Siku hizi ndoa hadi mimba, mimba ndo kigezo cha kuoana?

1. Hapa ndo wanaume tunadanyanyika..eti nina mimba yako tayari! Unamchukua unafunga nae arusi! Kumbe wapi..mtoto anazaliwa wa jamaa mwingine!!

2. Utajuaje kama mimba demu wako aliyobeba ni yako???

Mkulu mi naona hawa watengenezaji wa mashine zinazopima DNA wangejitahidi kutengeneza ambayo inaweza fanya vipimo hivyo hata wakati mtoto akiwa tumboni.

LOL!
 
Hili nimelishuhudia hivi karibuni kila harusi nayohudhuria zaidi ya tatu Bibi harusi tumbo ndi tena kuubwa,
Au huu ni utaratibu mpya hadi uhakikishe kitu kimenasa ndio utangaze ndoa dunia ya leo uongo umezidi??

5561d1250147892-siku-hizi-ndoa-hadi-mimba-dsc_29481.jpg

Mkuu si unajua katika soka mpira lazima utangulie mbele? Huwezi kucheza kama mpira bado uko nyuma yako....lazima uutangulize mbele mkuu...!
 
Kwa hiyo hakuna kuoana kwa kupendana wawili siku hizi, mpaka watu wawe guaranteed bonuses za watoto, au sio?

Na hapo hapo wengine wana advocate wazi kutia mimba kwa kutegana? is it any wonders ndoa zinavinjika kama nyumba za maboksi? Such low trickery! Mimi nikijua demu kanitegeshea nimtie mimba makusudi nimuoe hiyo ni guarantee kuwa sitamuoa.

What am I taklking about, I am not the marrying type anyway.

Ndoa ya kweli na mapenzi ya kweli yanatakiwa kuwapo regardless ya watoto.Hii mindset ni medieval kichizi, na kwa kifupi ni ya kibaguzi. Na kama watu wako katika hizi dini za Judeo-Christian philosophies hizi ndoa za kutiana mimba kwanza zina constitute a high degree of hipocrisy.
 
hata mi mwenyewe nikimzimia demu mkali sana, halafu naona analeta longolongo yani bado hajaamua vizuri nimuweke ndani, au wazazi wake wanaleta miyeyusho, dawa moja tu: NAMTUNDIKA MIMBA!
kwishney.

Onja onja unapata gonjwa itakuwaje wewe ndie umepata au umepatikana
 
Maadili siku hizi yameporomoka, nashangaa watu wazima wanatetea mimba kabla ya ndoa loh!!! Hili jambo mie sikubaliani nalo kabisa eti mfanye uasherati wenu na mimba juu ndio ndoa ifungwe. Kweli dunia ya sasa asilimia kubwa ya wanaume hawezi kuoa msichana bila kumegana, ambacho ni kinyume na maadili ya kwetu. Kutokana na mambo ya globalization watu sasa kumegana kama kawaida.
Ila hii tabia ya kumegana hadi mnatiana mimba na kwenda mbele altar huku mdada kitumbo kimejaa wala sio heshima mbele ya Mungu.
 
Wajisikiaje leo mrembo weye? Hebu naomba unieleze maana ya hayo maneno nloyatia wekundu hapo juu. Mnyaaazi Mungu na akubariki akujaze baraka tele.
 
Tena ni mbaya kabisa, hawa viongozi wa hizi dini zingine wamekengeuka kupitiliza kiwango kiasi cha kukubaliana na madhambi kama haya. MUNGU atusaidie.
 
Kuna jamaa yangu alioa..akaa na mke miaka 6 bila mtoto..kumbe yule binti aliwahi kubeba mimba mimba ya mtu mwingine akaitoa na kuharibu kizazi!

wanawake hawaaminiki siku hizi!
 
Wajisikiaje leo mrembo weye? Hebu naomba unieleze maana ya hayo maneno nloyatia wekundu hapo juu. Mnyaaazi Mungu na akubariki akujaze baraka tele.
Mie mzima mpendwa! Hayo maneno ni mmegano( mambo ya ndani ya kuta nne) kama ujuavyo kiswahili kinakua kila leo.
Nawe ubarikiwe.
 
Kuna jamaa yangu alioa..akaa na mke miaka 6 bila mtoto..kumbe yule binti aliwahi kubeba mimba mimba ya mtu mwingine akaitoa na kuharibu kizazi!

wanawake hawaaminiki siku hizi!

