Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 607
Tujiulize swali fupi, kwani sie tunaotoa maoni hapa, haya maoni na mijadala hii kwa nini haikufanyika hicho kipindi cha nyuma? Je, nasi tulaumiwe kwa kukalia maoni hayo hadi leo hii?
Umenena!
Tujiulize swali fupi, kwani sie tunaotoa maoni hapa, haya maoni na mijadala hii kwa nini haikufanyika hicho kipindi cha nyuma? Je, nasi tulaumiwe kwa kukalia maoni hayo hadi leo hii?
Yote mnayosema ni ubatili mtupu! Sisi huku mitaani tunapeta tu, wakristo kwa waislamu tunajichanganya bila shida yoyote. Hao Maaskofu na Mashehe ni njaa zao tu zinawasumbua!
[/COLOR]
Wengine wetu hatukufurahishwa na tabia ya maaskofu ya kumtagza mtu kuwa ni chaguo la Mungu.Lakini wao walijua ni kwanini waliamua kufanya hivyo.Kwani nini sasa wamemgeuka? Jibu ni rahisi,walidhani ataendeleza yaleyale ya Nyerere aliyowaahidi wakrsitu kuwa atalipa kanisa fursa maalum(soma kitabu cha Padri John Sivalon cha Siasa za Tz na Kanisa Katoliki). Alipoingia madarakani yeye akajenga nchi ya wote badala ya kujenga kanisa,akaboresha maslahi ya madaktari na manesi hivyo baadhi yao wakaanza kuhama hospitali za kanisa kwenda serikalini,akaanzisha shule za kata zikaonekana ni tishio kwa shule za seminari,akataka kuondoa misamaha ya kodi kwa taasisi za kidni kwani wanazitumia vibaya.Hapo ndo walianza kumchukia lakini wakajificha kwenye kisingizio cha mahakama ya kadhi huku wakijua kuwa hata wakati wanamtangaza chaguo la Mungu kwenye ilani ya uchaguzi kilikuwepo.
Kwa mtazamo wako finyu unadhani kuwa maaskofu wamesoma kuliko mashekh,ni elimu gani unayozungumzia? Muislam hawi sheikh hadi awe amehitimu kiwango fulani cha elimu ya dini ya kiislamu.Kama walivyo maaskofu wengi wenye degree za theolojia pia wako mashekh wengi wenye degree za elimu ya kiislamu,wapo hadi maprofesa na madokta wa elimu ya kiislamu.
Suala sio jk kuwa ikulu kama muislamu suala ni kuona anapigwa vita na maaskofu hadi wameambukiza chuki hata kwa waumini wao kama wewe.Hili waislamu wote wanaliona waliosoma na wasiosoma alike
......... wewe hiyo hamna ! .......... mbingu na ardhi hutetemeka kwa kumwita "mtu" ni MUNGU !!!
Yote mnayosema ni ubatili mtupu! Sisi huku mitaani tunapeta tu, wakristo kwa waislamu tunajichanganya bila shida yoyote. Hao Maaskofu na Mashehe ni njaa zao tu zinawasumbua!
Lakini.. bado hujasema upande wa pili, Mashehe nao wafanye nini?
Kawni mwenzangu una kiwango gani cha elimu?Kumshika mkono fisadi na kumnadi kuwa panga la zamani makali yale yale
kumtetea Mkapa kwamba tumuache mzee wetu apumzike wakati wakristo kina Mpendazoe Kimaro walisimama kidete Mkapa awajibishwe
kujiuzuru Lowasa ni ajali ya kisiasa
Epa richmond tangold dowans iptl
Na madhaifu mengi yaliyo dhahiri
YOTE HAYO NI KWELI ANAPIGWA VITA NA MAASKOFU? au anajipiga vita mwenyewe hadi waumini wanaona madhaifu hayo labda wewe mpaka uambiwe na shehe hili zuri hili baya huna akili ya kupembua!
MBONA MNATUCHANGANYA?
Kwenye hili la maslahi ya kitaifa masheikh watoeni,kwenye maslahi ya waislamu pekee na dini yao..........count them in! Wao wanaamini shida walizonazo zinatokana na wao kuwa waislamu na kutokupewa haki sawa kwa kuwa wao ni waislamu na si kama watanzania as if shida zimegawanyika kutokana na dini au effect za ufisadi zinaenda kwa watu wa dini fulani tu.
Maaskofu tuko nao kwenye maslahi ya kitaifa na ya kujenga roho,sasa sioni wapi watakutana???wawe na sauti moja. kila mmoja ana priority na kufikia malengo yao kuna wanaotumia akili na busara na wapo wanaotumia hisia.:A S 39:
Mipishano ya mawazo at a manageable level huleta maendelea , hivyo JK awahi kuyaweka sawa haya makundi ya maaskofu na Mashehe/Imaam kabla mgogoro haujafika hatua ya pili (i.e unmanageable). Katika hatua hii ya awali naamini ataweza kupata suluhu ya kwanini kundi moja linawanyima haki zao wengine (kama ni kweli , maana kama ni hivyo hata JK anakosa hizo haki) etcKwenye hili la maslahi ya kitaifa masheikh watoeni,kwenye maslahi ya waislamu pekee na dini yao..........count them in! Wao wanaamini shida walizonazo zinatokana na wao kuwa waislamu na kutokupewa haki sawa kwa kuwa wao ni waislamu na si kama watanzania as if shida zimegawanyika kutokana na dini au effect za ufisadi zinaenda kwa watu wa dini fulani tu.
Maaskofu tuko nao kwenye maslahi ya kitaifa na ya kujenga roho,sasa sioni wapi watakutana???wawe na sauti moja. kila mmoja ana priority na kufikia malengo yao kuna wanaotumia akili na busara na wapo wanaotumia hisia.:A S 39:
ndugu zangu,
nimeisoma hii thread lakini nadhani kuna kitu bado sijaelewa vizuri. tukisema maaskofu tunajua ni kiongozi wa taasisi fulani katika dini za kikriso na ama anachaguliwa kidemokrasia au anateuliwa kwa vigezo fulani.
hawa mashehe ni kina nani? wanaongoza taasisi gani? wanapatikanaje? wanasomeaje huo ushehe? kama wanaongoza taasisi fulani je zinatambulika na serikali na jamii? je, inawezekana muislamu yoyote akavaa kanzu na barakashehe akajiita shehe, na tukalazimika kuchukulia kauli yake kwa uzito sawa na ile ya Pengo au Laiza?
DUUUUUU,
M.M.Mwanakijiji Kwa kweli nakuunga mkono 100 Kwa 100 Yote uliosema ni kweli hapa kuna mgongano wa mawazo baina ya Masheikh na Maaskofu.
Ili tuwaelewe na twende pamoja nao ni kweli wakae chini waelezane wapi kila mmoja alikosea na nini watanzania tunategemea kutoka kwao waelewe kuwa Dini ni imani lakini Amani bila Imani hakuna na ili tuwe na Imani thabiti ni vema wao wote wawe nalengo moja, sijafika Ulaya ila nasikia baadhi ya Majengo yaliyotumika kama nyumba zaibada yamegeuka kuwa Majumba ya starehe.
Hata hapa kwetu hilo siku moja litatokea pindi tu tukijua hawa jamaa wapo kwa maslahi yao na si Watanzania.
Tuungane kudai Maslahi ya Watanzania na si waislam wala wakristu.
M.M. MwanakijijiIli maaskofu wapate mahali pa kusimamia wanapoikosoa serikali ya Kikwete ni lazima kwanza waombe msamaha kwa ukimya wao wakati Watanzania wameuawa Pemba na Mwembechai; si kwa sababu Waislamu waliuawa bali kwa sababu wananchi wameuawa.
Uchambuzi wako mzuri Mwanakijiji lakini jiulize scandals za Kagonda, Richmond, Dowans, n.k. ziliwekwa hadaharani wakati wa utawala gani...maaskofu wangeota? Mauaji ya Pemba yalikuwa ya kisiasa kama ya Arusha, hayakuwa na sababu kwa maaskofu kuhusisha dini. Na isitoshe msingi wa kauli ya maaskofu haikutokana na sababu za waliouawa Arusha kuwa ni wakristo!!!!
Moja wapo ni hii hapa kama hutaki achaSOURCE !!!!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...oliki-walivyolaani-mauaji-pemba-2001-a-3.html
Huu utapiamlo wa udini utaifikisha wapi Tanzania? Viongozi wa kweli wa kidini hawaweki maslahi binafsi mbele, kinachoongelewa hapa ni ubinafsi tu hakuna dini, viongozi wa kweli wa kidini hukemea maovu bila kujali nani anaongoza, uraisi wa Kikwete unamnufaisha vipi muislamu wa kawaida? Watanzania wengi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha badala ya kuongelea masula ya kimsingi, tunakwepesha hoja na kuangelea mambo ambayo hayana maslahi kitaifa. Dini ina nafasi yake ndani ya jamii lakini ni hatari inapotumika kuendeleza maovu. Tuangalie mfano hai Tunisia waliomuondoa madarakani Beni Alli si waislamu bali watunisia waliopinga udhalimu wake. Dini na siasa haviendi pamoja, mashekhe na maaskofu/mapadri mnaotaka kujiingiza kwenye siasa vueni kanzu na majoho vinginevyo mtakuwa wanafiki.