kutumia silaha hii..

naomba tuwaunge mkono walimu ili haki itendeke

Nashukuru kwa kutuelewesha, Mtu makini huelewa kwanza mambo kabla ya kudandia kama huyo makame aliyedandia uzi kwa kujisikia kuandika hayo aloandika.
 
... Mpaka tufike 2015, kutakuwa na migomo mingi sana kama serikali itaendelea na tabia ya kuku anakunya, bata anaharisha! Double standards! Ni kwamba watu wengi wanazidi kugundua serikali yao imeshindwa kutawala (ombwe la uongozi), imeelemewa na imekosa uongozi ktk masuala ya msingi. Matokeo yake, kila mtu anaibuka na kuanza "kuongoza" jamii au jumuiya yake kwakuwa hatuna uongozi unaotungoza watu wote kama watanzania.

Hivi ni nani anayejua kama watanzania wote watahesabiwa wakati wa sensa mwaka huu? Kuna viongozi wa dini wameshahamasisha wafuasi wao kutoshiriki sensa. Umesikia kiongozi wa juu (waziri mkuu, rais) akilizungumzia hili? Haya mabilioni yaliyokopwa ili kuendesha sensa ndo kusema yatapotea bure? Jamii zingine zinaona na kujifunza kuwa kumbe inawezekana kuidindia serikali-unategemea migomo itaisha leo?

Kuna propaganda kwamba kuna vyama vya upinzani vinachochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini. Wafuasi wao wanapigwa na kupewa kesi sehemu mbali mbali nchini. Well and good! Lakini kwa sasa, kila mtu anajuwa kwamba kama kuna kitu kitatuletea machafuko makubwa muda si mrefu basi ni religious extremism. Serikali haioni vitisho na chuki inayotangazwa na vyombo vya habari vya kidini. Imelala. Eti ndo demokrasia. Demokrasia gani kwa vyombo vya dini lakini sio madaktari wanaodai haki zao? Kuna demokrasia gani wakati wapinzani wanapigwa, wanauawa na kubambikiziwa kesi? Double standards! Kweli binadamu anajisaidia wakati kuku anakunya!
 
Ndg yangu, Mgomo unaitishwa inapotokea madai ya kimaslahi (Conflict of interest). Sasa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa madai ya kimaslahi kutokana na kwamba madai hayo kutokuwepo katika waraka wala sheria yoyote ambayo Mahakama ingetumia kutoa hukumu au uamuzi wa mgogoro.

Kutokana na ukweli huo, mgogoro wa kimaslahi huwa unamalizwa kwa MAJADILIANO ya pande zinazohusika (Wafanyakazi na Mwajiri) na sio Mahakamani. Kama mahakama itasikiliza shauri la aina hiyo, basi wanachokifanya ni kukutanisha pande mbili hiweze kufikia makubaliano juu ya Mgogoro wa Maslahi.
 
Wewe kweli Vijijini Lawama na unapenda kulaumu!

Soma thread, amejibiwa

Nashukuru kwa kutuelewesha, Mtu makini huelewa kwanza mambo kabla ya kudandia kama huyo makame aliyedandia uzi kwa kujisikia kuandika hayo aloandika.
 
Hiyo itakua sio nchi, itakuwa kichaka cha watu wasio na ustaarab u

Barabarians
ina maana huoni kwamba nchi imeshakuwa kichaka,hawa wanafunga barabara,madaktari wanagoma sasa waalimu huku wabunge wanaiba na hakuna sheria yeyote inayochukuliwa mpaka watoto wadogo wanaandamana hovyo hovyo kabisa nchi ya kiendawazimu hii.
 
Back
Top Bottom