Kwani yeye alioa kwa kumpenda huyo binti au alioa ili apate watoto?
 
ni vizuri kwani unaweza kuoa alafu ukakuta mkeo hawezi kupata mimba au wewe mwenyewe huna uwezo wa kupata mtoto.na mtoto ni baraka kubwa sana kwenye ndoa.kwahio ni vizuri sana japokuwa ukatazwi kuoa kabla mpendwa wako ajapata mimba.
 
tatizo mabinti wa leo ABORTION ZIMEKUWA MINGI na zimewapelekea kuwa barrens.watoto wa kiume wa sasa lazima watest zali kwa hali na mali ndipo kwenu wake watoe mahali ili iwe halali,then kuserebuka mambo ya hululation LELELELELELELELELELELLEEEEEE! yanafuata.kinyume na hilo hapana bana!

Unaweza kuwa na point kubwa sana Geoff, lakini ukiangalia upande mwingine wa shilingi, unakuta akina kaka ndio wanawasukuma kina dada kutoa hizo mimba.Na Mungu anavyojua kulipa hapahapa duniani, mwanaume ambaye ama alilazimisha mwanamke wake atoe mimba au alikataa mtoto anakuja kujutia kitendo hicho .Anapokuja kufunga ndoa na kitu "fresh" basi hawapati cha mtoto wala nini!

Na isitoshe kwani mwanaume unaposhirikiana na mwanamke kufanya kitendo ujue kuna uwezekano wa kupata ujauzito hivyo ni bora wewe mwanaume ukajitahidi kutumia kinga dhidi ya mimba,magonjwa na hasa UKIMWI.
 
Mimba kabla ya ndoa inatokana na mwanamke kuwa na uhakika wa kuolewa hivyo kujiachia na mara kunasa......na yawezekana mipango ya harusi ikachukua muda kuakamilika na tumbo nalo linakua
 
Kuolewa just because una mimba, ni kufunga ndoa for a wrong reason. Oaneni only if mna mapenzi ya kweli na mko tayari kuwa mume na mke. Wanawake wengi wanao olewa sababu tu wana mimba ndoa nyingi hazidumu, either zinavunjika/ ugomvi kila siku au jamaa anakuwa na "small house" tena huyo bi.mdogo unakuta labda alikuwepo/wapenzi enzi hizo kabla hata huyo wife hajakutana nae.

Tatizo letu watanzania tunafunga ndoa kuridhishwa watu (familia/ndugu/rafiki), au kukomoa wapenzi wetu wa zamani, au kwa kutaka ufahari, au unaogopa watu watakusema umezaa nje ya ndoa, au kufuata mkumbo baada ya kuona kila mtu kaolewa/oa, au umri umesogea but maana halisi ya "kufunga ndoa" watu tunaisahau.
Afadhali usioe/kuolewa leo kuliko kupeana talaka kesho na watoto wako mgongoni hujui wataishi vipi. My advice ni kuwa; GET MARRIED FOR A RIGHT REASON AND WHEN YOUR READY.
 
Unaweza kuwa na point kubwa sana Geoff, lakini ukiangalia upande mwingine wa shilingi, unakuta akina kaka ndio wanawasukuma kina dada kutoa hizo mimba.Na Mungu anavyojua kulipa hapahapa duniani, mwanaume ambaye ama alilazimisha mwanamke wake atoe mimba au alikataa mtoto anakuja kujutia kitendo hicho .Anapokuja kufunga ndoa na kitu "fresh" basi hawapati cha mtoto wala nini!

Na isitoshe kwani mwanaume unaposhirikiana na mwanamke kufanya kitendo ujue kuna uwezekano wa kupata ujauzito hivyo ni bora wewe mwanaume ukajitahidi kutumia kinga dhidi ya mimba,magonjwa na hasa UKIMWI.

Hivi mwanamke ambaye hana kizazi huwa anapata siku zake?
 
Asilimia kubwa ni mmomonyoko wa maadili.
Kuna msemo wa kiswahili unaosema 'kuolewa/kuoa ni wajibu na watoto ni majaliwa ya Mungu'.
 
amani kwenu wana JF..
naomba mchango wenu ktk hii ishu
Imekua ni suala la kawaida kwa wapenzi kufunga ndoa baaba ya bibi harusi kupata ujauzito, sababu kubwa ni eti wana test kama wapo shwari. Hii inamaanisha kwamba, kama mwanamke hawezi kupata ujauzito basi uhusiano woa unakua matatani!,jamani hapa kuna mapenzi ya dhati kweli? na je huyo mtoto atakayepatika atakuwa ni wa nje ya ndoa au? Kwa mawazo yangu, nadhani watu wanatakiwa kufunga ndoa kwa sababu wanapendana kwa dhati na si vinginevyo!

pamoja!!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom