Siku hizi vyama vya wafanyakazi vimekuwa haviheshimu mahakama

Kwenye hilo napenda nikukumbushe kuwa BOTH CWT na SERIKALI walienda MAHAKAMANI. sasa kwanini wakati Mahakama imeomba muda; tena wa Masaa kadhaa CWT wagome? au kwa kuwa LIWALO NA LIWE YA CHANDIMU?

Inakuwaje mahakama inaomba mda tena baada ya kuwa imeshatoa hukumu na cheti kinachoonyesha usuluhishi umeshindikana? Jamani Huu siniuhuni wa wazi? Yani unahukumu halafu kesho unaendelea kusikiliza kesi? kama hukuwa na maelezo ya kutosha kwa nini utoe hukumu?

UHUNI KAMA HUU NDO UNAOUFANYA HUO MHIMILI WA DOLA KUONEKANA HAUNA MAANA NA KUDHARAULIWA NA WANANCHI. HAYA PROVE ME WRONG KWA HILI.
 
NDUGU JILE 79

Mimi bado nasisitiza kuwa Mahakama ndio chombo cha sheria Nchini. CWT wanakitumia na Serikali wanakitumia. Mahakama iko huru, na inaweza kuitaka serikali itimize maagizo yake.\

Mie ningeelewa Mgomo dhidi ya MADUDU YA TANESCO yanayopoteza mabilioni. Hayo Mabilioni yangeokolewa; Walimu watapata madai yao; Madaktari; Polisi, na pia Daraja la Kigamboni litajengwa!

Makame kwa nini huo mgomo juu ya tanesco usiuanzishe wewe?
 
Gwalihenzi.

Ni kwamba

Kama Mahakama imeziamuru pande zote mbili kukamilisha maelezo, IMPLIEDLY imesema kuwa baada ya maelezo ndio itatoa LOCUS STANDE ya shauri la Walimu. Kitendo cha wao kutangaza Mgomo kuanzia tarehe 30, wakati Mahakama imeagiza Maelezo yawe submitted tarehe 31 ni kukiuka LEGAL GUIDANCE ya Mahakama. All parties ought to honour the wise directive of the Court.

Sio CWT kutafuta loophole ya kukanyaga 240 million Tshs kwa njia za ubabaishaji. Wangesubiri shauri halali ya mahakama.

Hiyo hela wangetumia sehemu ndogo kuajiri Mawakili Mahiri watete shauri lao Mahakamani

Makame mbona hizo mil 240 umezikazania sana? kuna nini hapa? Hoja yako ilikuw ani mahakama kutoheshimika saiz mil 240 au ndo Propaganda mloamua kuanzisha ili mtugombanishe? sisi hatutagombana kwa hili aisee. Mtuache wenyewe kama hatujaridhika tutasema wenyewe.. wewe sio msemaji wetu
 
HALAFU HII KAULI

'Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu' inatumika vibaya.

Wacheni upotoshaji NYINYI wenye Fikra za ovyo za kutaka kuleta ghasia Bongo.

Watu tunataka tufikirie maendeleo na mambo makubwa

SIO KILA KUKICHA MIGOMO

Hili Halipingiki... Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu

Ghasia na Migomo Bongo inaletwa na Viongozi wa serikali wenye uwezo mdogo wa kutatua matatuizom kwa njia ya majadiliano wakiamini UBABE, NGUVU YA VYOMBO VYA DOLA NA VITISHO ndiyo suluhisho kumbe wanaharibu nchi kabisa

Tunapataje maendeleo katika hali ambayo raia hawawezi kupata hata Panadol mahospitalini wanakufa kwa kukosa oxygen gas ambayo lita 1 ni sh 200 lakini VX V8 hazijawahi kukosa Petrol, wananchi hawawezi kuaford hata Chakula umeme maji kwao ni story

Kama haya madogo tumeshindwa hayo makubwa unayofikiria ni yapi? Unajua unanishangaza aiseeeeee.
 
mahakama ilikataza mitambo ya downs/richmond isiguswe hadi pingamizi yaliyoko mahakamani yatolewe hukumu....... lakini badala yake, mitambo iliuzwa................na mahakama ilifyata........hao symbion ndio wanatuuzia umeme kwa miatambo ambayo..............ununuzi wake tulikopwa hela ya kuidhamini.............!

-Sasa kuna mahakama hapo.....au is just a poppy, anaye ambiwa kamata yule......, yule mwache....?!

-Mahakama inayowaadhibu wezi wa kuku miaka 5 jela, wezi wa epa miaka miwili.....!
 
Mngeamua wenyewe kugoma CWT isingeidhinisha Tshs 240 million zitumike kuhamasisha mgomo!

Unadhani zoezi hili lingefanyika bila Pesa? Mbona serikali yako ilotumia zaidi ya Bil 2 kufanya propaganda kuzuia Mgomo wa Madaktari kwa kuwalipa wanahabari feki na TV Na maofisa usalama katk field agent hujasema? Nasasa wameanza kutumia tena kwetu sisi sijui safari hii watatumia billion ngapi.. Hizo pesa kwa nini hawazitumii kutatulia matatizo haya badala yake wanafanya Propaganda?
 
HALAFU HII KAULI

'Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu' inatumika vibaya.

Wacheni upotoshaji NYINYI wenye Fikra za ovyo za kutaka kuleta ghasia Bongo.

Watu tunataka tufikirie maendeleo na mambo makubwa

SIO KILA KUKICHA MIGOMO
Naona hapo kwenye redi umeamua kutuchekesha. watu wapi wanaofikiria maendeleo na mambo makubwa? Enyi magamba acheni kutusanifu watz. mmeruhusu wageni kung'oa kila kilicho cha thamani, mmeuza ardhi yetu kwa kodi tsh 200 kwa ekari moja kwa mwaka. wageni wanaleta hadi madege yao ya kijeshi kubeba twiga wetu na wanyama wengine wanakwenda kwa mikataba ya kimangungo. hospitali zetu hazina madaktari, lakini ninyi hawa wachache waliopo mnawatimua!! hayo mambo makubwa mnayofikiria isije kuwa mnawaza kutuuza sisi watz maana tafsiri ya maendeleo kwenu nyie ni kuuza kila kinachoonekana mbele yenu. mahakama mmezifinyanga mpaka zimekuwa kama mnavyotaka ziwe kwa ajili ya kukandamiza haki za wanyonge. mtu akitaka kudai haki ananyamazishwa eti swala liko mahakamani.TAMBUENI YA KUWA MNAWALAZIMISHA WATZ KUZIDHARAU MAHAKAMA. Ole wenu siku hiyo ikifika
 
mahakama ilikataza mitambo ya downs/richmond isiguswe hadi pingamizi yaliyoko mahakamani yatolewe hukumu....... lakini badala yake, mitambo iliuzwa................na mahakama ilifyata........hao symbion ndio wanatuuzia umeme kwa miatambo ambayo..............ununuzi wake tulikopwa hela ya kuidhamini.............!

-Sasa kuna mahakama hapo.....au is just a poppy, anaye ambiwa kamata yule......, yule mwache....?!

-Mahakama inayowaadhibu wezi wa kuku miaka 5 jela, wezi wa epa miaka miwili.....!

haaah haah naunga mkono hoja mia.mia
 
Majadiliano ya dhati mbona ndio CWT imeyagomea??

Mimi nadhani, kitendo cha kutangaza mgogoro cha CWT dhidi ya muajiri wake ni ngao tosha ya CWT inayomlazimisha muajiri aende mezani kutafuta suluhu. Sasa wakati suluhu inafanyiwa kazi; CWT wanagoma, sasa kitendo cha kugoma hakina maana kuwa madai ya walimu yatatekelezwa kwa kitendo hicho.

Muajiri ana maoni yake na CWT ina maoni yake; wakae chini na kujadiliana.

Mimi nadhani, na nitaendelea kudhani mgomo ni pre mature.

Committee for Mediation and Arbitration ikishindwa kusuluhisha; Mahakama inasikiliza shauri; na endapo itaridhika kwamba MUAJIRI hajashughulikia madai ya waajiriwa ipasavyo; itatoa kibali cha mgomo; tena ita specify muda wa mgomo. Kwa sababu kugoma kwa walimu ni janga kwa taifa; ni kuwatia adabu watoto ambao hawana hatia; ni kuwekeza mbegu mbovu kwa ajili ya kizazi kijacho. tunaenda kwenye utandawazi, inabidi kuyafikiria haya.

Mzee nafahamu hutonielewa, kwa sababu Nurse analipwa twice as much as mwalimu kwa wale waliomaliza form four na kufanya certificate ya 2 years. Ndio maana ya majadiliano; sio migomo Mkuu Tonnyalmeida

Sijauona na sitaki kuuona kwa sababu sidhani kama unasuluhisho la dhati la matatizo ya nchi hii... Wao wawe na msimamo wao na mimi binafsi na baadhi ya walimu wenzangu tutakuwa na msimamo wetu ambao uko ndani ya nafsi zetu na huu hautaondolewa hata kwa vifaru ispokuwa majadiliano yenye nia ya dhatu ya kutatua matatizo katika taifa hili.
 
Siwezi kukulaumu, kwa kuamua kuwa na fikra nyembamba.

Kila mtu anaumia na migomo hii; tena wanaoumia zaidi ni wale wanyonge.

Wewe unataka mwanao asome; walimu wamegoma UTAFANYAJE?? Utaanza kutafuta njia mbada ambazo zitakuingiza katika gharama kubwa zaidi. ile nyongeza ya gharama ungeliitumia kwa matumizi ya maendeleo. Same applies to migomo mingine.

Wa TZ wanadharau Mahakama pale inaposema ukweli, ila pale inapotoa hukumu ya kuwabeba magwanda wanasema mahakama safi?? sidhani; hao itakuwa CHANDIMU

Naona hapo kwenye redi umeamua kutuchekesha. watu wapi wanaofikiria maendeleo na mambo makubwa? Enyi magamba acheni kutusanifu watz. mmeruhusu wageni kung'oa kila kilicho cha thamani, mmeuza ardhi yetu kwa kodi tsh 200 kwa ekari moja kwa mwaka. wageni wanaleta hadi madege yao ya kijeshi kubeba twiga wetu na wanyama wengine wanakwenda kwa mikataba ya kimangungo. hospitali zetu hazina madaktari, lakini ninyi hawa wachache waliopo mnawatimua!! hayo mambo makubwa mnayofikiria isije kuwa mnawaza kutuuza sisi watz maana tafsiri ya maendeleo kwenu nyie ni kuuza kila kinachoonekana mbele yenu. mahakama mmezifinyanga mpaka zimekuwa kama mnavyotaka ziwe kwa ajili ya kukandamiza haki za wanyonge. mtu akitaka kudai haki ananyamazishwa eti swala liko mahakamani.TAMBUENI YA KUWA MNAWALAZIMISHA WATZ KUZIDHARAU MAHAKAMA. Ole wenu siku hiyo ikifika
 
Hayo maneno ya mtaani; fedha ya Serikali haitumiwi kinyemela hivyo.

Matumizi mabaya ya fedha za Serikali huwa hayafanywi na Serikali kukandamiza RAIA WAKE.

Matumizi mabaya ya Fedha za Serikali hufanywa na watu wenye tamaa ya kuneemesha matumbo yao kama akina NGELEJA; ZITTO KABWE, MALIMA nk kwenye sakata la TANESCO;

Ungeni Mkono vita dhidi ya matumizi ya aina hiyo na sio kuendelea kuikwaza Serikali inayowatumika

Unadhani zoezi hili lingefanyika bila Pesa? Mbona serikali yako ilotumia zaidi ya Bil 2 kufanya propaganda kuzuia Mgomo wa Madaktari kwa kuwalipa wanahabari feki na TV Na maofisa usalama katk field agent hujasema? Nasasa wameanza kutumia tena kwetu sisi sijui safari hii watatumia billion ngapi.. Hizo pesa kwa nini hawazitumii kutatulia matatizo haya badala yake wanafanya Propaganda?
 
That is a gross misreporting of the facts. na nadhani umelishwa sumu mbaya dhidi ya mahakama.

Sema kuna haja ya ku revisit sheria zetu kwenye adhabu za uhujumu wa uchumi.

mahakama ilikataza mitambo ya downs/richmond isiguswe hadi pingamizi yaliyoko mahakamani yatolewe hukumu....... lakini badala yake, mitambo iliuzwa................na mahakama ilifyata........hao symbion ndio wanatuuzia umeme kwa miatambo ambayo..............ununuzi wake tulikopwa hela ya kuidhamini.............!

-Sasa kuna mahakama hapo.....au is just a poppy, anaye ambiwa kamata yule......, yule mwache....?!

-Mahakama inayowaadhibu wezi wa kuku miaka 5 jela, wezi wa epa miaka miwili.....!
 
Unajua hakuna UBABE, NGUVU WALA VITISHO.

Serikali inataka majadiliano; CWT imeamua kutaka Public Sympathy in a wrong way. kwani Serikali iko tayari kwa majadiliano.

Ama kuhusu suala la kukosa vifaa hosp, hali kuwa ngumu na V8 kuwa na mafuta ikiwemo matengeneza ya gharama hilo nakubaliana na wewe, dawa akina

  1. Ngeleja,
  2. malima,
  3. Zitto,
  4. Kilango,
  5. Sendeka
and the list goes on; wachukuliwe hatua kali.

Tatizo, eti wabunge waliosababisha hasara ya mabilioni ambazo zingeweza kutumika kutatua matatizo mengi ya madai ya watumishi wanaundiwa kamati na wabunge wenziwao. Na huu wizi unafanywa kutokana na tamaa binafsi, political ambitions na kutaka kuwa na mapesa ya kampeni na kuhudumia majimbo.

Tutatue chanzo cha tatizo na sio kukurupuka na kutibu viashiria

Hili Halipingiki... Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu

Ghasia na Migomo Bongo inaletwa na Viongozi wa serikali wenye uwezo mdogo wa kutatua matatuizom kwa njia ya majadiliano wakiamini UBABE, NGUVU YA VYOMBO VYA DOLA NA VITISHO ndiyo suluhisho kumbe wanaharibu nchi kabisa

Tunapataje maendeleo katika hali ambayo raia hawawezi kupata hata Panadol mahospitalini wanakufa kwa kukosa oxygen gas ambayo lita 1 ni sh 200 lakini VX V8 hazijawahi kukosa Petrol, wananchi hawawezi kuaford hata Chakula umeme maji kwao ni story

Kama haya madogo tumeshindwa hayo makubwa unayofikiria ni yapi? Unajua unanishangaza aiseeeeee.
 
Mkuu

naruhusiwa kutoa maoni yangu kama Mtanzania mwenye uchungu na Nchi hii
Makame mbona hizo mil 240 umezikazania sana? kuna nini hapa? Hoja yako ilikuw ani mahakama kutoheshimika saiz mil 240 au ndo Propaganda mloamua kuanzisha ili mtugombanishe? sisi hatutagombana kwa hili aisee. Mtuache wenyewe kama hatujaridhika tutasema wenyewe.. wewe sio msemaji wetu
 
Mimi sina Chama,

Mimi ni Raia mwema,

Ila ukija huu, kwa kweli NITAUUNGA MKONO KWA ASILIMIA ZOTE, hata uhai ;; hapo ndio nitasema, LIWALO NA LIWE!!!!!!!

Makame kwa nini huo mgomo juu ya tanesco usiuanzishe wewe?
 
Kuna maelezo yalikuwa hayajatimia ya CWT na Serikali.

Kwa kuwa Mahakama ni chombo cha Sheria kinacholenga kutoa HAKI; wamaziamuru pande zote mbili kukamilisha maelezo ili Mahakama itoe Shauri.

Mahakama, haijatoa hukumu; na itatoa Shauri baada ya kupokea maelezo hayo.

na shauri la Mahakama linaweza kuwa in favor of CWT.

Ila kwa kitendo walichokifanya cha kujichukulia sheria Mkononi kabla ya Mahakama kutoa shauri, sijui reaction ya Mahakama itakuwaje.

Nia yangu sio ku ku prove wrong, ila ni kujadili hii hali.

Inakuwaje mahakama inaomba mda tena baada ya kuwa imeshatoa hukumu na cheti kinachoonyesha usuluhishi umeshindikana? Jamani Huu siniuhuni wa wazi? Yani unahukumu halafu kesho unaendelea kusikiliza kesi? kama hukuwa na maelezo ya kutosha kwa nini utoe hukumu?

UHUNI KAMA HUU NDO UNAOUFANYA HUO MHIMILI WA DOLA KUONEKANA HAUNA MAANA NA KUDHARAULIWA NA WANANCHI. HAYA PROVE ME WRONG KWA HILI.
 
Kwa kuwa naona Mahakama inatoa maelekezo lakini wanayapinga. Au ndio chachu ya kusema nchi isitawalike?

  1. Madaktari --hawakuheshimu maamuzi halali ya mahakama;
  2. Walimu ----- wamesema hawatoheshimu.

kitendo cha kwenda kinyume na amri za mahakama sio ishara njema, na kitatufanya tuwe kama majahili. hatuna majadiliano, hatuna heshima, hatujui mamlaka wala hatuna ustaarabu.

Tuheshimu MAHAKAMA
Mahakama hazitaheshimiwa, wala hazistahili kuheshimika kwa sababu ya mfumo wa sasa, tukumbuke kuwa viongozi wa mahakama ni wateule wa serikali. Hapa ndipo tunapoona hitaji la kuwa na katiba mpya.
 
Tonnyalmeida

  1. Serikali na CWT waliamuriwa kwenda kwenye Kamati ya Usuluhishi na Mahakama. Wala Serikali haikumuita CWT kwenye hio Kamati, nadhani hukunielewa pale. Kamati ya usuluhishi inavyoelekea imeshindwa kumaliza mgogoro (kwa mujibu wa CWT). Hatua inayofuata ndio pande mbili ziende Mahakamani. Wakaenda, wakaambiwa wakamilishe maelezo yao ifikikapo Tarehe 31/07. CWT ikaitisha mgomo kabla ya kukamilisha kipengere hicho.
  2. Kukusu Court Injuction pia nishaitolea maelezo, labda hukusoma thread; kuwa ni IMPLIED kwamba pande hizo zimeagizwa kukamilisha maelezo. Hapo manake ni kwamba hakuna kuchukua uamuzi wowote kwa upande wowote mpaka mahakama itakapotoa shauri.
  3. Hivyo Kipengele chako cha tatu hakina mashiko

Nawasilisha

Makame unaona unavyojichanganya?
1: Hivi tangu lini serikali inalegal mandate ya kuita mwajiri wake mahakamani badala ya mahakama? au unamaanisha SERIKALI=MAHAKAMA, Na kama ndo hivi ndo mana unaona Mahakama inapoteza CRDIBILITYKwa Raia.
2: Nimekuwa nikikuliza kila mara na hutaki kunijibu sijui unafanya makusudi au ni bahati mbaya... unauhakika kuwa mahakama imezuia mgomo? kama ndivyo.. LETA CORT INJUCTION ILOTOLEWA NA HIYO MAHAKAMA NA KANA HUNA ACHA HIZO PROPAGANDA ZISIZOKUWA NA MASHIKO
3: Mahakama haikuheshimu ndo mana iliwaita tena wakati ilishatoa uamzi na ni mahakama ile ile na sio ya juu zaidi ya hiyo ilotoa maamzi. TANGU LINI MAHAKAMA INAENDELEA KUENDESHA KESI BAADA YA HUKUMU? NDO MANA INADHARAULIWA
 
Back
Top Bottom